19 November 2010

Wasomi watofautiana CHADEMA kumkataa Kikwete.

Na Gladness Mboma

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutomtambua Rais Jakaya Kikwete kama rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limechukua sura mpya baada ya
wasomi na wachambuzi wa mambo siasa kutoa maoni yao juu ya msimamo huo.

Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye mkutano wa Wanafalsafa katika nchi za Afrika Mashariki, Mhadhiri Mwandamizi wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye kwa sasa ni mwanasiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Profesa Wamba Dia Wamba alisema kuwa hakuna nchi yoyote Afrika ambayo haikosi malalamiko.

Prof. Wamba alisema kuwa haoni sababu ya CHADEMA kumpinga Rais Kikwete wakati walishaapa na kuingia bungeni.

"Huwezi kumpinga rais wakati umekula kiapo, kama walitaka kumpinga walitakiwa wasile kiapo kwanza, wanachokifanya kwa sasa ni makosa," alisema.

Alisema kuwa kutokana na hilo bunge linatakiwa kuwashughulikia na siyo rais, na kusisitiza kwamba walitakiwa kumpinga wakiwa nje ya bunge kabla ya kula kiapo na siyo kukubali kula kiapo na kisha kumpinga.

Prof. Wamba aliwataka watu wanaolalamika waangalie ukweli uko wapi na kuongeza kwamba wapo wanaofuata demokrasia ya kweli na pia wapo ambao hawaifuati.

Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Azaveli Lwaitama alisema viongozi wa Afrika wanatakiwa kukomaa waende mbele, kwamba wale wanaomkataa Rais Kikwete wana hisia za kimtazamo.

"Hiki ni kipindi cha kufikiri, na kuondokana na mambo ya jana, kufikiri kuwa yanaweza kuwa kama ya jana, tuachane na mambo ya hisia na kimtazamo, hakuna anayemkataa rais kisheria, huo ni mfumo wa hisia za kisiasa tu, mimi sioni kama kuna mgogoro wa kisiasa," alisema.

Akizungumzia uchaguzi mkuu wa mwaka huu, alisema kuwa ulikuwa na changamoto nyingi ambazo hazijawahi kutokea Tanzania kwa Watanzania wachache kujitokeza kupiga kura tofauti na miaka iliyopita.

"Nasema hivi kama ni mimi ndiye mtawala, ni lazima nifikirie mara mbili mbili ni kwa nini hali imekuwa hivi, inatisha na haijawahi kutokea, wengi walioenda kupiga kura ni vijana na wale wazee watu wazima hawakupiga kura kulikoni," alihoji.

Alisema kuwa ni lazima mtawala ajiulize imetokea nini, watu kususia kupiga kura na kwamba haijawahi kutokea katika Afrika.

Naye Mwenyekiti wa Chama Falsafa Tanzania (PHATA), Bw. Alex Manonga alisema kuwa nchi za Afrika Mashariki wamekuwa wategemezi, hawana mawazo huru na badala yake wanategemea wengine kwa mawazo.

Alisema kuwa mkutano huo ulioshirikisha maprofesa na waadhiri kutoka Afrika Mashariki utajadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzungumzia jinsi ambavyo wataondokana na utengemezi wa mawazo ya wengine.

26 comments:

  1. Naitwa Kara, Dodoma

    Ni ukweli usiopingika kwamba Chadema kukubali kuapa, kule bungeni na baadaye kukataa kuwa hawamtambui rais ni kiini macho, je hizo posho za kikao cha bunge walizosaini na kuchukua, huo sio wizi na ufisadi?

    ReplyDelete
  2. wewe kara unajua ufisadi nini?? na katiba inasemaje kuhusu bunge wabunge na rais,inasemaje juu ya haki za mwananchi,usidandie hoja.JIFUNZE KWANZA KABLA YA KUTOA MAONI,USIFIKIRI KWA KUTUMIA AKILI YA MTU MWINGINE FIKIRI KWA KUTUMIA AKILI YAKO,NA KAMA IMECHOKA MWOMBE MUNGU AKUSAIDIE.

    ReplyDelete
  3. Ni wizi mtupu kwa kukubali kutumia hela ya walipa kodi wa tanzania. wakati hawawakilishi kikamilifu waliowatuma. Wameapa kuilinda katiba ya Tanzania. Kama sio ufisadi kwa nini waliapa?

    ReplyDelete
  4. CHADEMA,mimi ni supporter na niko mikoanai,wapiga kura wengi hawawaelewi mnachafanya,wana hofu hamtawawakilisha ipasavyo,mmoja aliyewapa kura leo kaniambia mbona CHADEMA wanatuingiza choo cha kike,ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida kumuelimisha akaelewa mnchokifanya kwa sasa.

    ReplyDelete
  5. Ndugu watanzania kweli tunadanganyana au ni uelewa mdogo, CHADEMA wako sahihi kama hawako sahii toeni sababu kama wao walivyotoa msimamo wao. Katiba inasema utamtii Rais endapo ni halali sasa ndugu zangu ukiangalia vurugu zote za uchaguzi zinawapa ya kuwa hawakutendewa haki kwa mantiki hiyo yule Rais wa ukweli anaeongewa kwenye ile katiba hayupo na chokochoko zote ni tume ya uchaguzi. Sasa kama tume ipotayari ifuatili na itoe ripoti kwa wananchi kwa nini wanakaakimya.

    ReplyDelete
  6. WALICHOFANYA CHADEMA WAKO SAHIHI NA WALA HAWAJAVUNJA KANUNI WALA SHERIA ZA BUNGE,KUTOMSIKILIZA RAIS KIKWETE NI KUFIKISHA UJUMBE KWA WANANCHI NA MATAIFA MENGINE KUWA TUNAHITAJI KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,MFANO RAIS AKISHATANGAZWA HATAKIWI KUPINGWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI HATA KAMA AMEIBA KURA AU TUME IMECHAKACHUA MATOKEO,HIVYO TUNAHITAJI KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI.WENGINE MNATOA MAONI HAMJUI ACHENI USHABIKI NCHI HII NI YETU SOTE,MSIWE NA MAWAZO MGANDO.SAMMY LOTHY,MASWA,SHINYANGA

    ReplyDelete
  7. JK UMEZIBA KWA MWENZIYO KWAKO KUNAVUJA MBAYA MNO, UMEWEZA ZENJI HUKU BARA NI BARAA TUPU SASA UKITAKA KUFANIKIWA KOTEKOTE KAA NA SLAA MUMALIZE TOFAUTI ZENU.VINGINEVYO UTAKUWA UNAOKOA KWA JIRANI KWAKO KUNAUNGUA MOTO.SO WHICH IS WHICH,ANYWAY JK SINCE I KNOW YOU VERY WELL THAT YOU ARE HERO IN POLITICS, THEN THIS IS A TRIVIAL MATTER YOU WILL SETTLE IT IN AMICABLY WAY.

    ReplyDelete
  8. Wanachofanya Chadema ni mchezo wa kuigiza, na ndio maana mambo wanayoyafanya ni yakibinafsi,angalia kama sisi tuliokuwa Dodoma hawa watu wana pupa na madaraka,waliamuakuunda kambi ya upinzani peke yao bungeni utazani wao ndio wapinzani peke yao, lakini kwenye maslahi hawapingi,angalia logic iko wapi unaingia bungeni unaapa na unasema utalinda katiba ya jamuhuri ya muungano wa tanzania ambayo moja kwa moja unakubali utawala kwa ujumla alafu unatoka nje unasema unampinga Rais, huoni kuwa hufai weye?chadema niliwaona tangu mwanzo ni washari walichukua fomu ya Urahis kwa Possibility moja ya kushinda na wala sio kushindwa au kulingana.

    ReplyDelete
  9. Duniani kote,historia inaonyesha,wachache daima ndio huongoza dira ya ukombozi,ila huandamwa na vikwazo ndani ya safari ya ukombozi.Kuna msemo wa kitanzania unasema PANYA WENGI HAWACHIMBI SHIMO...!Kila wanachofanya CHADEMA mimi naona ndio dira ya ukombozi.Kwa mara ya kwanza Kikwete atakuwa ameonja aibu kimataifa...!Baada ya wabunge wa CHADEMA kumsusa ni aibu..!Watanzania hatuna budi kutoka darasa la kwanza la fikra.Sasa lazima tujitambuwe wapi tunaelekezwa kwa sababu sisi ni binadamu,tuna utashi na uthubutu.Tuache kuburuzwa kama mbuzi.Muda umefika wa kuamini kuwa ukombozi wa kweli utatoka UPINZANI.CHADEMA ni chama cha ukombozi...! Amina

    ReplyDelete
  10. Duniani kote,historia inaonyesha,wachache daima ndio huongoza dira ya ukombozi,ila huandamwa na vikwazo ndani ya safari ya ukombozi.Kuna msemo wa kitanzania unasema PANYA WENGI HAWACHIMBI SHIMO...! Wingi wa wabunge wa CCM hamna tija yoyote kwa Taifa. Ukuzaji viwanda,ukuzaji kilimo na kuendeleza Elimu ni kama wimbo tu sasa.Tumesikia tangia enzi hizo na hamna kinachoonekana.Kila wanachofanya CHADEMA mimi naona ndio dira ya ukombozi. Sera zao ni za kumkomboa Mtanzania,ambaye kila kukicha anazidi kua MASKINI. Ni laana au nini..! (MFUMUKO WA BEI...!MBONA HAJAFAFANUA..! VIJIJINI WATU WANA HALI MBAYA SANA KIMAISHA...!) Kwa mara ya kwanza Kikwete pamoja na washabiki wake atakuwa ameonja aibu kimataifa...!Baada ya wabunge wa CHADEMA kumsusa ni aibu..! Watanzania hatuna budi kutoka darasa la kwanza la fikra.Sasa lazima tujitambuwe wapi tunaelekezwa kwa sababu sisi ni binadamu,tuna utashi na uthubutu.Tuache kuburuzwa kama mbuzi.Muda umefika wa kuamini kuwa ukombozi wa kweli utatoka UPINZANI.CCM haina jipya.Hata hiyo hotuba dira ya Mheshimiwa ilikuwa karibu ipoteze fahamu watu wa vijijini..inakatisha tamaa kwa mtu wa maisha ya chini..! Sijui...! tuangalie yawezekana ndani ya CCM kuna muujiza unakuja...! CHADEMA ni chama cha ukombozi...! Amina

    ReplyDelete
  11. Huwezi ukaiba kura halafu ukataka watu wafumbate mikono bila kupinga. Ukweli ni kuwa mwizi haheshimiwi na ni lazima apingwe kwa nguvu zote ikiwa ni pamoja na kumuaibisha. Kikwete karibu Tanzania mpya wewe ni mwizi wa kura. Mwizi mwizi mwizi!

    ReplyDelete
  12. Mimi naona chadema wanajaribu mbinu ambazo ni old fashioned, wenziwao cuf walitumia hii hawakufanikiwa mambo yakaendelea. mpaka walipokubali kukaa chini na kuzungumza ndio ccm wakawasikiliza ila si kwa mbinu za kugomea bunge. Acheni hizo Chadema!!

    ReplyDelete
  13. Nimesoma maoni yote naona kuna kitu hakisemwi. Watu wanasema chadema wamefanya kitendo cha kijasiri. Sawa. Lakini wanapinga nini? sula ni kuwa je, ni kweli kura zimechakachuliwa? Kama ni kweli well-done chadema. Lakini kabla ya welldone, inabidi mtupe vielelezo watanzania kuonyesha nec imeiba kura za Slaa. Inaonyesha mnaunga mkono matokeo ya ubunge, mbona nako mmepata kura ndogo? Haingii akilini chama kilichopata viti 23 vya ubunge kikatoa rais kwa kushinda 70% (Mtikila alidai hivyo), kwa kushinda chama kilichopata viti 189. Mimi sielewi. Halafu tofauti ya kura kati ya Slaa na Kikwete ni kubwa mno. Tume ya uchaguzi ilitakiwa kufanya kazi kubwa kubadilisha hayo matokeo ambayo ingekuwa ni wazi rahisi kukamatika. Matatizo yaliyokuwa yanajitokeza Zanzibar ni kwa sababu Seif na marais aliogombea nao walikuwa wanazidiana kwa kura ndogo sana. Hata uchaguzi wa mwaka huu tumeona hivyo. Ndiyo maana chadema watoe hizo hesabu zao zilinganishwe ili tuondoe ushabiki. Jamani nchi yetu ina mambo mengi ya kufanya. Nyie mnaoshabikia hicho kitendo cha chadema kutomtambua rais mna ushaidi wa kura kuchakachuliwa? Nadhani hili ndilo swala hapa. Kwa sababu chadema haisusii uchaguzi kwa sababu ya katiba ni mbaya. Kama ni hivyo ni katiba hiyo hiyo iliyotumika kuwachagua pia wabunge. Kinachoongelewa ni kuwa Slaa kaibiwa kura, je ni kweli? Hesabu zangu zinanionyesha kuwa si kweli. Chadema toeni vielelezo. Sababu namba za kila kituo toka mikoani zipo, ambazo wakala wenu walitia sahihi. Sasa hizo namba, za Chadema, na za NEC, zilinganishwe ili tuone nani kaibiwa kura na ni ngapi. Baada ya hapo nitaona kama niwapongeze wabunge wa chadema au la kwa kitendo chao cha kutomtambua rais.

    ReplyDelete
  14. WATANZANIA TUMEKUWA WAGUMU KUELEWA,HASA PALE JAMBO LINAPOFANYWA KTK MTAZAMO WA KIMATAIFA...KUMSUSIA RAIS NI JAMBO KUBWA SANA KWA KUTUMA UJUMBE KIMATAIFA...MIMI NIPO HAPA NEW YORK KWENYE MJI UNAOITWA BUFFALO..WATU WENGI WANAOJUA MAMBO YA KIMATAIFA WANASEMA TANZANIA IS UNDER POLITICAL CRISIS,HII IMETOKANA NA TAARIFA ZA CHAMA CHA UPINZANI KUGOMEA KUSIKIA HOTUMA YA RAIS.TO THOSE WHO DON'T HAVE ABILITY TO MEDITATE THINGS THEY THINK IT'S TO WASTE TIME.BUT THAT IS THE WAY TO SEND A MESSAGE TO OTHER NATIONS.

    ReplyDelete
  15. Unajua watu wanakuwa wanfiki. Wanazunguka ukweli na kuilaumu Chadema. Kama wangekuwa wako serious na wapenda maendeleo wangemtuhumu kwanza aliyeiba kura na tume ilyomweka madarakani sio kuwalaumu walioibiwa. Hivi nyinyi mtu amekuibia, badala ya kusaidia kumuaibisha mnawasakama walioibiwa. acheni unafiki aisee

    ReplyDelete
  16. KWAKO ALOYCE,
    Ujumbe wako ni mzuri mno lakini sina hakika kuwa hata kama wakitoa ushahidi wa kura walizopata sijui kama utakubaliana nao kwa maana maneno yako yanaonyesha kuwa you have already made up your mind kwamba chadema haikushinda. unatumia kura za wabunge lakini kumbuka kuwa hata kura za wabunge pia unazotumia zilichakachuliwa ushahidi mzuri ni Vunjo kwa mrema ambapo Msimamizi wa uchaguzi alimuongezea mgombea wa CCM kura elfu sita hiyo ni zaidi ya asilimia kumi ya kura zote zilizopigwa. yeye anaita ni makosa lakini sisi tunaita ni wizi wa kura wa wazi, huko geita slaa alipunguziwa kuwa 18000 na baadaye kurekebishwa na Tume hiyo hiyo na kama waliweza kufanya hivyo kwenye jimbo moja wanashindwaje kufanya na maeneo mengine??.

    ReplyDelete
  17. Maaaneeenoo hayooooo KIKWETE,,,,,,???????

    ReplyDelete
  18. It is really absurd when you here people who have to school to allege that votes were chakachuliwad. Lts be serious, hebu sikilizeni. Kila chama kilikuwa na mawakala katika vituo vya kura. Hawa walishiriki kuhesabu kura zao na kusaini forms za matokeo. Tume ilichapisha kila matokeo kwa kila jimbo, sasa Chadema toeni takwimu zenu tuone sio kusema kuwa kura zimeibiwa tupeni Data.
    Au ni vile Dr. Slaa amezoea kuiba ndio maana anafikiri kila mtu ni mwizi...tusimsikilize mwizi wa wake za watu atatupeleka pabaya huyo

    ReplyDelete
  19. sasa wewe hujui kuargue wizi wa mwanamke na wizi wa kura vina mahusiano gani? acha ujinga kama huna point usichangie, wewe unataka tu kumdhalilisha slaa kwa kuwa huju usemalo. CCM wameiba kura na kila mtu mweny akili analijua hilo, embu imagine kwenye jimbo la segerea Mpendazoe alishinda tena kwa Kishindo, eti wanathubutu kumpa Mahanga.Kikwete ameshinda ushindi wa aibu aibu! shame upon his face, watu milioni 19, walitakiwa wapige kura, lakini wamejitokeza wachache hata milion 9 haikufika, ajiulize ni kwa nini hii itokee, watu wamechoka na uongozi wake , fikra zake ni ndogo, ana upeo mdogo huyu yeye akakae na waswahili wenzake akacheze bao huko Bagamoyo,halafu anazungumzia udini wakati yeye ndo anayeleta udini.Kila kukicha anachadua waislam wenzake ambao hata sifa hawana, angalia kwenye balozi zetu wamejaa Maimuna kibao, HATUKUBALI SISI WATU TUMEAMKA

    ReplyDelete
  20. Nashukuru ndugu yangu wewe unayejiita anonymous kwa kunielewesha. Ndiyo maana tunawaambia chadema leteni matokeo mliyonayo tuone makosa kama haya yamekuwa kiasi gani ili sisi wananchi nasi tuone mkweli ni nani. Inabidi tukumbuke kitu kimoja. Katika process yoyote kuna makosa. Hakuna mfumo wowote usio na makosa. Hata hapa Marekani kwa mfano (mimi naishi Chicago) kulikuwa na matatizo kwenye kura za ugavana hapa Illinois ambapo ilibidi ipite wiki moja kabla ya kura kutangazwa. Na wenzetu wamebobea kuliko sisi katika technologia. Tume ya kuchaguzi hata iwe huru kiasi gani lazima kutakuwa na matatizo ya kiutendaji. Sasa inabidi tutumie akili tulizojaliwa na Mungu kujiuliza kama matatizo yalikuwa ni sehemu ya uchakachuaji au ni makosa ya kibinadamu? Mimi sikatai kulikuwa na kasoro nyingi katika prosess ya uchaguzi, lakini hizo kasoro zilijitokeza ili kuiba kura? mimi sijui na nafikiri hata wewe anonymous huna uhakika. Kutumia matatizo yaliyojitokeza katika jimbo moja au mawili kama kielelezo cha wizi wa kura siyo sahihi. Chadema walete vielelezo vyao kama tofauti itaonekana hata kwenye 10% ya vituo vyote nchini hapo tutasema kuna kitu kimefanyika. Kwa sababu chadema walikiwa na wakala kila kituo ambaye asaini fomu za matokeo. Sasa inabidi matokeo yaliyotangazwa na NEC, matokeo ambayo Chadema wanadai wanayo, na yale vituoni yaliyowekewa sahihi na mawakala wao vilinganishwe. Nina uhakika matokeo ya vituoni na yale ya NEC yanajulikana, ambayo hatuna ni yale ya chadema ambayo sisi hatuna, wayatoe. Bila ya kufanya hivi chadema wanyamaze hatutawaelewa. Halafu ukiangalia tofauti ya kura za ccm kwa wabunge na rais ni kubwa mno kuweza kusema tofauti hiyo imetokana na kuchakachuliwa. Mimi siyo mwana ccm lakin naunga mkono serikali yoyote inayowekwa madarakani. Unapoamua kumkataa rais lazima uwe na ushahidi kweli kweli. La sivyo sisi wantanzania hatutawaelewa nyinyi mnaounga mkono chadema. Naomba unisamehe ndugu anonymous mimi ni njia yangu ya kufikiri namna hii. Huwa napenda kuanalyze facts. Huwa siishi kwa hisia tu. So far sioni facts zinazoonyesa Kikwete kaiba kura.

    ReplyDelete
  21. Mh. Rais. Nafikiri unafurahia kwakusema hata wakitoka rais wao ni yuleyule!!! huku nderemo za wabunge wapya zikirindima. Nakusihi Hakuna aliye hubiri udini na kama yupo basi hotuba yake irudiwe kuonyeshwa kwy TV kwani zote zilionekana dhahiri. Unafurahia hao chadema kufikisha ujumbe ila unashindwa kutambua madhara yake/? Unasahau kwamba mwanzo wa moto ni cheche???. Umepata takwimu za wangapi wanaunga mkono kitendo hicho??. Ama kweli kusoma siyo kujua. 4 sure CCM unaichimbia kaburi 2015.

    ReplyDelete
  22. CCM NA ENZI ZA UFARAO.
    Kwa wale wanaopenda kusoma maandiko au historia ni wazi wanafahamu Dhama za FARAO.Kiongozi ambae alikuwa amelewa mawazo ya kishetani..! Kwa maana uongozi wake ulijaa dhuluma,uonevu,na kila aina ya dhambi.Ndipo upinzani(Waizarael) walipotaka ukombozi! Mungu alimvika Farao ugumu si kwamba wapinzani(Waizarael) wapate tabu..alikuwa na kusudio...Apigwe mapigo yale makuu na apate anguko la utawala wake dhalimu...!! CCM. na wapenzi wake ndio MAFARAO katika nchi yetu tukufu Tanzania. Ni wazi kabisa wameshaanza kupata yale mapigo ya Mungu. Tukianzia anguko kwenye uchaguzi,CHADEMA kususia kuapishwa kwa rais na Wazir Mkuu na pigo la tatu ni aibu ya historia pale tena CHADEMA waliposusia hotuba ya rais,atake asitake HANA HESHIMA tena kimataifa.Watampokea,watamsikiliza lakini moyoni watakuwa wana lao jambo..! CCM wametuaibisha kimataifa, kwa sababu wao ndio chanzo au msingi wa yote haya.
    Ni tayari kuna mapigo hayo matatu yawezekana kuna mengine yanakuja, ili azimio la Mungu litimie la kuwaletea WATANZANIA (Waizarael mbadala)TUMAINI,HESHIMA,na UKOMBOZI wa KWELI.
    CCM si chama kuleta matumaini na maisha bora kwa Mtanzania,Tusubiri ANGUKO LAO...! kwa maana Yale MAPIGO ya Mungu bado yangali yanakuja... ni karibu tu.
    Mungu ibariki CHADEMA na wale wote wenye MAPENZI MEMA.
    UFARAO NDANI YA CCM...Unakaribia kuanguka. Yatabaki MAPIRAMIDI kama historia.

    ReplyDelete
  23. Anony nov 20: 2:47, kumbe ni udini ndio unaowasumbua? Huo ulokole wenu utawafikisha pabaya na watu watakimbia chama chenu? Hebu nikuulize vizuri ni Mungu yupi unayemzungumzia? Maana kama kumuasi huyo Mungu mbona mumemuasi kwa kuvunja ndoa ya mtu na kukengeuka maandiko yaliyosema aliyekiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe? Na vile vile kukaa na wanawake bila kufunga ndoa kanisani na kuzaa nao watoto nayo hiyo je? Na kufanya biashara ya kuuza mapombe na muziki, ni Mungu yupi huyo Mungu wenu? Maana ukute unazungumzia Mungu mwingine mwenye kukubaliana na hayo ya mapombe, miziki na mambo ya kuwa na vimada na kuvunja ndoa za watu. Otherwise kama ni Mungu huyu huyu wa haki, basi asingeliweza kuwasimamia na kuwapa uongozi wa kutawala wengine hata kama mlimuomba na kumlilia. Mlihitaji toba ya nguvu kwanza ndio mumtegemee Mungu kuwasimamia lakini kufanya ya shetani kisha kudai Mungu wa Yehova atawasimamia ni unafiki

    ReplyDelete
  24. Wanaobisha kuwa chadema hawajaibiwa kura si wapiga kura au ni jamaa wa wachakachuaji(mafisadi). Hivi Lewis Makame, takukuru, wakuu wa mikoa na wilaya,mkuu wa jeshi la polisi nk wataachaje kujenga mazingira ya kuiba kura ili aliyewapa vyeo aendelee kutawala? Wanauhakika gani kama angepita mpinzani angewaacha waendelee kula? La hasha, hao wanaakiri zao timamu, daftari la wapiga kura lilivurugwa makusudi ili vijana wengi wenye mtizamo wa kimapinduzi wasipige kura. Aloyce, takukuru walikuwa rikizo wakati Riziwan anagawa pesa kama njugu Kahama na sehemu zingine, Chadema inaendeshwa na wasomi na kamwe hawakurupuki bila kuwa na ushahidi, hivi ushahidi waupeleke wapi wakati jaji mkuu kawekwa pale na jamaa. Aloyce, Maige alichoma masanduku ya kura kagongwa nk na aliulaumu uongozi wa mgodi wa bulyanhulu kwa kutowa basi kupeleka wafanyakazi wake (wanamapinduzi)kwenda kupiga kura, muulize kama hajapiga simu, mimi binafsi simtambuwi huyo jamaa yenu kikwete

    ReplyDelete
  25. jamani noamba tusiwe majuha kwa kusikiliza hoja kuwa Slaa au CHADEMA wameiba mke,haingii akilini kuwa mwanamke anaibiwa?mwanamke haibwi?ningeunga hoja hii mkono iwapo ingekuwa kabakwa?!huyo dada ni mtu mzima na inatosha kabisa alifanya uamuzi wake, mbona hatushangai inakuwaje huyo mumewe (mahimbo) akimbiwe na mkewe for 2 years awe kimya halafu aibuke wakati wa kampeni?Mr.Mahimbo aibu imempata yeye na CCM maana alijua kuwa ingekuwa ni gain kwake, ila siye wenye akili tumefahamu kuwa alifisadiwa na CCM ili alopoke ila tunamfahamu mahimbo hela yote aliyonunuliwa na CCM ameimaliza kwenye pombe pale MAEDA Pub Mwenge. Na tunakujua Mahimbo since ukiwa Tambaza sec ulikuwa unapenda vitu vidogo ambavyo umeviendekeza hadi ukaicha familia.....jamani mwanamke wa kiafrika haibwi ndugu zangu, wana utashi wao.....hivi mbona Kikwete hammsemi?na vimada vyake?tunajua na tufahamu yeye ni mwizi wa kila kitu, au tuje na orodha ya vimada vyake?

    ReplyDelete
  26. CCM na enzi ya Farao....mchangiaji amesahau kutaja pigo la 4 ambalo linaloijia CCM soon...noana CCM watajichanganya watakapoleta azimio lao fake (kwa kutumia wingi wao bungeni ili kuwaondoa CHADEMA bungeni. Hatuna wasiwasi CHADEMA tutarudisha hoja kwa wananchi - kwa kuwa wananchi ni welevu basi naamini watahukumu vizuri...Mungu ibari Tanzania, Mungu ibariki CHADEMA, tumefahamu CCM wapo kwa ajili yao wenyewe na mabwana zao akina Chenge, Rostam, Lowassa, na vibarua wao Kikwetwe na Makamba

    ReplyDelete