25 November 2010

Baraza la mawaziri 2010.

Baraza la mawaziri hili hapa
BARAZA LA MAWAZIRI 2010
NO OFISI/WIZARA WAZIRI NAIBU
1 Ofisi ya Rais .    WN – OR – Utawala Bora

Mathias Chikawe
2.    WN – OR – Mahusiano
na Uratibu

Stephen Wassira
2 Ofisi ya Rais,
Menejimenti
ya Utumishi
wa Umma
Hawa Ghasia
3 Muungano. Samia Suluhu




  
4 Ofisi ya
Waziri Mkuu
Sera, Uratibu na Bunge

William Lukuvi 

5 Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tawala
za Mikoa na
Serikali za
Mitaa (TAMISEMI)
George Huruma Mkuchika 1.Aggrey Mwanri
2. Kassim Majaliwa
6 Wizara ya
Fedha
Mustapha Mkulo 1. Gregory Teu
2. Pereira Ame Silima
7 Wizara ya
Mambo ya Ndani
ya Nchi
Shamsi Vuai Nahodha Hamisi Kagasheki
8 Wizara ya
Katiba na Sheria
Celina Kombani
9 Wizara ya
Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa
Kimataifa
Bernard K. Membe 1.  Mahadhi Juma Mahadhi
10 Wizara ya Ulinzi
na Jeshi la Kujenga
Taifa
Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi
11 Wizara ya Maendeleo
ya Mifugo na Uvuvi
Dr. Mathayo David Mathayo 1.  Benedict Ole Nangoro
12 Wizara ya Mawasiliano,
Sayansi na
Teknolojia
Prof. Makame Mnyaa Mbarawa 1. Charles Kitwanga
13 Wizara ya Ardhi,
Nyumba na
Maendeleo ya
Makazi
Prof. Anna Tibaijuka Goodluck Ole Madeye
14 Wizara ya
Maliasili na Utalii
Ezekiel Maige
15 Wizara ya Nishati
na Madini
William Mganga Ngeleja 1. Adam Kigoma Malima
16 Wizara ya Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli 1. Dr. Harrison Mwakyembe
17 Wizara ya
Uchukuzi
Omari Nundu 1. Athumani Mfutakamba
18 Wizara ya
Viwanda na
Biashara
Dr. Cyril Chami Lazaro Nyalandu
19 Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya
Ufundi
Dr. Shukuru Kawambwa 1. Philipo Mulugo
20 Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii
Dr. Haji Hussein Mpanda 1. Dr. Lucy Nkya
21 Wizara ya Kazi
na Ajira
Gaudensia Kabaka Makongoro Mahanga
22 Wizara ya
Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na
Watoto
Sophia Simba Umi Ali Mwalimu
23 Wizara ya Habari,
Vijana na Michezo
Emmanuel John Nchimbi 1. Dr. Fenella Mukangara
24 Wizara ya
Ushirikiano wa
Afrika Mashariki
Samuel John Sitta Dr. Abdallah Juma Abdallah
25 Wizara ya Kilimo,
Chakula na Ushirika
Prof. Jumanne Maghembe 1. Christopher Chiza
26 Wizara ya Maji Prof. Mark James Mwandosya Eng. Gerson Lwinge
27 Mahusiano na
Uratibu.
Stephen Wassira
28 Mazingira Dr. Terezya Luoga Hovisa
29 Uwekezaji na
Uwezeshaji
Dr. Mary Nagu

12 comments:

  1. tuna waombea mawaziri utekelezaji mwema wa majukumu yao.mgosingwa

    ReplyDelete
  2. Kwa kuwa wengine hatujui utendaji wao, hatuwezi kulaumu au kusifu uteuzi. Tunawapa muda tuone utendaji wao. Hata hivyo, ninashauri kuwa pale rais atakapoona asiyewajibika kwa ufanisi basi mtu huyo aondolewe mara moja siyo kusubiri mpaka avurunde zaidi

    ReplyDelete
  3. pETRO eUSEBIUS mSELEWANovember 25, 2010 at 9:49 AM

    Jana nilisema Rais Kikwete atatuonyesha usanii wa CCM...si mmeona? Sasa tuna Mawaziri na Manaibu wao 50!!! Kwanza,ameunda Wizara mpya ambayo sio lazima iwepo,Wizara ya Ofisi ya Rais-Mahusiano na Uratibu ambayo amemkabidhi Mh.Stephen Wassira.Wizara hii itapoteza mishahara ya Kiserikali bure...usanii mtupu! Kuna haja gani ya kuwa na Ofisi mbili zinazoshughulikia Uratibu? Kwani ni uratibu wa nini hasa kama si vyeo vya kupeana tu? Pili,Mh.Rais si msikivu.Kuna haja gani ya kuwa na Wizara mbili zinazoshughulikia mambo ya nje? Kwani Afrika Mashariki ni NDANI?Jambo lingine ni kuwa hadi sasa Mh.William Lukuvi ana vyeo vya kitaifa vitatu:Mbunge wa Ismani,Mkuu wa Mkoa wa Dar na Waziri Mteule wa Sera,Uratibu na Bunge.Hii haki jamani? Ye kwani nani hasa? Kwakuwa mi si mnafiki napongeza kwa moyo wangu wa dhati uteuzi wa Prof.Anna Tibaijuka,Dr.John Pombe Magufuli na Dr.Harrison Mwakyembe ambao wote wapo kwenye Wizara Stahiki..Ila hakukuwa na sababu ya kuigawa Wizara ya Miundombinu.Kwa hawa wateule,mambo yangewezekana...Mzigo mzito mpe
    Msukuma!Kilichofanyika hapa si lolote ila kuunda ajira mpya tu.Kwanza kubadilibadili Wizara namna hii kunaleta tabu kubadili majina ya majengo ya ofisi na hata 'platenumber' za magari ya waheshimiwa.Pia haionyeshi muendelezo wa majukumu ya kiserikali...kila siku mambo yanaanza upya!Mh.Kawambwa ni mtalii wa Wizara mbalimbali? Kwanini asitulie sehemu moja tumpime uwezo wake? Mh.Sitta,ile Ofisi ya Spika kule Urambo aigeuze Ofisi ya Afrika Mashariki.Kwakuwa wengi ni wapya tusubiri ili tuone meupe na meusi yao.Tuwe na subira...Mh.Kikwete ingia na timu yako Uwanjani.

    ReplyDelete
  4. Mhariri, Majira

    Ahsante kwa hii taarifa. Fanya kazi ya uandishi ya ziada kwa kutuwekea picha za wateuliwa husika.

    ReplyDelete
  5. Wizara 29, GDP ya Tz below USD 25 billion, hapa kidogo JK ume overlook!

    Kwa nini usijenge kikosi kibunifu cha wachapa kazi kama wizara chini ya 15, ndani yake manaibu mawaziri proffesionals kushughulikia matatizo na maendeleo mbali mbali ya nchi.

    Pia, ungelipamba baraza lako kwa kuwaingiza qualified opposition MPs kwa lengo la kuwa wewe ni Raisi wa raia wote, wakiwemo wasiokuchagua.

    Hata hivo unastahili CREDIT kuweza ku double Tz per capita GDP within 5 years!

    Be focused, economy inaweza ikawa legacy nzuri ya utawala wako!

    ReplyDelete
  6. Sina tatizo na wasifu wa mawaziri walioteuliwa wala ukubwa wa baraza hili. Tatizo lipo kwenye uwekaji vipaumbele. Hotuba ya Raisi inaonesha kuwa kwa miaka mitano serikali itafanya kila kitu. kwa jinsi hiyo ni lazima awe na baraza kubwa kama hili la mawaziri. Sitarajii mawaziri hawa watafanya miujiza kufanya makubwa yanayoonekana kwa kugawana ka-sungura tulikonako na kwa kubembeleza huruma ya majirani ambao pia wanaotea uzembe wetu ili wanufaike na tulichonancho. Laiti Raisi na washauri wake wangechagua vipaumbele vichache kulingana na uwezo tulionao, vipaumbele ambavyo vikitekelezwa vitainua uwezo wetu wa kufanya makubwa zaidi msimu ujao, angegundua kuwa hahitaji mlolongo wa mawizara kama huu.

    ReplyDelete
  7. Kusifu ni baada ya kuona utendaji wa kazi. Natumaini watafanya kazi kwa ajili ya/ na Watanzania na sio ubinafsi.... jamani ufisida Tanzania umezidi!!! Naomba nyie mawazili kufanya kazi kwa kushirikiana na Watanzani.

    ReplyDelete
  8. Mimi namuunga mknono Dr. Slaa, katibu wa Chadema, kuwa uteuzi unaozingatia "USWAHIBA" badala ya uwezo wa mtu ni hatari kwa kuwa unalenga kumpatia kila rafiki Uwaziri.Mawaziri wanaotokana na bunge ni hatari sana!!!

    ReplyDelete
  9. HONGERA SANA MHE. RAIS KWA BARAZA LAKO TUKUFU LA MAWAZIRI 2010-2015. ILA CHAGA DEV.MAN HAWATAKAA WAFURAHIE KWANI UCHU WAO WA KUINGIA IKULU UMEGONGA MWAMBA. SASA MUDA UMEFIKA KWAO KWENDA KULA MIHOGO HUKO KEWENYE MAJIMBO YAO HASA MHE... KAMA ALIVYODAI KWAMBA AKIINGIA IKULU BASI ANGEKUNYA CHAI NA MIHOGO ILI KUBANA MATUMIZI ILI FEDHA YAKE AIPELEKE KULETA MAENDELEO YA WANACNCHI. MBONA ALIPOKUWA MBUNGE HAKULA MIHOGO BUNGENI ILI MARUPURUPU YAKE AWPELEKEE WANACHI WALIOMCHAGUA????

    ReplyDelete
  10. NA HAO CHADEMA WANAODAI KABWE KAKIKOSEA HESHIMA CHAMA CHAKE, JEE HAO WABUNGE WA CHADEMA HAWAJAWAKOSEA HESHIMA WANANCHI WALIOWAINGIZA BUNGENI NA HATIMAYE KUJISAHAU KWAMBA WALIAPA NINI...?

    ReplyDelete
  11. WIZARA NYETI KAMA,ELIMU,ULINZI,FEDHA,MAMBO YA NDANI,SAYANSI NA TECHNOLOGIA,KILIMO ZIKO KWA AKINA NANI???? KIKWETE KADHIIRISHA UDINI ALIOKUWA ANAUKATAZA,HONGERA KIKWETE KWA KUWEKA MBELE UDINI

    ReplyDelete
  12. Hakuna jipya ni uswahiba atakiona cha moto, kwa sasa tunaongelea mabadiliko ya katiba na yatakuja kwa nguvu ya umma na si kuomba kwa JK

    ReplyDelete