19 November 2010

Wachezaji Kili Stars kupewa vyandarua.

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania limepanga kugawa chandarua kwa kila mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara ili wavitumie wakiwa kambini wakati
wa michuano ya Chalenji itakapokuwa ikifanyika ili kujikinga na malaria.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Sunday Kayuni alisema kuwa wameamua kugawa vyandarua hivyo ili kupiga vita ugonjwa wa malaria kupitia mpango wa 'Tushirikiane kutokomeza Malaria'.

TFF imeamua kupiga vita malaria kwa kushirikiana na United Against Malaria (UAM), ili kutokomeza ugonjwa huo ambao huua zaidi watoto wenye umri kuanzia siku moja hadi miaka mitano pamoja na wamama wajazito.

Katika mashindano ya Chalenji ambayo yanatarajia kuanza Novemba 27, mwaka huu Tanzania bara imepangwa kufungua dimba na Zambia 'Chipolopolo' wakiwa kundi A.

Timu nyingine zilizopo kund A ni Burundu na Somalia, huku Zanzibar ikiwa kundi B na timu za Rwanda, Ivory Coast na Sudan.

Kundi C likiwa na timu za Uganda, Kenya, Malawi na Ethiopia.

No comments:

Post a Comment