*Ni wakutomtambua Rais Kikwete.
*Awaita Mbowe, Zitto wateta.
Na John Daniel, Dodoma.
SPIKA wa Bunge Bi. Anne Makinda, amewashauri wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufuta msimamo wao wa kutoitambua Serikali na
Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa msimamo huo unaweza kuwagharimu katika uwakilishi na utumishi wao ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi usiku baada ya kukabidhi majukumu yake kwa Naibu Spika, Bw. Job Ndugai, Bi. Makinda alisema baada ya kupata taarifa za wabunge wa CHADEMA kutoitambua Serikali na Rais Kikwete aliwaita viongozi wa wabunge hao, Bw. Freeman Mbowe na Zitto Kabwe ofisini kwake kuwapa ushauri wa kufuta msimamo huo kwa kuwa madhara yake ni makubwa kwao kiutendaji.
"Unajua usipoitambua serikali maana yake ni kwamba huwezi kufanya kazi yoyote ndani ya bunge, zipo kamati nyingi, kuna nafasi mbalimbali za uwakishi wa wabunge katika taasisi, mashirika, vyuo na nje ya nchi sasa kama hawaitambui serikali maana yake hawawezi kuwakilisha katika nafsi yoyote.
Nimewashauri wafikirie upya, wakumbuke hata CUF kule Zanzibar waliwahi kufanya hivyo na katika kipindi chote cha miaka mitatu hawakuwakilisha katika nafasi yoyote na walikaa kana kwamba hawapo, kwa maana hiyo hawawatendei haki wananchi waliowachagua," alisema Bi. Makinda.
Alisema alifikia uamuzi wa kukutana na viongozi hao kuwapa ushauri kwa kuwa hakuna sababu ya mbunge kudai kuwa hatambui serikali iliyopo madarakani wakati anahudhuria vikao vyote vya bunge linaloongozwa na kuendeshwa na serikali hiyo hiyo anayodai si halali.
Alisema tayari wabunge hao wa CHADEMA wameapa na kuahidi kutii na kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoitambua na na kutii serikali iliyopo mdarakani na kuongeza kuwa kutomtambua rais ni kupoteza muda au kutafuta umaarufu wa kisiasa.
Alisema baada ya Uchaguzi Mkuu na matokeo yote kutangazwa hadharani kazi kubwa ya wabunge sasa ni kuacha malumbano ya kisiasa na kuungana pamoja bila kujali itikadi kutatua kero za wananchi na kutekeleza ahadi mbalimbali walizotoa wakati wa kampeni.
"Niliwashauri kwa kuwa malumbano hayo hayatatufikisha popote, pengine watu wanajitafutia tu umaarufu, lakini kazi ya mbunge ni kuwakilisha wananchi, sasa ukibaki kuimba tu hatumtabui Rais haisadii," alisema Bi. Makinda.
Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana, Bw. Mbowe alikiri kukutana na Spika Makinda kufanya mazungumzo lakini si kwamba waliitwa kujadiliana kuhusu kubadilisha msimamo wao.
"Kwanza sisi hatujaitwa na Spika wala sijui suala la yeye kutushauri kitu kama hicho. Sikiliza nikuambie, hatukwenda bungeni kutafuta vyeo wala manufaa yoyote, mimi mwenyewe nimeendesha siasa kwa miaka 20 bila kupata manufaa yoyote, hatuwezi kununua vyeo kwa kumtambua rais.
"Unajua huku Bara hatujawahi kupata 'Political Pressure'
(shinikizo la kisiasa), wamezoea tu mambo yanaenda vibaya tunakubali haya bora liende, sasa hatuwezi kuendelea hivyo, kule Zanzibar walipata 'Political Pressure' ndio maana leo kuna serikali ya Umoja wa Kitaifa, usifikiri kwamba ule muundo unapendwa na CCM, wamelazimishwa na 'Political Pressure' baada ya kuona hali si shwari," alisema Bw. Mbowe.
Alisema wao kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo, njia pekee ya kueleza masikitiko yao kwa njia ya demokrasi ni kutoa tamko kama walivyotoa juzi ya kutoitambua serikali kwa kuwa katiba iliyopo sasa inawanyima haki ya kufanya jambo lolote zaidi ya hapo.
"Kama ukiibiwa kwenye ubunge unaweza kufungua kesi na mahakama ikatoa hukumu ukapata haki yako, lakini kwa upande wa urasi Jaji Lewis Makame (Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi) akishatangaza mshindi awe ndiye au siye basi, hauna nafasi ya kukata rufaa wala kwenda popote sasa njia pekee tunayoweza kutumia ni kutoa tamko kuonesha kile tunachokiamini, tunahitaji tu ukweli si kukubali kirahisi rahisi,"alisema Bw. Mbowe.
Alisema yeye pamoja na msaidizi wake Bw. Kabwe pamoja na Mnadhimu wao Bw. Tundu Lissu, walimtafuta Spika Makinda kwa kutaka ufafanuzi kuhusu kanuni za Bunge na kwamba hawakuzungumzia suala la msimamo wao kama ilivyoelezwa na kiongozi huyo wa shughuli za Bunge.
Alipoulizwa msimamo wao kama watapewa ushauri huo alisema wao kama CHADEMA wameacha milango wazi kwa mtu yeyote kuwapa ushauri na kwamba msimamo wao utatokana na aina ya ushauri na hoja zitakazotokana na ushauri huo.
"Sisi hatujafunga milango kupokea ushauri wa mtu yeyote kuhusu msimamo wetu, tutapokea na kuufanyia kazi ushauri, lakini kwa sasa hatuwezi kusema eti kutomtambua Rais sasa wabunge wetu wasikae bungeni hapana,'alisema Bw. Mbowe.
Mimi Naitwa John Mayala (Biharamulo).
ReplyDeleteTatizo la Upinzani Tanzania bado ni kubwa sana hasa pale ambapo vyama mseto kushindana na chama kimoja chenye nguvu, Ushauri wangu ni vyama hivyo vya upinzani kujiunga na kuunda chama kimoja tu, ikiwezekana Tanzania nzima tuwe na vyama vya siasa viwili tu.
Asante.
Hapa kuna tatizo la kisheria,kimaadili,kinchi na kivyama.Kiapo cha utii kinawazuia CHADEMA kuonyesha msimamo wao juu ya Rais na Serikali yake anayoendelea kuiunda? Je,CHADEMA wanawakosea heshima watanzania kama Spika Makinda anavyodai? Je,kweli CHADEMA hawataruhusiwa kushiriki kwenye uongozi wowote,hata ule wa Kamati za Kudumu za Bunge? Nani yuko sahihi:CHADEMA au Makinda? Je,hii itabomoa au kujenga CHADEMA au/na CCM?
ReplyDeleteHivi kumbe bunge linaongozwa na serkali,au makina kakosea.Halafu kumbe anawashauri Chadema waache msimamo wao ili wapate vyeo,ebu ona sasa,huyo ndiye spika wetu,tumeshaona mapema kabisa alivyo na hoja finyu.kwa hiyo heri udhulumiwe haki yako halafu uponzwe kwa cheo.Kama chadema wanahitaji ushauri na hoja kuhusu msimamo wao,si kama alivyoshauri huyu mama,tena ana kauli zisizomkomboa mtanzania.wanasema... hata mpumbavu akinyamaza kimya uhesabiwa hekima..Ni heri asingesema maana tumejua mtazamo wake kuhusu bunge,kwamba ni mahali pa namna gani.mtazamo ambao si sahihi.
ReplyDeletemimi nadhani CHADEMA wako sahihi kupinga ushindi wa Rais Kikwete kwa kuwa hawana mahali pengine popote pa kueleza hisia zao zaidi ya UMMA wa WATANZANIA.
ReplyDeleteVyombo vya sheria vinamlinda Rais akishaapishwa huwezi kufanya chochote. Suluhisho la tatizo hilo ni kufanyia marekebisho kama siyo kubadili KATIBA ya nchi ili kuruhusu demokrasia ya kweli na haki za Vyama vya upinzani na wanachi kwa ujumla
Hili naunga mkono kabisa uamuzi wa CHADEMA kutotambua uongozi/uraisi wa kikwete. Maana haki haipatikana kwa mafisadi, ukitaka haki ipatikane basi mageuzi lazima yatokee. Nadhani muda wa CCM umekwisha kabisa, watachakachua mpaka lini? huu ni mwisho wa kuchakachua kura za watanzania. Safari hii CCM wanajitengenezea kitanzi wenyewe na watajinyongo muda siyo mrefu.
ReplyDeleteLolote wanalofanya CHADEMA sasa wazingatie mambo kadhaa, ikiwemo, kama ni jambo la kuwajenga au kuwabomoa, nini matakwa ya waliowapa uwakilishi, hatma ya upinzani bungeni, n.k
ReplyDeletekazeni uzi fisi hawezi kutema mfupa bila kupigwa kibao
ReplyDeleteCHADEMA naona wanatuchanya tu.Kama kweli hawatambui serikali ya JK wangekuwa waungwana kwetu hata Bungeni wasiende hapo tungewaelewa..Hapa wanampoza tu Dr.Slaa lakini wao wanakula posho za Bungeni tu.. Dr.Slaa pole kwa kutoswa na jaama zako wa CHADEMA vumilia miaka 5 siyo mingi utapata tena Ubenge wako kama kawaida.Urais wagombee wengine hata ZITTO naye hajaribu.
ReplyDeleteMimi ni yule yule Hafidh kutoka visiwa vya amani - Zanzibar. ningependa kuchangia katika suala zima la msimamo wa Chadema wa kutoitambua Serikali ya Rais Kikwete.
ReplyDelete1)Kwanza na cha msingi Chadema wasiache kuhudhuria vikao vya Bunge hata kama wanamtazamo hasi, wajenge hoja madhubuti na pakutetea watetee wananchi kwa ujumla pale wanapoona mambo hayaendi mazuri katika serikali hiyo hiyo iliopo madarakani kwa sababu wakiacha kutoa michango yao inamana kua kile anachokiona Serikali kua ni sahihi hata kama si sahihi basi kitapita kiwepesi zaidi.
2) Lakini la pili wakati wakiendelea kuingia Bungeni Chadema inawapasa waweke baadhi ya mambo chini ili wajenge NGUVU ya upinzani Bungeni katika kuweka Kambi moja tu, inamaana waache tofauti zao na wapinzani wa vyama vengine washauriane wajenge Kambi moja yenye mtazamo mmoja tu. kwa sasa huwezi kudai huitambui Serikali ilhali ndani ya bunge hilo kuna wapinzani wanaonyesha kuitambua serikali iliopo madarakani- logic ya binadamu huezi kuungwa mkono na Taasisi za kimataifa za nje.
3)Wakiweza kuunda Nguvu ya upinzani Bungeni ndio ile dhana ya Mh. Mbowe ya Political Pressure ndio inaweza kupatikana hapo na huweza kusababisha madai yako kusikilizwa ndani na nje. Mfano anaotoa Zanzibar ni kwamba CUF ilikua peke yao ktk baraza la wawakilishi na ndio mana iliweza kuzaa matunda ingelikua kuna vyama vengine ambavyo viliikubali serekali basi CUF ingeshindwa mtazamo wake kwa sababu dhana ingekua mbona vyama vengine vinakubali wao tuu ndo wanakataa?!! nafikiri nimeeleweka vema.
4)Nguvu ya upinzani ya pamoja inaweza kuleta msukumo wa kubadili Katiba ya nchi na kuifanyia marekebisho,hapo ndipo pahala pekee pa kuangaliwa kwa sababu inaonyesha katiba ndio kikwazo na wote wameepa kwamba watailinda na kuitetea,so kufanya marekebisho haina mana kwamba huilindi wala huitetei!! unataka iwe bora zaidi. hizi ndio hoja zangu na mchango wangu kwa wapambanaji wa Chadema.
TANZANIA ILIOJAA NEEMA YA RASILI MALI,BADO NI MASIKINI YENYE KUHITAJI MISAADA !!TANZANIA YENYE NEEMA INAWEZEKANA - WE NEED CHANGE - YES WE CAN.
CCM wamepata ushindi kwa wizi wa kura. Naunga mkono CHADEMA kutomtambua raisi. Tunataka tume huru ya uchaguzi kwa vile tume iliyopo ni ya CCM. Ana Makinda umetumwa na Mafisadi lakini nakuhakikishia mwisho wako utakua mbaya kwa vile hao mafisadi waliokuwezesha watakua wa kwanza kukutosa. Tunataka mabadiliko ya katiba. Sheria inayokataka kupingwa matokeo ya uraisi ni sheria dhalimu inayominya demokrasia. CCM ni chama cha mafsadi
ReplyDeleteThis is their constitutional right to express views according to demand of people whom they selected,to continue pretending that the National election was fair and peace,that is a big sin and you are betraying your own people who elected you.
ReplyDeleteLastly,I would like to remind this corrupt party that they will not reign the country forever,just wait for 2015 election there would be enormous constitutional changes compared to this electoral year(2010).
It's me political Analyst,
DEO.
Mimi, nadhani siasa kwanza lazima iwe chini ya mambo yafuatayo: Uwazi, ukweli, upendo na pia hao walioko uongozini wajuwe kwamba hawakujiweka pale bali wamisimikwa na wapiga kura. Hivyo wajue kwamba vyama vyote ni vya Watanzania na sio watu wa nje. kwa jinsi hii hakuna chama chenye haki yakufanya watakavyo. kama uchaguzi ulikosea kwanza chama tawala kinatakiwa kionyeshe ukomavu kwa kusikiliza mawazo ya ambao hawakuridhika na ikiwezekana wawaite wagombe wote kwenye meza ya duara kazichukua kura zetu na kuzilinganisha na hati zile zilizosainiwa na wasimamizi wa msingi hadi juu. kutokufanya hivyo ni kuvunja sheria na mwishowe wananchi watakapoelewa kwmba kuna mizengwe.... majuto ni baadae.
ReplyDeleteNani alaumiwe kwa hili la CHADEMA kutomtambua rais? Ni CHADEMA au TUME ya uchaguzi?Watanzania muogopeni MUNGU na ebu tumuombe MUNGU na tuwaombee viongozi wetu pia.
ReplyDeleteWewe huna akili timamu kabisaaa!!! Hivi unafikiri Mungu anashangilia wezi wa kura? Acha kuropoka ovyo, watanzania waliowengi wameibiwa kura zao na Mungu ni sahahidi kabisaa wala hakuna ubishi. CHADEMA wana haki kabisa kudai na kuujulisha uma haya yote.
ReplyDeleteUtawala wa Ki-Nazzi wa CCM lalima utaanguka tu. Kwa sababu mwaka huu hawakushinda. Wasingechakachua ilikuwa tayari tuna serikali mpya. Mwizi hata umuombee hawezi kubarikiwa! Watanzania wote wapenda haki tunaunga Mkono CHADEMA na msimamo wao wa kutomtambua Raisi.
ReplyDeleteKiongozi aliyepitishwa kiubavu hafai kuiongoza nchi,maana hatawatendea haki wanachi wake, ni kweli baadhi ya majimbo ccm wameiba kura, ukiangalia usemi Jk alisema Tanzania bila umasikini inawezekana.
ReplyDeleteKwa uchaguzi huu uliofanyika Tz kwa umasikini itaendelea, wanachi badilikeni kisiasa,na kifikira. Tutaendelea kuomba omba mpaka lini? sisi watanzania uwezo tunao, vitega uchumi tunavyo, lakini vinatumiwa na watu wachache amba ni mafisadi. vyama pinzani kuweni makini kutete nchi yetu.Ni haki yake Dr.Slaa kutomtambua Jk.
Mdau toka Guatanamo
Hivi ni kwanini Chadema mnaleta hadithi ya 'Sizitaki mbichi hizi' mnasema hamumtambui JK baada ya kukosa urais lakini posho zake mnazitamani pale bungeni! mnasikitisha,ukipenda ua upende na boga lake posho sawa ila mtoa posho hapana hatuwaelewi.Kama kweli mna uhakika kuwa mmeporwa ushindi na hamumtambui JK, fanyeni kama CUF walivyuofanya walipoamua kutomtambua rais waligomea hata posho zake kwa kutoingia Bungeni na kufikia hata kawaadhibu baadhi ya wabunge walikiuka amri ya chama ya katoingia bungeni kwa kuwafukuzilia mbali kutoka kwenye chama. Pili huo ubaguzi mnaouleta bungeni hauna tija kwa taifa kwa kuwatenga wenzenu wa upinzani, kwani msione hiyo nguvu mliyonayo sasa hivi kuwa itaendelea milele hamjui kuwa kutesa kwa zamu? mmesahau NCCR mwaka 95 nguvu waliyonayo hivi leo hii iko wapi?
ReplyDeleteCHADEMA WASIKUBALI RUSHWA YA MADARAKA NA UONGOZI, MSIMAMO UWE MMOJA! HUWEZI KUUNGANA NA WATU TAYARI WANA NDOA NA CCM, LAO NI MOJA, NA PIA HUWEZI KUUNGANA NA MTU KAMA LYATONGA MREMA AMBAYE SIKU ZOTE ANASHABIKIA CCM, NA HATA HAKUWAHI KUMKAMPENIA RAIS WA CHAMA CHAKE SASA HUYU NI MPINZANI AU YUKO KWA MASLAHI YAKE BINAFSI? CHADEMA KAZENI UZI HATA MSIENDE BUNGENI KUMSIKILIZA KIKWETE, KAENI HATA KWENYE TV MTAMSIKILIZA!
ReplyDeleteHUO NDIYO UKOMAVU WA KISIASA.
Chadema, tatizo ni Dr Slaa kukosa u rais au nini?.Kama ndio hivyo basi si wakomavu kisiasa!.
ReplyDeleteUchaguzi ni ushindani, kushinda au kushindwa ni matokeo.
Hiyo 'political pressure' ya Mbowe is unattainable is segregational politics.Acheni ubinafsi, 'soldier under United Opposition Forces - UOF.
It is a sad moment in the development of our country. The chadema MP should meet to give us the alternative direction from that of Kikwete government. They agreed to form the shadow government. When you agree to form a shadow government it means you have to work with the endorsed president. Who is advising these people? Yes, they have said they don't recognize the president, and they should show it in deeds by walking out not only from his speech but also from the activities of the Parliament. Then we will know they are serious. They should show us that the presidential results were fabricated. Why can't they bring their evidence to the public scrutiny? Or they haven't finished "chakachuaring them? It is now more than two weeks since they claim to have the evidence. I am not sure what would happen, if Slaa had won. All Tanzanians with good will should condemn this move.
ReplyDeleteWATANZANIA ACHENI WOGA HUWEZI KUUNGANA NA MTU KAMA MREMA,CHADEMA KAZENI BUTI WAPIGANAJI TUKO NYUMA YENU MSITISHWE NA NYAU,YEYOTE ANAE MTETEA KIKWETE ANA MASLAHI BINAFSI AU HAELEWI NCHI YAKE .
ReplyDeleteMPIGANAJI KUTOKA UDOM
People's Power!!!!!!!! Wapiganaji wa UDOM tunapenda kuwapongeza Wabunge wetu wa CHADEMA kwa kuonyesha ushujaa wa kuisusia hotuba ya huyu nduli Kikwete ambaye hata sisi wana UDOM hatumtambui kabisa kama ni Rais wa TZ.....
ReplyDeleteNi Hayo Tu.PEOPLE'S POWER,CHADEMA VEMA,HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE.......
Kama hujui njoo ujionee huku Dodoma jinsi mafisadi wanavyo jipongeza na kuzidi kutafuna kodi ya masikini wa Tanzania, Hakika tunahitaji ukombozi wakifikra na nilazima nguvu ya umma itumike. Tunamuomba Bwana Mbowe usilegeze msimamo wako tuko pamoja baba hiyo ndo Nguvu ya umma, Makinda awe makini na ushauri wako kwani watanzania hatuna imani nawe kabisa
ReplyDeleteCHADEMA KAZENI UZI HUO HUO,SIE WAPIGANAJI TUKO NYUMA YENU.
ReplyDeleteCHADEMA leteni mabadiliko TANZANIA ya pili toka mwisho kwa umasikini Duniani, hata maji ya kunywa mpaka atafutwe muhisani ili yawafikie wananchi kweli ni sawa hiyo?
ReplyDeleteWaungwana tuko pamoja nanyi msituangushe CHADEMA na maendeleo ya Watanzania.
CHADEMA MSIOGOPE SEMA SEMA KIELEWEKE MAFISADI NA MAFISI YA CCM WAELEWE SISI WATANZANIA TUMECHOKA NA CCM ALINACHA ZAO NA POROJO ZAO TU, HAKUNA WANACHOKIFANYA ILA WIZI TU, NCHI HII LAZIMA MABADILIKO.NCHI YA UTAJIRI WA KILA AINA HATA MSINGI WA MAJI YA KUNYWA MPAKA MZUNGU ATOE MSAADA, CHADEMA WAPIGANAJI NA WANANCHI WENYE USONGO NA NCHI YAO TUKO PAMOJA NANYI! KIBUTI CHA NGUVU TU KWA CHAMA CHA MAJAMBAZI AKA CCM
ReplyDeleteWatanzania tulioko nje ya nchi tunaunga mkono CHADEMA, SLAA, MBOWE, ZITTO na Msimamo wenu. Sisi pia huku nje ya nchi hatumtambua JK.
ReplyDeleteWameiba kura halafu wanalazimisha kumtambua!
KULA WAMEIBA SANA TU, MKURUGENZI WA UCHAGUZI ANAOGOPA KITUMBUA CHAKE KISIINGIE MCHANGA NDO KASEMA JK KASHINDA, NINI NYIE CCM LAKINI? CHADEMA MSIOGOPE SEMENI TU, SPIKA NAYE ANA LOLOTE NAYE WAMOJA TU ANALAZIMISHA KUMTAMBUA RAIS? MSIKUBALI CHADEMA TUKO PAMOJA NA MSIMAMO MMOJA.
ReplyDeleteWATANZANIA TUMWOGOPE MUNGU HIVI KWELI TUMEFIKIA KUWA NA RAIS WA NCHI ANAE ZINI TENA KWA KUVUNJA NDOA YA MTU,TENA AKIWA MBUNGE AKIWA RAISI SINDIO BALAA WAKE ZETU TUTAFUNGIA KIMANGA
ReplyDeleteSisi hatuna ugomvi binafsi na JK. tunawaachia matusi wana CCM. Chadema Mna support kubwa kila mahali msiogope. Chadema tuko wengi saaanaaa.
ReplyDeleteJk umecahguliwa na Watanzania walio wengi. Hivyo tutumikie sisi Watanzania ambao bado tunakuhitaji, tukakupigia kula na kisha ukaibuka mshindi! Songa mbele. Mpaka sasa Wanaodai kula zimeibiwa wameshindwa kutueleza ziliibwa ngapi na wapi maadamu walisema wana matokeo yote nchi nzima. Kama wao hii wiki ya tatu wameshidwa kuyajumlisha watuambie idadi iweje wailaumu NEC leo ambapo ilishahesabu na kutoa matokeo? Binafsi naona hatujapa upinzani wa kumkomboa masikini bali ni upinzani wa maslahi. hapa Mbowe anatuambia wanachofany ni political pressure ili kuwa na serikali ya pamoja, kumbe hilo ndilo lengo lao!!!! Inanipa mashaka kuwamini upinzni wetu huu.
ReplyDeleteSERIKALI HAINGOZI BUNGE,KUSEMA HIVYO NI KUTOKUJUA.MAANA NCHI INAVYOMBO 3 SERIKALI BUNGE NA MAHAKAMA.KILA KIMOJA KINAJITEGEMEA..MTU ANAWEZA KUWA MBUNGE NA ASIMTAMBUE RAIS...CCM INATIA UCHUNGU SANA KWA KUUMIZA WATANZANIA.LEO KIKWETE ANALALAMIKIA UDINI WAKATI YEYE NDIYE AMEKUZA UDINI NCHI..MAKAMU WAKE TAYARI AMESHAAHIDI KUWAFURAHISHA WAISLAMU KWA KUWAPA MAHAKA YA KADHI,JE HUO SIYO UDINI?
ReplyDeleteWachangiaji walio wengi hawajui kuwa hela zitolewazo kwa wabunge ni kutokana na kodi za wananchi siyo kutoka kwa Raisi. Wawakirishi wakiwa pale kuwatetea wananchi katika bunge ambayo ni nguzo mojawapo ya mihimili mikuu mitatu yakuliongoza taifa kutokana na katiba.
ReplyDeleteNaitwa James, Kondoa
ReplyDeleteChadema kubalini kuwatumikia wananchi waliowachagua na mjipange kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015. Naamini kuwa watanzania wanahitaji elimu ya uraia, na hivyo kuondokana na dhana ya ukale. Njooni vijijini mhamasishe watu kukubali mabadiliko. Tumieni hizo ruzuku mnazopewa kuwafikia watanzania walio wengi. Msifikiri kuruka na helikopita ndiyo watu watawachagua. Bado safari ni ndefu ya kuleta mabadiliko ya kweli. Kwa kuapa kwenu bungeni kwa kutumia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mlikubali kumtambua rais wake. HIvyo nawashauri muwatumikie waliotuma wana imani na ninyi.
CHADEMA VEMA SANA,WAPIGANAJI TUKO NYUMA YENU
ReplyDeleteMimi ni yule yule Hafidh kutoka Zanzibar.
ReplyDeleteNawaomba ndugu zangu katika maoni yenu mujenge na kushauri vizuri ili malengo yafanikiwe. Jazba haijengi ila inaharibu katika kukuza Demokrasia nchini,toweni maoni na ushauri mzuri wa kukielewesha Chadema nini wanatakiwa kufanya kwa sasa sio tu kukurupuka na kusema endeleni Chadema na msimamo!! Kwa nnavyo ijua CCM hata ukigoma wao hawajali na wanatia pamba za masikio kabisa. Cha msingi ni kujipanga na kutoa dira wapi chama kinaelekea.
Naomba mujenge hoja nzuri zenye nguvu ili tujadiliane kwa ajili ya mustakbal wa Taifa letu.
TANZANIA YENYE NEEMA INAWEZEKANA.
Hivi wewe Makinda, Unadhani huu ni wakati wa kubebana kwa vyeo??? Umeonyesha udhaifu na yale yaliyopo ndani ya CCM kulindana kwa vyeo. Nani kakwambia Chadema wana njaa ya pesa. Hao wapo kutumikia wananchi na siyo wa kwa njaa. kama hao akina..... Ujue Sita aliona mbali kuruhusu demokrasia ndani ya bunge. Hivi unajua kuna wasomi wangapi leo hii hapa Tanzania?? Unafikiri huu ni wakati uleeee wa kipindi kileeee chenye madokta 5. Walimu 10 na Rubani mmoja. Amka hadanganywi mtu. Hata Mama zetu tuna waelimisha juu ya ubovu wa CCM na Makinda ndio maana mukapigwa chini then mukachakachua
ReplyDeleteHao wabunge vijana wa Chadema wako hapo kwa ajili ya magari ya mashangingi na posho zao basi.
ReplyDeleteKama mimi muongo leo hii Chadema wafanya hiyo political pressure yao kiukweli kabisa. WAFANYE KAMA CUF HUKO ZANZIBAR WASUSE KILA KITU WASIHUDHURIE VIKAO WALA WASIUNDE SERIKALI YA UPINZANI KWANZA WANAMPINGA NANI NAO HAWAITAMBUI SERIKALI ILIYOKO MADARAKANi?
Hiyo jumuiya ya kimataifa pia inawaona ni kichekesho kwani huku mnadai hamuitambui serikali lakini Bungeni mnaingia ambapo ni mhimili mmojawapo wa nchi, na posho mnachukua, na serikali ya upinzani mmeunda. Hivi hamjui kuwa mnatuma conflicting messages? Mnaonekana kuwa mnajali zaidi mafao yenu na si vinginevyo. Wenzenu CUF Unguja hali kama hiyo iliwacost kisiasa, na hatari yake ni hiyo Mama Makinda keshawahabarisha.
Kwa wale wanaosema kuwa hawako kupata vyeo, mjue kuwa kwenye kamati mbali mbali za Bunge ndiko unakoweza kujua kama kuna tatizo la ufisadi mahali, kwa kutoshiriki kwao kwenye kamati hizo kama kamati za nishati, madini, na za mambo ya fedha je watajuaje kinachoendelea kwenye hizo sekta?
Shauri yenu nyie fuateni ushauri wa vijana wenu ambao hawajui gharama ya hicho mnachotaka kufanya, mtabakia kusikiliza hotuba za bajeti bila na kuzipinga huku zikipita kwa kura za CCM na hamtapata nafasi ya kuchambua na kutoa changamoto kwenye bunge hili.
Na waswahili husema ngoma ikilia sana mwishoe hupasuka. Kwanza ninachokiona ni kuwa Zitto peke yake anajua gharama ya hicho wanachokifanya lakini hawezi kumwambia Mwenyekiti wake akamwelewa kwanza ni haambiliki, kwa hiyo hiyo pia ni nafasi ya Zitto kumwachia pweza ajipalie makaa kwa mikono yake mwenyewe. Only time will tell! Only time will tell! For some of us we had seen this kind of move before we are just watching the political drama unfolding before us!
Kwanini kusiwepo na makubaliano ya kuanza kuandaa katiba mpya na kuwa na tume huru ili kuondoa mvutano unaojitokeza? Kama chaguzi zinazojitokeza zinatazamiwa kuwa za halali na siyo kwa ajili ya watu wachache kwanini uongozi uliojilazimisha kutokuwa tayari kuwa na katiba mpya inayokidhi matakwa ya mfumo wa vyama vingi? Tunashukuru kuna changamoto hivi sasa inayotolewa na CHADEMA na watanzania wanaunga mkono, na itazaa matunda.
ReplyDeleteHapa tu spika kaishaonyesha UCCM wake, je huko mbele itakuwaje, angalia mama tunakuangalia kwenye luninga na kukusikiliza toa maamuzi ya busara siyo ya upendeleo, tuko nyuma tunataka haki yetu ya watanzania ionekane. na siyo uccm. acheni siasa, fanyeni kazi kwa maslahi ya wanainchi.
ReplyDeleteU-Chadema, U-Nccr, U-Cuf, U-Tlp,...nk hautupeleki popote!
ReplyDeleteAmkeni na kufahamu kuwa bila ya nguvu ya pamoja & clear strategy, we will never beat CCM and enjoy the fruits of multiparty politics.
What to do?:-
1. Upinzani bila ya kuwa na tamaa au selfish agenda, ujipange safu moja na kuwa na common goal- kuingoa CCM.
2.Ili kufia lengo hilo, lazima tujue sasa tupo katika level gani. Hivi sasa tuko katika level inayoitwa CHAKACHUA level.
3. Kawaida CHAKACHUA level inachukua miaka 15-45 kuidhibiti.Wenzetu Zenj, wameanza kuikamata na huenda ktk 5-10yrs wakafanikiwa. Ni Kenya pekee ndio walioweza kuimudu ndani ya miaka 15!
4. Kugomea serikali, kutomtambua Raisi, nk, huo ni upuuzi mtupu bali ni kurefusha CHAKACHUA level life.
5. Hamasisha kila mTz, viongozi wa upinzani wawe mifano bora ya kumkabili common competitor.
Kipimo kile upimacho ndicho utakachopimiwa. Leo hii ni zamu ya upinzani kuminywa ila ccm ijuwe kesho itakapokuwa ndicho chama pinzani kitajuta. Angalia upande wa pili wa shilingi. Nashauri ccm na dola yake isikilize sehemu nyingine ya wawakilishi wa wananchi kama walivyo. Madai yao ni ya msingi katika zama hizi za demokrasia na mageuzi. Mambo yamebadilika. nani angejkuwa leo Rais atapita kwa 60%. Wimbi hili halitaishia hapo. Kuweni kama Baba wa Taifa hili alivyoona wimbi la mageuzi akasema "ukiona mwenzako ananyolewa na wewe tia maji". Leo wanawanyoa CHADEMA siku itafika tena yaja na haipingiki, Upinzani utachukua dola, tutatafutana hapa. Hapatakua pakutosha. Wakati umefika na huo ndio ukweli. Statu-quo hailipi tena. Hebu fikiria Mabutu, Makaburu, huko Guinea. Ulipofika wakati hakuna aliyeuzuwia. Epusheni machafuko yasijeyakatokea. Hebu someni tu maoni ya wananchi alafu chujeni wangapi wanaelekea upande upi ndipo mtabaini kuwa wakati wa mabadiliko ya lazima umefika. Akatakeye kinga kifua kicha upepo huu utambeba. Mabadiliko ya sasa ya kudai Katiba na Tume huru ya Uchaguzi hayaepukike. anonimous
ReplyDelete