29 November 2010

CHADEMA yalaani kuzuia mikutano.

*Yasema polisi inataka kujenda dola ya kipolisi
*Yatoa sharti kushirikiana na CUF katika bunge


Na Tumaini Makene.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani kitendo cha Jeshi la Polisi, kuzuia mikutano ya wabunge wake na mingine ya hadhara ya chama hicho, kikidai kuwa ni
dalili za wazi za 'kuminya haki za raia, kuvunja sheria ya haki, kinga na mamlaka ya bunge na kukaribisha dola ya kipolisi' nchini.

Kimesema kuwa vitendo vya Jeshi la Polisi, vinashiria hatari kwa demokrasia nchini, haki za kikatiba na za kisheria za wananchi, huku kikitoa mifano ya dhana hiyo ya dola ya kipolisi (police state) ni kama vile ilivyokuwa katika nchi za Zimbabwe, Afrika Kusini wakati wa utawala wa makaburu; na Kenya wakati wa utawala wa Rais wa Pili, Daniel Arap Moi.

Kimesema kuwa kama chama kikuu cha upinzani chenye kubeba matumaini ya mabadiliko ya Watanzania walio wengi, hakikubali nchi kufikishwa huko, wabunge wake kunyamazishwa wala bunge kurudishwa kuwa kamati ya chama cha siasa kama ilivyokuwa enzi la chama kimoja.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa CHADEMA, Bw. Tundu Lissu alisema kuwa chama hicho kimepokea taarifa za kimaandishi kutoka mikoa na wilaya mbalimbali nchini kwamba Jeshi la Polisi limepiga marufuku mikutano ya hadhara ya wabunge wa CHADEMA katika maeneo kadhaa nchini kwa kutumia sababu mbalimbali kama vile 'taarifa za kiintelijensia' na kuwa baadhi ya vyama vya siasa havina nia njema.

"Taarifa tulizozipata kimaandishi zinaonesha kwamba Jeshi la Polisi limezuia mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika katika viwanja vya Kwaraa, Babati Mjini kwa ajili ya kumpokea Paulina P. Gekul, mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Manyara...mkutano wa hadhara Shule ya Msingi Mkendo, mjini Msoma kwa ajili ya kumpokea Vicent Kiboko Nyerere nao umepigwa marufuku.

"Mikutano mingine ya wabunge wa CHADEMA iliyopigwa marufuku na polisi ni pamoja na ule wa Said Arfi (Mpanda Mjini) na Annamary Stella Mallack (viti maalum Rukwa), Peter Msigwa (Iringa Mjini), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) na Ezekia Wenje (Nyamagana).

Katika mikutano yote hiyo taarifa zilikwishatolewa na wabunge husika kwa mujibu wa Sheria ya Kinga, Mamlaka na Haki za Bunge. Polisi pia wamezuia mkutano wa kisiasa ulipangwa kufanyika leo (jana) Jimbo la Segerea kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa," alisema na kuongeza;

"Jeshi la Polisi limetumia visingizio vya 'taarifa za kiitelijensia' (Babati mjini na Musoma mjini), 'baadhi ya vyama vya siasa havina nia njema' (Mpanda Mjini) n.k. kama sababu ya kupiga marufuku mikutano hiyo ya hadhara.

"Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ukonga, Dar es Salaam amedai kwamba '...mikutano na maandamano ya kisiasa imezuiliwa maeneo yote kutokana na hali ya kiusalama'. Jeshi la Polisi halijatoa ufafanuzi wowote juu ya vyanzo vya taarifa hizo wala kutaja vyama vinavyodaiwa kuwa na nia mbaya."

Bw. Lissu alisema kuwa haki ya wananchi kujumuika na kujadili mustakabali wa nchi yao inalindwa na katiba ya nchi na inatambulika kimatifa na nchi zote zinazoheshimu demokrasia na haki za binadamu, huku akiongeza kuwa kuzuia mikutano ya wabunge ni kuwazuia kufanya kazi zao, hivyo kitendo hicho ni shambulio la waziwazi kwa haki, kinga na mamlaka ya bunge ambazo zinatambulika kimataifa na zinalindwa na katiba na Sheria ya Kinga, Mamlaka na Haki za Bunge (1988).

Akinukuu moja ya vifungu katika sheria hiyo, Bw. Lissu alisema kuwa mbunge anayo haki ya kufanya mikutano ya hadhara na mamlaka zote husika zitatakiwa kuwezesha mikutano hiyo kufanyika kwa namna itakayomfaa mbunge kwa kadri inavyowezekana kwa mazingira yaliyopo, huku akiongeza kuwa kwa mujibu wa sheria hiyo ni kosa la jinai, chini ya sheria hiyo, kwa mtu yeyote kuzuia mikutano hiyo kufanyika na anaweza kushtakiwa na mamlaka husika.

"Kama kweli kuna 'taarifa za kiintelijensia' juu ya tishio la usalama katika mikutano hiyo, kama inavyodaiwa na polisi, basi jukumu lao kuhakikisha usalama wa kutosha unakuwepo badala ya kuzuia wabunge kufanya kazi zao na kuvunja katiba na sheria za nchi yetu...vitendo vya polisi vinaashiria hatari kubwa kwa demokrasia nchini kwetu na kwa haki za kikatiba na kisheria za wananchi wetu.

"Jeshi la Polisi linapoanza kupiga marufuku wananchi kujumuika pamoja kwenye mikutano ya hadhara ni mwanzo wa kuielekeza nchi katika dola ya kipolisi mithili ya Zimbabwe ya Robert Mugabe, Kenya ya zama za Daniel arap Moi na Afrika Kusini ya wakati wa Makaburu...linapopiga marufuku mikutano ya wabunge majimboni kwao ni mwanzo wa kupiga marufuku mijadala huru bungeni na kuielekeza nchi katika utawala wa kiimla, kama si udikteta wa kijeshi.

"Kama chama kikuu cha upinzani chenye kubeba matumaini ya mabadiliko ya Watanzania walio wengi, CHADEMA haiwezi kukubali nchi yetu kugeuzwa kuwa Zimbabwe ya Afrika Mashariki. CHADEMA haiwezi kukubali wabunge wake kunyamazishwa na bunge letu kurudishwa kuwa kamati ya Chama Cha Mapinduzi kama ilivyokuwa miaka ya chama kimoja. CHADEMA haiwezi kukaa kimya wakati haki za wananchi zinazotambuliwa na kulindwa zinakanyagwa."

Wakati huo huo, Bw. Lissu alitoa ufafanuzi wa kisheria namna mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ambavyo yanatishia hatma ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania, kati ya Zanzibar na Tanzania Bara, ambapo alisema kuwa ili kuwepo na muungano wa dhati baina ya vyama vya upinzani, hususan CHADEMA na CUF, ni vyema wenzao wa CUF wakaweka bayana msimamo wao juu mabadiliko hayo, akidai yamevunja Katiba ya Tanzania, wazi wazi.

Bw. Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema kuwa mabadiliko hayo 'ni ukiukwaji wa wazi katiba ya muungano na kutishia usalama wa nchi na mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama zilivyoungana Aprili 26, 1964'.

Bw. Lissu alikuwa akijibu swali juu ya msuguano uliopo sasa, hususan katika uundaji wa kambi ya pamoja ya upinzani bungeni, hasa kwa kushirikiana na Chama cha Wananchi (CUF) ambapo alisema kuwa ni vyema watu wanaposhirikiana wakawa na mahali pazuri pa kuanzia hasa katika masuala ya msingi ya kitaifa kama hilo la uvunjaji wa Katiba ya Tanzania, ambayo bado inatambua Tanzania ni nchi moja, yenye sehemu mbili Tanzania Bara na Zanzibar.

"Ndoa ya CCM na CUF, maridhiano ya mwafaka CUF na CCM yaliyopelekea marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ni ukiukwaji wa waziwazi na wa makusudi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa katiba, baada ya muungano Tanzania ni nchi moja, sasa mwafaka umerudisha nchi mbili, maana Zanzibar nayo ni nchi kwa mujibu wa ibara 3 ya mabadiliko hayo.

"Kifungu hicho cha 3 kinasema kuwa Zanzibar ni nchi ambayo mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogovidogo vilivyoizunguka bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar...Kifungu cha 4 chenyewe kinasema kwamba Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano bado inatambua kuwa Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano...Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo...mabadiliko yale hayatambui vyote hivi...yameondoa pia mamlaka ya Rais wa Tanzania kugawa mikoa ya Zanzibar, mabadiliko yanamwita Rais wa Zanzibar kuwa ni mkuu wa nchi ya Zanzibar, head of state...

"Pia hata suala la mahakama ya rufaa ambalo linatambulika katika katiba ya nchi kuwa ni la muungano katiba mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar haitambuliki tena...wamefuta rufaa kutoka mahakama kuu kwenda Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, sasa baada ya CCM na CUF kujitangazia uhuru wao Zanzibar, tungependa kujua msimamo wao juu ya mambo haya ya ukiukwaji, kuchanwa chanwa kwa katiba na kutishia kwa usalama wa nchi.

"Baada ya hayo ajenda ya CUF Tanzania bara sasa ni ipi, ni vyema wakasema msimamo wao ni upi ili twende sawa, maana iko siku tunaweza kupeleka hoja bungeni kuomba kuchunguzwa kwa nani hasa alihusika katika kuvunja katiba sasa wao watasimamia wapi.

"Unajua tunaweza kusahau tukasamehe makovu sijui ya uchaguzi na vitu vingine lakini haya ni mambo ya msingi kwa taifa, ili tushirikiane vyema ni bora tuelewane katika mambo kama haya," alisema Lissu. 

 

25 comments:

  1. hAWA JAMAA WA CHADEMA NAONA SASA WANAZIDI KUCHANGANYIKIWA KWANI WAO WANADHANI KILA JAMBO WANALOLITAKA WAO LIWE NDIO HIVYO

    ReplyDelete
  2. Peoples power will always win. Wewe anonym wa kwanza nadhani wewe hujuia tumetoka wapi, tuko wapi na tunaelekea wapi. Bora ukakaa kimya kuliko kuongea kwa mithili ya KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI ambazo zimebaki historia. Unadhani CCM ni chama cha muungano au sasa kimebakia chama cha Tanganyika? Nineema kuwa watu wanafanya mambo bila kuelewa. Hii tatusaidia kuunda taifa la Tanganyika!

    ReplyDelete
  3. Ni kweli kabisa,Muungano umebaki ni maneno tu,inabidi Mr Lissu mkomae bungeni ili wadanganyika tujue moja kama muungano upo au umekufa na kama Zanzibar ni nchi au sio nchi na kama Kikwete ni Rais wa Tanzania bara na visiwani ambako tayari wana raisi wao kama taifa huru,pia tujue role ya wabunge wa CUF toka Zanzibar kwenye bunge la Bara"La MUUNGANO" etc vinginevyo kama wao ni state tujue kama sasa tuna federation instead of union,vinginevyo sioni role ya wabunge wa CUF tokea Zanzibar kwenye bunge la Dodoma,nadhani nafasi yao ni kwenye baraza la wawakilishi.

    ReplyDelete
  4. Chama cha upinzani ni kimoja tu nancho ni CHADEMA. Kwa maoni yangu vyama vingine vyote ni mamluki hasa CUF, NCCR MAgeuzi na TLP.

    ReplyDelete
  5. pETRO eUSEBIUS mSELEWANovember 29, 2010 at 9:24 AM

    Sina sababu wala uwezo wa kubisha au kuongeza juu ya aliyoyasema Msomi mwenzangu,Mh.Tundu Lissu.Mambo yataeleweka tu...subirini muone.

    ReplyDelete
  6. Chadema achaneni na CUF, wenzenu tayari wana ndoa na CCM, msiwakubali watauza siri zenu kwa CCM.Na ndio maana wana kibuli ,watawavuruga mkiungana nao.Hao tayari wako kwenye ndoa na CCM,na ni ndoa yenye masilahi kwao na si vyama vingine. CUF sio chama cha upinzani tena.Cahama ambacho tayari kinashirikiana na CCM huwezi kusema ni chama cha upinzani na muungane nao.

    ReplyDelete
  7. AMMA KWELI MSEMO WA UKIPATA MATAKO KULIA BWATA!
    LEO CHADEMA WAO WANAJIONA NDIO HASWA CHAMA CHA UPINZANI KULIKO WENZAO,INAJIONYESHA NI UBINAFSI GANI WALIONAO,HATA HAJA YA KUSHIRIKIANA NA WENZAO HAWATAKI,N AWATAANZA KUTIMUANA MUDA SI MREFU YETU MACHO! HATUNA HAJA YA MIKUTANO SASA NI WAKATI WA KUTAFAKARI NA KUSONGA KIMAENDELEO MBELE,MAMBO YANAYODAIWA YOTE YAELEKEZWE BUNGENI, KUWAITA WANANCHI KWA SASA NI KAZI BURE LIPITISHWE BUNGENI HALAFU MIKUTANO IJE ILI KUWAHAMASISHA WANANCHI. MIEZI 3 WATU WAKO VIWANJANI SASA NI KUJIPANGA KWA UTEKELEZAJI NYINYI WANASIASA KAZI YENU NI KUHUBIRI KWA HIYO MNATAKA WATU WAACHE KAZI ZAO KUWASIKILIZA NYINYI TUU!MMESHAONYESHA HAMNA NIA NJEMA WAZO LETU KUWAHAMASISHA WATU SASA ILI WAINGIE MITAANI WAWAFANYIE FUJO WENYE KUTAFUTA RIZKI ZAO BARABARANI ACHENI HIZO

    ReplyDelete
  8. Ni lazima tuwe wakweli kwamba sasa hivi CUF siyo chama cha upinzani kwa sababu wao wako kwenye serikali. Hivyo hawawezi kuipinga serikali waliyomo. Tena muafaka wao na CCM Zanzibar umewapa wao faida kuliko CCM sasa kwanini tena wawe na upinzani na CCM wakati wao ndo wanafaidika zaidi kuliko hata CCM? Muungano wetu ni ndoa ya kulazimishana wao wanachotaka Wazanzibar wafaidike CCM wa Tanganyika tuendelee kudhulumiwa haki zetu. Wao wanapata kazi na vyeo Tanganyika kelele zao ni kutaka kuendelea kubembelezwa na kutishia kujitoa kwenye Muungano na wana siasa wa Tanzania wakisikia hivyo basi matumbo moto kana kwamba Zanzibar wana lolote la kutupa wabara. Sasa hivi watakuja na nafasi ya Maalim Seif kwenye Muungano ili wawe na superpower nne sisi tuendelee kuwa na wawili tu. Muungano wa kubembeleza haufai na wala hautadumu tuwaache wazanzibar ili wauawe kati ya Wauunguja na Wapemba. Ndipo watakapoona faida ya Muungano

    ReplyDelete
  9. ni vyema CHADEMA mkapunguza u mimi wa kujiona ni nyinyi tu wenye mawazo ya kukubalika na Watanzania Hatujawona kama mmekomaa sana kisiasa kiasi cha kuwaona wenzenu wote ni mbumbumbu tu msisahau kuwa mpasuko ndani ya CCM ndio uliokupeni hiyo Neema ya viti jipeni muda wa mkubalike kwa Wananchi wa wakubali ndio muonyeshe UBABE LA SI HIVYO jiandaeni kusambaratishwa ndani ya miaka 5.

    ReplyDelete
  10. Maoni yaliyotangulia yanajionyesha dhahiri kuwa wasomo wengi wa Tanzania hasa upande wa Tanganyika hawaifahamu kabisa historia na wala mkataba wa Muungano wa mwaka 1964. Walio wengi wameukuta tu huu muungano na hata wale waliousoma katika vitabu basi ni vile vilivyoandikwa kwa kupotosha historia sahihi ya muungano.Ndugu zangu awali kulikuwepo na mambo 11 tu katika mkataba huu na mambo mengi yaliingizwa baadae kwa kutia viraka katiba ya Jamhuri ya Muungano kila pale Tanganyika ilipohitaji kuipunguzia Zanzibar madaraka yake kama nchi. Hivi ndugu zangu leo hii Wazanzibari wakidai Rais wa Zanzibar ndio awe makamo wa Rais wa Jamhuri ya muungano kama ilivyokuwa kabla ya katiba kuvurugwa na Bara kwa kisingizio cha vyama vingi mtasema wamekosea? Mambo kama haya ya mahakama ya rufaa kuhusika na Zanzibar pia hayakuwemo kwenye mkataba wa muungano. Masuala ya ushuru wa biashara, ushirikiano wa maendeleo na mataifa mengine(tofautisha na mambo ya nje kisiasa, na mengine kadhaa Zanzibar ilikuwa na mamlaka nayo lakini leo hii Tanganyika imetunyonyoa mbawa mithili ya ukoloni. Ndugu zangu Watanganyika laiti mngelikuwa nyinyi ndio waathirika wa muungano huu basi kipengele kimoja tu cha Tanganyika kutumia rasilimali zote za nchi inayoitwa ya muungano na aina zote za misaada kutoka kwa wahisani wa maendeleo kwa ajili ya kujenga ustawi wa upnde mmoja tu wa Bara basi mngepiga kelele hadi mitume na malaika wa Mungu wangeshtuka.
    Najua ni vigumu kuibadilisha "Attitude" yenu kwa vile ndivyo hata wahadhiri waliowafunza kwenye vyuo mlivyosoma waliwapika muwe hivyo na ndivyo wao walivyotumwa wawatayarishe mithili ya mtoto wa kiyahudi anavyotayarishwa dhidi ya Mpalestina. Lakini nawaombeni mtafute ukweli wa muungano huu kabla ya miaka ya 80s ulikuwa na sura gani? Jee Zanzibar haikuwa na mamlaka yake katika mambo yake kadhaa ambayo sasa yametwaliwa (yameporwa)na Tanganyika?

    ReplyDelete
  11. CHADEMA MKUMBUKE KAMA SIO CCM KUWEKA KURA ZA MAONI MSINGEAMBULIA HIVYO VITI MNAVYOVIONA SASA, NAWAAMBIENI HAMJAKUBALIKA BADO, SASA MNATAKIWA MJE VIZURI KWA MIAKA MITANO LA SIVYO MTASHINDWA VIBAYA, SIO WOTE WALIOCHAGULIWA WATAFANYA CHA MAANA ILI TUWACHAGUE TENA BAADA YA MIAKA 5, SO LAZINA MUWE MAKINI JINSI MNAVYOKUJA SASA......

    ReplyDelete
  12. Tumechoka na kero za Chadema, kila siku wana makele utadhani kasuku mia kwenye tundu moja. Hawataki kukubali kwamba sasa mambo ya kampeni yameisha na tunasonga mbele ili kuwapa CCM kufanya wanalo weza na wao Chadema, tunawapa nafasi ya kujitafakari wapi wameboronga, wafanye nini kipindi kijacho ili kuchukua nafasi zote. Sasa wao kila siku kelele, wana vinyongo na hasira zisizo isha, hata kama tuliwapigia kura, na hatukupata kuongoza nchi, basi waridhike na kusubiri next time, wana vuruga watu, na kweli ni haki wanyimwe kufanya hiyo mikutano yao ya majungu na maandamano yao kwani niya yao wanataka nchi isiwe stable. Wana lengo gani, hata sisi wanachama tumechoka kusikia majungu na makero kila siku. Kuwa na wanachama wengi nchini isiwe kero kwa watu wote nchini. Huyu Slaa ndiye mwenye kelele ambazo hazija soma (un-cooth, un-civilized, un-mannared, un-cultured) Tumechoka. Tunakipenda sana chama lakini chini ya Uongozi wa Slaa aliye jaa chuki itatubidi kukihama. Tuweni na busara basi angalao, laah, too much, kila mtu kiongozi kwenye Chadema, kila mtu anajua, what is all this??? Kaeni, mfikirie na kutafakari, mnatuonyesha nini sisi wafuasi, tumechoka, tuacheni tufanye kazi za kuleta maendeleo na siyo kazi ya kuleta vurugu, majungu na chuki.

    ReplyDelete
  13. Huyu mzee Slaa ndiye mwenye vurugu kubwa sana hapa nchini. Mwanzo wanachama wote tulishawishika kwamba tuna Kiongozi makini, lakini sasa umakini wake unatia shaka maana hata kama sisi na chama chetu cha chadema tungeupata Urais, bado nchi hii ingekwenda vibaya sana. Inawezekana hata watu wangeuawa, maana yeye ana hasira, chuki na kila duku duku la dunia. Roho yake haiachilii hasira au ni aibu ya kuukosa urais maana alisha waahidi wake zake kwamba watakuwa first ladies, basi asitumie mwiko huo kusongea ugali wa mchanga. Anatuchosha sana anapokuwa hana busara, hana akili ya kutaka kushindwa na kutoa mwanya wa ushirikiano na walio madarakani. Mungu siyo mjinga Kumpa JK urais maana anajua anafanya nini. Na Mungu huyu huyu anajua angempa yeye Slaa Urais angefanya nini, mimi kama mwana chadema, kuliko kumpa Slaa Urais, bora kumpa Mbowe maana hana hasira kama huyu Slaa. Slaa yeye anataka maangamizi, ya kuua, kususa, kuvunja, kuharibu na kuangamiza kabisa kama sodoma na gomora. Sisi, wanachama wa chadema, hatuko tayari kukataa matokeo aliyo yapanga Mungu na kulazimishwa kukubali matakwa ya Slaa. Au anataka kujiita Malaika Slaa na siyo Wilbroad Slaa?? aone aibu, asiwayumbishe watu nchini na choko choko zake za uchochezi. Mimi kama mwanachama siafiki mikutano ya majungu na wala maandamo ya makero kwa watu wengine. Hao watu wanao andamana kazi yao ni chama tu au wanazo shughuli nyingine za kimaisha za kufanya?. Slaa, mzee mkubwa, mzee mzima, kuwa na busara, kaa chini, achia nafasi watu wafanye kazi nyingine za kujikimu kimaisha. Nchi hii moja tu wewe unataka kuigawa iweje!! Tumechoka na malumbano yasiyo isha. Tukubali matokeo na tusonge mbele ili watu waweze kulijenga taifa na kujijenga majumbani kwao. Yeye Slaa siyo Mungu kwamba kila mtanzania maisha yake yange badilika kwa siku moja, asitudanganye na kutuacha tukipigana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili yake. KUBALI MATOKEO MZEE, NENDA HOME USUBIRI 2015, KAMA URAIS UMEANDIKIWA UTAUPATA KAMA MUNGU KASEMA NO, BASI NI NO, NO, NO HADI KUFA. KAMA NI YES, BASI NI YES, YES HADI UKAMILIFU WA DAHALI.Mwache JK amalizie ngwe yake kwa usalama.Kama una huruma kwa wananchi wako, ungeanza na kuwapa hizo pesa majumbani na mifukoni wananchi wa jimbo letu la karatu na wote walio masikini katika kijiji chako, uwe mfano kwamba wewe unazo baraka nyingi toka kwa Mungu. Maneno tu kwamba utaibadilisha nchi, ki vipi, ki-miujiza au? Kwa kutupiganisha, tuuane ili wewe uwe Rais, ACHA HIZO MZEE, UMEKUWA MTU MZIMA. USIJE KUWA MTU MZIMA HOVYO!! Tunakupenda bado, usituudhi tukakuacha kwenye mataa na kukukacha baba. Wenzio kina Mbowe wana akili basi acha hao waongoze, wewe na Tundu Lisu, mkae tuwaletee baraka mnazo zitaka toka mbinguni, msilete vurugu nchini kwa mambo yanu ya uchochezi. Mimi ni Mwanachama hai, aliye iva kabisa wa chadema ila nimechoka na majungu ya Slaa na Lisu.

    ReplyDelete
  14. Hatuwaelewi mnaposema SLAA NA LISU ni majungu, people powerrrrrr. Wananchi tunafajia kwa kwenda mbele.

    ReplyDelete
  15. pETRO eUSEBIUS mSELEWANovember 29, 2010 at 3:00 PM

    Moungo mkubwa wewe uliyenitangulia kutoa maoni.Kama kweli ni mwanachama wa CHADEMA,WEKA HEWANI JINA NA KADI NO YAKO.Acha unafiki.CHADEMA haina watu wanafiki kama wewe.Tuachie viongozi wetu.Tuachie Slaa na Lissu wetu.Ishia hapohapo!

    ReplyDelete
  16. ww anonymous said unayako si bure au unaishi kwa msaada ccm kiuwa na fikra za kuikomboa nchi .ABASI

    ReplyDelete
  17. huyu aliyekutangulia petro ni mwana ccm tena shushu wa usalama wa taifa, wanataka kuwapotosha wanchadema wakati wao wameshiba dhuluma; Mchawi na mganga ni mtu huyo huyo; wenye hasira hawawaoni? wamefunga watu gerezani hata hawana makosa; je tuwaacha watu wa namna hiyo wateseke bila makosa katika nchi inayoitwa ina amani na utulivu?. wanafiki nyie wote wawili mliomtangulia petro si wanachama chadema, wala ccm, ila nyie ni nguvu ya dola mliozoea kuwadhulumu watu, hamjui hata historia ya Tanganyika, Tanzania ndani ya TANU, na CCM. mmepelekwa kwenye kazi za usalama na mikono ya akina baba na mjomba, hivyo hamjui uchungu wa kupigania haki, maana mmezoea kura jamu, Blue band, nyama, kitanda mavazi, na kulala kwenye nyumba za serikali ambavyo vimetokana na kodi ya watanzania. lala usingizi wa kukoroma, maana mnalindwa. chadema itaendelea kupigania haki ya watanzania, msitufunge kamba za minyororo ya utumwa mara mbili; wafungeni wajinga sisi tumeamka. Chadema aluta kontinua!!!. kiboyo wewe huna kura ya kumpigia chadema.

    ReplyDelete
  18. Petro umesema kweli ndugu yangu tangu lini ukachoka bila kupata acheni huo ushamba wenu maana sasa na nyie mnatuboa sana kuwaona wanaharakati wachoke pamema kiasi hicho, hata Mwalimu Nyerere hakuchoka mapema mpaka kapata uhuru, ukisoma vitabu vya dini vinaeleza kabisa yesu alitufia msalabani ili na sisi tupate kuokolewa sasa nyie mnao mponda Slaa na Lisu mko wapi nyie hivi mnaelewa kweli ama mnaona raha tu kuandika huo upuuzi wenu nyie ndio mnatuchosha kabisa hii ni filamu mzee bila kufika mwisho story yake hutoelewa waache wanaofuatilia hii story wafike mwisho. tunajua mwisho sio sasa hivi ila ni lazima uwe na vipande vya kuunga ili story yako iwe na maana kwa wananchi huwezi kubweteka kama mvilivyobweteka nyie hapo mnaowasema Chadema oooh ni chama changu chama chako huku unawaponda mwanachama.Mwanachama gani wewe ambaye unachoka mapema hiyo ndio siasa kuukaa kimya sumu ss tulio na uchungu wa chama ndio tunaelewa sana nini wanachokitaka hawa jamaa.Chadema oyeeee na bado tunawaunga mkono ili tufike muafaka wa kuikamata nchi na sio kukata tamaa kwa wajinga wasiojua watasema sana ila kwa wanaojua nini maana kutafuta ushidi hawapati shida.Atafutaye hachoki akichoka ujue kapata Chadema hakuna kuchoka bado mnatafuta na tena ongeza bidii ili kukomesha wizi wa CCM. Lisu simameni imara na muwe makini maana wasijekujitokeza ndumilakuwila hapo kwenye kundi lenu.

    ReplyDelete
  19. chadema si wanssiasa ila ni wababaishaji na waganganjaa mara hatuviamini vyama vya TLP UDP NA NCCR, eti si vyama makini, halafu wanaruka ooh CUF wameungana na CCM Zanzibar wamevunja katiba, sasa mbona mnatutia aibu wajomba kueni na msimamo wa kiume, Zanzibar wanaserikali yao kamili upinzani wa bunge uko Tanzania Bara bunge linaongozwa na hio katiba mbovu tusioitaka mbona haya ni mambo mawili tofauti? kuweni wakweli shida hasa nini? kama kweli ni kuhusu Zanzibar na Cuf kwa nini hamukujiunga na vyama vingine, kwanza hii sheria kuunda kambi ya upinzani ina makosa makubwa sana,ili chama kiwe na haki ya kuunda kambi ya upinzani sharti kiwe cha kitaifa maana kiwe na wabunge kutoka pande zote za muunganu kama ilivyo sheria ya usajili wa vyama vya siasa, Watanganyika mkiwaendekeza Chadema mutapigana mapanga halafu chadema wataruka na helkopta lao nyinyi mnauana kwa ujinga wenu, watoto wao wote wanasoma nje ya nchi hawana shida hao wao wanalianzisha halafu hao,kazi kwenu.

    ReplyDelete
  20. Nyinyi munaochangia pengine muna mawazo mazuri lakini naamini wengi hawatoyasoma na kufaidika maoni yenu kwa vile namna mulivyoyaandika inakuwa tabu mtu ku concentrate.

    wakati munaandika, jaribuni kuweka paragraph au mstari mtupu kila baada ya mistari michache kama 5-7 na kuweka vituo kila inapohitajika.

    Mhariri wa Majira hana time ya ku edit makosa yenu ambayo kila siku yanazidi kurejea rejea.

    Jitahidini ili sote tufaidike na tuwafahamu!

    ReplyDelete
  21. Nionavyo ni kuwa chanyavu (chadema) shida yao ni Zanzibar kwa kuwa hawakupata hata kiti kiomoja,je wamesahau kuwa zenji ina mamlaka yake ? kuna kadi zao za uraia(ukaazi) kwa hiyo ya zenji ni kwenye baraza la wawakilishi ya muungano ni kwenye bunge msituchanganye,mmetumwa na wananchi katika majimbo yalioko bara kwa hiyo sifikirii kama walio wengi wana maslahi ya moja kwa moja na zenji,anzeni kazi kwa kuwatumikia walokutumeni sio kusema cuf hivi ama vile......
    hii haileti faida yoyote kwa raia........hata kama bunge watasema kuwa sio halali hiyo serikali ya zanzibar basi mjue kwamba bunge halina mamlaka zanzibar kwa hiyo ni kumpigia mbuzi gitaa,
    pia serikali hiyo ya zanzibar imeamuliwa na raia kwa hiyo ni kusema kuwa kuigeuza haiwezekani ama iitwe kura nyengine ya maoni
    wacheni zogo fanyeni kazi............
    ya zenji waachieni wenyewe na kama kukiukwa muungano haikuanza leo tangu mambo 11 mpaka yaliopo sasa ....je huu sio ukiukwaji ? kunya anye kuku, akinya bata ....
    Younde-kamerun

    ReplyDelete
  22. Ikiwa Chadema wanajifanya Ukoloni mambo leo basi Wzanzibar hatuko tayari kwa hilo tuko timamu na mitego yao.

    Lengo la Chadema nikuvunja Muungano kwa technic ya kutaka kuwatowa muhanga CUF, Haiingii akilini Chadema kuwasakama CUF kwa mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kifungu cha 10 na kutaka maelezo zaidi kwa Chama cha Wananchi CUF na Sio Baraza la Uwakilishi la (SMZ) .

    Jee Chadema wamesahau kuwa Zanzibar ni Nchi na ina Katiba yake na Sheria zake za Nchi bila kuingiliwa na sehemu nyingine yoyote? Kama SMZ wamevunja Katiba ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yupi alio anza kuvunja mwanzo halafu Zanzibar asulubiwe yeye wa hili?.

    Mumesahau Watanganyika mulipo vunja mkataba mama (Aticle of Unioni) Tanganyika na Zanzibar kwa kuitisha Bunge lenu la Tanganyika bila kuwashirikisha Wzanzibar na kuiuwa Tanganyika yenu?.
    Tanganyika ni kifoo chakujitakia wenyewe, na Kwa vile Tanganyika imekufa vipi sisi Wzanzibar tulinde Muungano na tudumishe Muungano ambao mshirika moja wa Muungano yani Tanganyika kavunja mikataba na makubaliano ya Muungano?.

    Wzanzibar siwapumbavu wa kupepea Mwiku au kuishi na Maiti, Hili wanalifahamu fika Chadema lakini wametawaliwa na Utanganyika wao kufumbia masho hakiza Wzanzibar ndio ukawaona hivi sasa wanaanza kuazirika na kujibainisha unafiki wao na ubaya wao kuwa suala la kutawaliwa kimabavu Zanzibar niletu pamoja Wtanganyika.

    Musijidanganye Chadema mukahisi Wzanzibar wako radhi na mfumo huu wa Muungano, Muungano usio na ridhaa ya Wananchi wenyewe sio Muungano na Prof Shevi wa Chuo kikuu amesa mara nyingi Muungano huu ni wakisiasa zaidi kuliko ridha za walioungana na unapendwa zaidi Bara kuliko Zanzibar ,kuishi kwa Muungano Zanzibar ni kuweko kwa Chama cha ccm.

    Wzanzibar tunaushukulia Muungano huu ni mzigo mzito tulio bebeshwa kwa nguvu bila tidhaa yetu na umeona uchaguzi ulio pita tulivyo mwagiwa Jeshi kutoka Tanganyika kuja kulinda Kolonilao, Vipi leo Zanzibar ilikuwa na utulivu mkubwa na kama ni hali ya hatari na kauli za umwagaji damu ilikuwa ni bara sio Zanzibar na nyiyi Chadema ndio mulio towa kauli za vitisho. Lakini tulimiminiwa Jeshi sisi Zanzibar na kukaa ktk zile sehemu nyeti Bandari,Tv,ikulu,Air port na kuwema Manuari yenu ya kijesh nje ya Zanzibar whay? huku ndiokutawaliwa kijeshi.

    Kwa hio Chadema kama munataka haki itendeke kwanza mujuwe haki za Zanzibar ktk Muungano na lapili mgomvi wenu awe ni Chama tawala CCM sio CUF musiwe mwenye sura ya unafiki panapo jitokeza haki za Zanzibar kulindwa mukaingiwa na ukirikimbwa wa Utanganyika musigeuke Mh Pinda mkoloni mweusi haki ni haki daini Tanganyika yenu ilioungana na Zanzibar ukapatikana huo Muungano,

    ReplyDelete
  23. Hatuwezi kuza utaifa wetu Wzanzibar ktk mdomo wa Muungano kama Tanganyika haipo na kujuwa kipi cha Muungano na kipi sio cha Muungano mukiweza kufanya hevyohaki itatendeka no metter kuwa Muungano haukufuata vigezo na ridhaa za wananchi lakini tunaweza kuendelea nao bila ya hivyo itakuwa Zulma na Wazanzibar hatuko tayari kuendeshwa mkenge wa kuuza utaifa wetu.
    Zanzibar ni nchi hata kama ina watu kidogo ukilinganicha na mikowa ya Bara lakini ni Nchi na ina historia yake miaka 200 na haiwezi kufutika aukuruhusu kufutwa historia yetu hii ni kwa faida ya kizazi shetu cha badae.
    Wala hatuko tayari kujisulubu kwa jina la Muungano kuitwa Wtanzania wa mkoa wa Pwani yaguju. Mungu ibariki Zanzibar na Wazanzibar wote

    ReplyDelete
  24. Chadema wanataka kujifanya Hero,lakini kwa Cuf bado kabisa hawajafika,mbowe hanauzoefu wa siasa ni mtoto mdogo sana hata ile sura ya usomi hana kabisa,anaonekana hata elimu yake mungu nsaidie,watanzania bara wengi wanasoma sio kwa kuelimika basi kwa kupata sifa,na kuwa na vyeti tu. Unapofanya challenge nae unajua kuwa huyu hakusoma.

    Chadema wanachotaka kuwa waonekane hero ili waweze na wao kuingizwa katika serikali ya ccm kuwa ccm b,kama vile wanavyofikia zanzibar kuwa chama cha chf si mpinzani tena,hawatambui ya kuwa kuingia serikali cuf ndio kufanya hayo mageuzi ambayo walikuwa wakiyaletea upinzani ili wawe na wao watendaji kama kulikuwa hakuna utendaji.

    sasa chadema wao wanataka kuwa wapinzani wa kuongea bungeni tu lakini hawataki kufanya kazi ya utendaji,kwali hii ndio democracy tunayoitaka ?

    Zanzibar na waliko zanzibar na wazanibari wote sasa wakati umefika kwa kupigana na adui zetu,watanzania bara sio marafiki kabisa wa kweli,wanajidai kutumia jina eti sisi sote watanzania ni ndugu,hapana, kiubinadamu ndugu,kidini ndugu ,lakini kiroho naona tofauti,kwa hiyo haina haja kuwa na watu kama hawa wenye roho mbaya na kuona zanzibar inapiga hatua na kiunuka kiuchumi na watu wake kufaidika,wanachotaka wao kuona tanganyika ikoo juu ili watutawale.

    Bakora ya hawa kuitumia katiba ya zanzibar,kama kuna marekebisho mengine fanyeni ili iwe fimbo kwao kama,idaya ya mambo ya ndani na nje kuweka katika katiba ya zanibar kuwa china ya zanibar na sio ya muungano,pili kuwa zanzibar ina jeshi lake la kulinda wananchi kama JWZ,tatu idara fedha,kuwa china ya zanzibar na kusimamia wazanibari wenyewe pamoja na kodi za zanzibar,rasilimali zote za zanzibar kuwa chini ya wazanzibar wenyewe.

    hapa ndio tutapiga hatua kubwa sana katika kuiletea maendeleo zanzibar, na hapo ndipo chadema na ccm ndio wataweka kongamano lao sio na cuf.

    Kumaliza kwa mgogoro wote kwa chadema ni kufanya KURA YA MAONI zanzibar.

    .

    ReplyDelete
  25. Waswahili wanasema mzarau kwao mtumwa,Ikiwa Tanzania ilikuwepo kabla ya Tanganyika na uhuru wa Tanzania ndio wa Tanganyika basi hilo nilenu wenyewe wala halina ushirikiano na Zanzibar wala Wazanzibar.
    Itakuwa ni kujibainisha zahiri kuwa Tanganyika haikufa ikonyuma ya Pazia la Tanzania lililo badilika ni jina tu nisawa na Zaire kuita Kongo?.
    Nyiyi ikiwa munajifanya wajanja ili Zanzibar ingie ktk kodi la Tanganyika (Tanzania) basi mumeula na shuwa, Sisi Wzanzibar niwajanja Zaidi kuliko nyiyi ndio ukaona Simba kanyeshwa chai Zanzibar.
    Wzanzibar tuko up 2 date ktk Utaifa wetu kwa hilo hatuna mchezo nalo tunaweza kuondoka na ushango wamtu mara moja. Longo longo zikiwa nyingi na blaa blaa tunaitisha kura ya maoni kuvunja Muungano ambolo Wazanzibar wanalisubiri kwa hamu litokee tumeshoka kutawaliwa ki-Jeshi na machogo.
    Sisi wazanzibar tunaona ufahari kujita Wazanzibar wa Zanzibar. Nyiyi Mukijita Watanzania kazi kwenu musije mukaazirika tu tukivunja Muungano, na sijuwi mutaendelea kujita Watanzania au Watanga Tanga ktk msitu wa Nyika?.

    ReplyDelete