Na Mwali Ibrahim
WACHEZAJI na viongozi wa judo, leo watahudhuria semina ya mafunzo ya mchezo huo, iliyoandaliwa na ubalozi wa Japan Tanzania ambayo itatolewa na wakufunzi
kutoka nchini humo katika Ukumbi wa Don Bosco, Dar es Salaam.
Wakufunzi watakaoendesha semina hiyo ni Akira Kai, Yoshiharu Makishi, Tomoya Hira na Yoshihisa Ishikawa ambao watatoa mafunzo hayo ya jinsi ya kukuza na kuendeleza mchezo huo, ikiwa ni pamoja na mbinu mbalimbali.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Judo Tanzania (JATA), Kashinde Shaban alisema mafunzo hayo yatahudhuriwa na wachezaji wa judo wa Tanzania Bara na Zanzibar walioshiriki michuano ya wazi yaliyoanza Dar es Salaam jana na pia wadau wengine wa mchezo huo wanakaribishwa.
Alisema mashindano yaliyoanza jana katika Ukumbi wa Don Bosco yanashirikisha wachezaji 32, ambao wanatoka 16 wanatoka Tanzania Bara na wengine wa Zanzibar.
Shaban alisema katika mashindano ya jana yalikutanisha wa Bara za Visiwani kwa wachezaji mmoja mmoja kila upende ambapo Zanzibar walitamba katika mzunguko wa kwanza baada wachezaji 13 kutoka na ushindi.
No comments:
Post a Comment