Na Mwali Ibrahim
TIMU ya taifa ya kuogelea kutoka Klabu ya Stingrays, juzi imewasili nchini na medali 74, ilizozipata katika mashindano ya wazi ya mchezo huo yaliyofanyika, Lilongwe nchini Malawi Oktoba 22 na 23, mwaka
huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana katika hafla ya kuwapongeza wachezaji ha,o iliyofanyika katika bwawa la kuogelea la Funkys, Masaki mkuu wa msafara wa wachezaji hao, Ramadhani Namkoveka alisema mashindano hayo yalishirikisha nchi tatu za Malawi, Tanzania na Zambia.
Katibu huyo alisema katika mashindano hayo, Tanzania ambayo ilipeleka waogeleaji 23, ilishika nafasi ya tatu.
Alisema, mashindano hayo yaliandaliwa vizuri na yalikuwa ya ushindani mkubwa ambapo, walifanikiwa kupata medali za dhahabu 16, fedha 22 na shaba 36.
Namkoveta alisema, katika mashindano hayo wamejifunza mambo mengi ukiwemo mfumo mzuri wa kurekodi matokeo ya waogeleaji, Pia yaliandaliwa vizuri na Wamalawi waliungana kuishangilia timu yao.
“Huo ni mfano mzuri sana, hasa timu inapokuwa katika mashindano kwani kuwashangilia wachezaji wenu kwa wingi kunatoa hamasa na ari ya wachezaji hao kuongeza juhudi ili kuweza kupata ushindi,” alisema Namkoveka.
Namkoveka aliwasifu wachezaji, Neena Patel na Christian Dom ambao walikubali kucheza na waogeleaji wenye umri mkubwa, ili kukidhi masharti ya mashindano na waliweza kufanya vizuri katika hatua hiyo na mchezaji Christina (10), kung'ara kwa kupata dhahabu moja, fedha sita na shaba tatu ambapo aliogelea na wachezaji wenye umri wa miaka 11 na 12.
Naye Neema (12), aliogelea na wachezaji wenye umri wa miaka 13 na 14 na kupata fedha moja ambapo muogeleaji, Christian Opperman (10) ambaye alishiriki matukio 8 na kupata dhahabu 6, fedha 1 ndiye aliyeng'ara zaidi.
Namkoveka alilishukuru Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa kuwapokea pamoja Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA) kwa mchango wake katika kuendeleza mchezo huo.
No comments:
Post a Comment