Na Theonestina Juma, Bukoba
WANANCHI wenye hasira wamemuua Bw. Charle Mushozi, maarufu kwa jina la Kalwani (25-30) baada ya kumfumania nyumbani kwao akimbaka mpwaye mwenye umri wa
miaka saba.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mjini hapa na kuthibitiswha na Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Bw. Henry Salewi, tukio hilo lilitokea Novemba 14, mwaka huu saa 11 alfajiri katika Kijiji cha Ibosa Kata ya Nyakato katika Wilaya ya Bukoba.
Kamanda Salewi alisema alfajiri hiyo, baba wa mtoto huyo, Bw. Wilbard Kalebe alikuwa ameondoka kwenda ziwani kuvua samaki kwa ajili ya kitoweo, na nyumbani alibaki mama mzazi wa mtoto huyo, Bi. Veronika Kalebe (38).
Ilidaiwa kuwa wakati wa tukio hilo, mama mtoto huyo alisikia makelele ya mwanawe kwenye chumba anamolala, ambapo alilazimika kuchoka mbio ili kwenda kungalia kulikoni ambapo alipofungua mlango alimkuta mdogo wake huyo wa kiume akitoka kwa kunyata akiwa ameshikilia suruali.
Kutokana na hali hiyo, Bi. Kelebe alilazimika kupiga makelele huku akimfukuza kulelekea nje ya nyumba, ndipo lilitokea kundi la wananchi ambao walianza kumshambualia huku akilia na kuomba asamehewe kutokana na kosa lilotenda.
Alisema kuwa wananachi baada ya kusikia kauli ya kijana huyo akikiri kwamba amembaka mtoto huyo, walipandwa na jazba na kuendelea kumshambulia kwa mawe na marungu hadi kufa.
Hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusika na mauaji hayo, na mtoto aliyebakwa alikutwa ameharibiwa vibaya sehemu zake za siri.
Wakati huo huo, polisi mkoani hapa wanamshikilia Bi. Advera Kennedy (45) mkazi katika kijiji hicho kwa tuhuma za kukifukia shimoni kichanga cha siku moja na kukisababishia kifo.
Kamanda Salewi alisema kuwa tukio lilitokea Novemba 8, mwaka huu ambapo mwanamke huyo alifika nyumbani kwa Bi. Paulina Lwakatare (64) mkazi wa Kijiji cha Kiilima ambacho kiko katika kata ya Nyakato na kumuomba msaada ili aweze kumzalisha.
Alisema Bi. Lwakatare ambaye ni mkunga wa jadi katika kata hiyo alimzalisha na baadaye Bi. Advera aliondoka na kurudi nyumbani kwake na kichanga chake kikiwa hai na chenye afya.
Alisema kuwa mauaji ya kichanga hicho yalibainika Novemba 15 mwaka huu baada ya mkunga huyo kwenda nyumbani kwa mzazi huyo kumjulia hali na kudai kitenge chake alichomwazima Bi. Advera kumbebea mtoto.
Alisema kuwa baada ya mkunga huyo kufika nyumbani kwa mzazi huyo hakukuta mtoto ambapo alimuuliza habari za mtoto ndipo alipojibiwa na mzazi kuwa yeye hakuwahi kufika kwa mkunga huyo, hajawahi kuzaa na hakijui kitenge alichokuwa anaelezwa
Alisema kuwa baada ya bibi huyo kujibiwa hivyo alikwenda na kutoa taarifa katika Serikali ya Kijiji cha Ibosa na baadaye polisi, ndipo askari walifika kwa mzazi huyo na kumuhoji akakiri kutenda kosa hilo na kuomba asamehewe, polisi walimtaka awapeleke alipokizika kichanga hicho.
Alisema mtuhumiwa aliwapeleka katika pori lililoko nje kidogo na kijiji hicho kwenye shimo la kukatia mbao alikokuwa amekifukia kichanga hicho, ndipo kilifukuliwa na mwili wake ukapelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera na taarifa ya hospitali inasema kuwa mtoto huyo alitokwa na damu nyingi kitovuni.
Kamanda alisema kuwa mwanamke huyo atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika huku wakiendelea kufuatilia vipimo kama mama huyo ana akili timamu au la.
Mimi hujiuliza kila mara,hivi hawa wanaobaka watoto kama wa umri huu wanamaumbile madogo au unyama tu? Lakini,wananchi wamepelekeshwa mno na hasira zao.Wangempa muda wa kumhoji Marehemu ili kuweza kujua sababu za yeye kufanya unyama kama huu.Labda wananchi wangepata majibu na sababu ambazo zingepelekea kudhibiti hali kama hiyo isijirudie tena.Hatahivyo,binafsi nalaani kwa nguvu zangu zote tukio kama hilo.Kuhusu mtupa mtoto,nalaani na kuziomba Mamlaka husika pamoja na jamii kwa ujumla kutafuta sababu za tatizo hili rudiwa ili kulimaliza.
ReplyDeleteNdio dawa yao! hakuna kuwapeleka mahakamani, rushwa, kupindisha sheria, ujanja ubabaishaji vimetawala huko, dawa ndio hiyo! piga! ua! liwe fundisho kwa wengine
ReplyDeleteMzinifu hiyo ndio dawa yake!
ReplyDelete