LONDON,England
MCHEZAJI Rio Ferdinand amesema kwamba kupumzishwa katika mechi ya England dhidi ya Ufaransa alikuwa siyo majeruhi bali ilikuwa ni kwa ajili ya tahadhari.
Beki huyo wa kati wa timu ya Manchester United alipimzishwa baada ya kucheza zikiwa ni takribani dakika 45 za mchezo huo wa kirafiki ambao ulipigwa juzi kwenye uwanja wa Wembley.
Wakati akitolewa nje ya uwanja,Simba hao watatu walikuwa wamelala kwa bao 1-0 na katika muda huo Ferdinand alikuwa hana nguvu ya kuweza kuizuia timu hiyo isiondokane na kipigo cha mabao 2-1 kwenye ardhi yake ya nyumbani.
Kukosekana kwake uwanjani kipindi cha pili ndicho kilichozua hali ya wasiwasi kwa mashabiki wa Manchester ambao wanataka Ferdinand awe fiti kwa ajili ya mtanange wa kesho dhidi ya Wigan.
Kutokana na hali hiyo ndiyo maana akaamua kuwaondoa woga wote waliokuwa na wasiwasi kuhusu hali hiyo akisema kuwa aliamua kupumzika katikati ya wiki ili kuzuia asishindwe kucheza katika mechi hiyo.
Akiondoa hali ya wasiwasi huo, Ferdinand aliiambia Sky Sports kuwa: "Ilikuwa ni hali ya tahadhari. Tumecheza mechi chache kwa upande wetu,hivyo nilipumzika kwa ajili ya tahadhari,".
Akizungumzia kiwango cha timu yao dhidi ya Ufaransa ambapo ilishuhudiwa kocha Fabio Capello akiwachezesha chipukizi wengi, Ferdinand alisema kuwa England ni lazima ifanye vizuri.
"Tumegundua kwamba tuliwatumia wachezaji wapya na wasio kuwa na uzoefu katika timu yetu," alisema Ferdinand
No comments:
Post a Comment