DUBAI, Falme za Kiarabu
WAYNE Rooney alifanya ziara nchini Dubai kusherehekea miaka 25 ya kuzaliwa kwake ambapo ameteketeza sh. milioni 207 kwa siku tano, akiwa na mkewe, Coleen huku wamemwacha mtoto wao
Kai.
Ziara hiyo ililenga kuweza kumwondolea mawazo mkewe Coleen, baada ya kutowepo hali ya kuelewana tangu zilipotoka habari kuwa alifanya mapenzi nje ya ndoa na kahaba.
Pati ya awali ilipangwa kufanyika London kabla ya kuahirishwa, ili kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ambayo imegharimu kiasi cha pauni 90,000 (zaidi ya sh.milioni 207) katika siku tano, ambapo watu 100 walipangwa kuhudhuria na kuhudumiwa chakula na viwanji.
Wanandoa hao walisafiri kwenda Dubai kwa ndege ya United Arab Emirates, kisha kujiachia mbele za watu wakiwa katika hoteli ya kifahari ya Atlantis kwenye nchi iliyokuwa na nyuzijoto 36F.
Gazeti la Sun limeeleza jinsi, Rooney alivyoadhimisha miaka yake 25 ya kuzaliwa Jumapili akiwa katika hoteli waliyofikia, ambayo ina baa na bwawa la kuogelea.
Mwanasoka huyo amesaini mkataba mwingine katika Klabu ya Manchester United, ambapo atakuwa akipata mshahara wa pauni 250,000 (zaidi ya sh. milioni 575 kwa wiki.
Katika hoteli hiyo, wawili hao walionekana wakila kunywa na kwenda kuogelea kwenye bwawa na kulikuwa na ulinzi mkali.
Wenza hao kuna wakati walionekana kuwa na wasiwasi kutokana na kuanguka glasi wakati wakila mlo wa mchana, ambapo Rooney, alionekana akimfokea
Coleen mwenye umri wa miaka 24.
Mmoja wa mashuhuda alisema, walikuwa wakitamani kwenda kumsalimia Rooney kwa kuwa wao ni mashabiki wao, lakini mlinzi aliwakatalia.
Kitendo cha Rooney, kufoka kutokana na kuvunjika kwa glasi kiliwakera baadhi ya watu waliokuwa wakiwaangalia.
Mama mmoja wa kingereza, aliyekuwa karibu yao alisema: "Wanafedha zote katika Dunia kwa sasa, lakini hawaonekani kuwa na furaha wanaonekana bado kuwa katika matatizo."
Shuhuda mwingine alishangazwa na hali ya kuchuniana kwa wawili hao, wakati wakiwa katika hoteli ya nyota saba ya Burj al Arab.
Naye shuhuda mwingine alisema, aliwaona wakiwa peke yao bila ya kuwa na mashabiki, wala wapiga picha na kila mmoja alikuwa kimya. Coleen alikuwa amekaa huku, Rooney akiwa wima mbali kidogo naye.
"Hakuna aliyekuwa akizungumza na mwenzie, kufurahi wala kugusana katika siku ya Jumapili, ambapo walikuwa katika bwawa la kuogelea, kila mtu akiongea kivyake na kuota jua.
Mmbeya huyo aliyekuwa akiwafuatilia, alisema katika saa mbili wawili hao hawakuzungumza, hawakuwa kwenye kufurahiana wala kuzungumza, hali hiyo ilikuwepo pia Jumatatu.
Coleen kisha alikwenda kula chakula cha mchana kisha Rooney, alimfuata na kuungana naye mezani.
Hoteli waliyokuwa nyota hao, gharama yake ni pauni 2,600 (zaidi ya sh. milioni 5.9 kwa siku.
Rooney ambaye alikosa mechi ya Ligi Kuu Jumapili ugenini, wakati timu yake ya United ilipocheza na Stoke kutokana na kuumia enka, kuna wakati alionekana akizungumza na Waingereza wenzake waliokuwa katika hoteli hiyo wakati wakinywa bia.
Wanandoa hao walikuwa wakitarajia kuwa ziara hiyo, ingesaidi kuponya makovu baada Rooney, kujulikana kuwa alifanya mapenzi na makahaba wawili, Jenny Thompson na Helen Wood.
Rooney alilazimika kumwomba msamaha, mkewe na kumsihi wasitengane kwa ajili ya kumlea mtoto wao mdogo, Kai. Lakini marafiki zao wanasema Coleen bado anasumbuka kusamehe moja kwa moja kutokana na usaliti wake.
No comments:
Post a Comment