LONDON, Uingereza
KIPA wa Chelsea, Petr Cech anaamini timu yake ina nafasi ya kutetea ubingwa wake, katika msimu huu baada ya kujiweka vyema.Vijana wa Carlo Ancelotti, waliifunga Wolves mabao
2-0 mwishoni mwa wiki, lakini wakawashudia wapinzani wao wa London, Arsenal wakiwakaribia baada ya kuifunga Machaster City, mabao 3-0 na kuwafanya kuwa na tofauti ya pointi tano kati yao.
Mabingwa hao watetezi walianza ligi vizuri na kujikuta wakishinda mabao 21, katika mechi tano za kwanza.
Lakini Cech, alisisitiza kuwa si lazima timu yao kufunga mgoli mengi.
Kipa huyo alisema: "Kama hufungwi, unakuwa na nafasi nzuri ya kushinda mechi.
"Sisi hatujafungwa magoli nyumbani, lakini kitu cha muhimu zaidi ni kwamba tunashinda mechi zetu.
"Unatakiwa kutofungwa na kushinda mechi kila wakati, lakini nimefurahi kwa kutofungwa kwetu kunasaidia kushinda mechi.
"Msimu uliopita rekodi yetu ya nyumbani ilitusaidia kutwaa makombe mawili, hivyo ninatumaini kufanya hivyo msimu huu."
No comments:
Post a Comment