LONDON, Uingereza
KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho anataka kuona mlinzi Pepe, akieeleza nia ya kubakia katika Uwanja wa Santiago Bernabeu wiki ijayo.
Kocha huyo wa kireno anaamini, Pepe mwenye umri wa miaka 27 bado ni mchezaji muhimu kwa timu yake.
Mkataba wa sasa wa Pepe, unamalizika mwaka 2012 na Madrid iko tayari kumwongezea miaka mitatu, ili kumzuia mchezaji huyo ambaye anatakiwa na timu za Chelsea na Barcelona.
Alisema: "Real Madrid inajaribu kutompoteza na Pepe, hawezi kupotezwa na Real Madrid.
"Klabu inajua katika wiki chache itaweka sawa kila kitu na Pepe atabakia hapa."
No comments:
Post a Comment