Na Jamillah Daffo, Babati
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara kimepata pigo kwa kufiwa na Katibu wake wa Wilaya ya Babati, Bi. Tuli Mwang’amba anayeaminika alifanikisha
kampeni za ubunge wa jimbo la Babati Mjini kwa kura za kishindo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara, Bi. Avelin Mushi alisema kuwa Bi. Mwang'amba aliyehamishiwa wilaya ni humo kikazi mwaka huu akitoka wilaya ya Mbeya Mjini, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo siku nyingi, uliosababisha kifo chake Jumapili wakati akipatiwa matibabu na mazishi yake yalitarajiwa kufanyika jana.
Bi. Mushi alisema kuwa Bi Mwang'amba ambaye alikuwa ni tegemeo la chama wilayani humo, ameacha pengo kwa kuwa alikuwa mchapa kazi aliyekuwa anahakikisha chama kinapata mafanikio.
Wakati wa uhai wake Bi. Mwang'amba alisimamia mchakato wa
uchaguzi mkuu katika jimbo la Babati Mjini na kuhakikisha CCM kinaibuka mshindi.
No comments:
Post a Comment