19 November 2010

Argentina yailaza Brazil 1-0.

DOHA, Falme za Kiarabu

WAKATI Argentina iliilaza Brazil bao 1-0, Uingereza jana ilipata kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Ufaransa ikiwa ni miongoni mwa mechi za kimataifa za kirafiki za
soka zilizofanyika jana, sehemu mbalimbali duniani.

Uingereza ikiwa katika Uwanja wa Wembley, ilichapwa na Ufaransa huku mshambuliaji wake Andy Carroll, akicheza vizuri katika mechi yake ya kwanza kwenye kikosi hicho.

Ufaransa iliyoonekana kutawala katika mechi hiyo, ilipata magoli yake kupitia kwa Karim Benzema na  Mathieu Valbuena, huku bao la Uingereza likiwekwa kimiani na mchezjai aliyetokea benchi, Peter Crouch ikiwa ni goli lake la 22 katika timu hiyo.

Mchezaji bora wa mwaka wa Dunia,  Lionel Messi alifunga bao pekee ambalo liliifanya Argentina kuibuka mshindi dhidi ya mahasimu wao Brazil katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Doha, Falme za Kiarabu, huo ulikuwa ni ushindi wao wa kwanza katika kipindi cha miaka mitano.

Messi anayechezea Barcelona ya  Hispania, alifunga goli hilo katika dakika za mwisho, alipata pasi nzuri kutoka kwa Ezequiel Lavezzi kisha akawalamba chenga walinzi wanne wa Brazil na kukwamisha mpira kimiani.

Mchezaji wa AC Milan Ronaldinho, alikuwemo katika kikosi cha Brazil kwa mara ya kwanza, baada ya kupita miezi 19, alicheza vizuri lakini alishindwa kufunga goli, huku kocha wa Argentina, Sergio Romero akiondoka na fuaraha kwa ushindi wa Argentina.

Ureno ililipa kisasi cha kutolewa katika Kombe la Dunia dhidi ya Hispania, baada ya kuwafunga majirani zao mabao 4-0, katika mechi iliyochezwa mjini Lisbon.

Mabao ya Jorge Carlos Martins, mlinzi wa Hispania Sergio Ramos alijifunga, huku mabao ya Helder Postiga na Hugo Almeida ndiyo yaliifanya ureno kuondoka na kicheko uwanjani.

Ubelgiji nayo ilipata ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Russia katika mechi iliyopigwa Voronezh.

Romelu Lukaku ndiye aliyeleta tofaunti kati ya timu hizo mbili kwa kufunga goli dakika ya pili, baada ya Eden Hazard kumchenga kipa wa Russia, Igor Akinfeev na kumpasia mfungaji.

Lukaku tena alifunga bao la pili zikiwa zimesalia dakika 17 mchezo kumalizika.

No comments:

Post a Comment