Na Agnes Mwaijega, Dar es Salaam
KAMPUNI ya mawasiliano Zantel imefungua duka kwa wateja wanaotumia huduma ya Highlife jijini Dar es Saalam.Akizungumza katika sherehe za ufunguzi huo Dar es Saalam jana
mmoja wa wateja wa huduma hiyo, Bw Aggrey Marealle alisema kwa ufunguaji wa duka hilo Zantel imejenga jina kwenye mtandao wa kibiashara
"Sasa Zantel imekuwa mgawaji wa huduma za kimtandao kwa haraka nchini kote zinazorahisisha mawasiliano na shughuli za kibiashara," alisema Bw. Marealle
Alisema kutokana na ufunguzi wa duka hilo Zantel inatoa matumaini kwa wateja wote kuwa ipo kwa ajili kuhakikisha wanapata mahitaji ya kimawasliano yenye uhakika kwa haraka.
Aliongeza kuwa kufunguliwa kwa duka hilo inadhirishia jinsi Zantel inavyowathamini na kuwajali wateja wake.
Alisema alijiunga na huduma ya highlife Juni mwaka huu na anawadhihirishia Watanzania kuwa huduma ya Highlife ni mojawapo ya bidhaa bora nchini na inakidhi mahitaji ya kimasiliano na kibiashara.
No comments:
Post a Comment