Na Shaban Mbegu
Klabu ya Yanga jana imetangaza kuwa ndiyo siku rasmi ya upigaji
kura za maoni kwa ajili ya kuchagua timu hiyo iwe kampuni au kutokuwa kampuni.
Katika mkutano
wa kawaida wa wanachama uliofanyika Januari 16 mwaka huu Mwenyekiti wa klabu
hiyo, Yussuf Manji kwa niaba ya Kamati ya Utendaji alitoa mapendekezo kwa
wanachama juu ya timu kuwa kampuni.
Katika
mapendekezo hayo, Mwenyekiti huyo aliwaeleza wanachama juu ya umuhimu wa
kampuni na kuwataka kutafakari kwa makini juu ya jambo hilo. Pia aliwaeleza
kuhusu kuwepo kazi ya kupiga kura za maoni, ili kuweza kuona mawazo ya
wanachama ambao ndiyo wenye klabu hiyo wanasemaje juu ya jambo hilo.
Kaimu Katibu
Mkuu wa timu hiyo, Lawrence Mwalusako akizungumza katika mkutano wa waandishi
uliofanyika katika makao makuu ya klabu hiyo, alisema kuwa hiyo ndio siku rasmi
kwa ajili ya kazi hiyo.Alisema kila
mwanachama ambaye yupo hai ataruhusiwa kupiga kura, lakini atalazimika kufika
na kadi yake ili kuepuka na wajanja watakaotaka kurudia mara mbili.
“Nachukua
nafasi hii kuwaambia wanachama wa Yanga, kuanzia leo tarehe 16 mpaka Novemba 10
mwaka huu, kutakuwa na sanduku moja hapa klabuni kwa ajili ya kura za maoni,”
alisema.Alisema
kutakuwa na kura za aina mbili, za kukubali kuwa kampuni zitakuwa kwenye
karatasi iliyoandikwa (NDIYO) au (HAPANA) kwa wale wasiotaka kuwa kampuni.
Katibu huyo
alisema viongozi wameona watumie busara katika kufanikisha jambo hilo na ikumbukwe kuwa
shughuli hiyo ni muhimu kwa ajili maendeleo ya Yanga.Ak i z u n g
umz i a k u h u s u wanachama wa mikoani kama wa t awe z a j e k u p i g a k u
r a , Mwalusako alisema itakuwa ni jambo gumu kwa wao kwenda kila mkoa.
Akifafanua
kauli hiyo alisema kuwa watu wa mikoani si ‘watata’ kama ilivyo wa Dar es Salaam, pia
viongozi na waasisi wa timu hiyo wapo jijini.“Unajua hapa
ngoja niwe muwazi, Dar es Salaam ndiyo kuna watu
watata ambao kama hujaenda nao sawa na
kuwaelesha vizuri inaweza kuleta tatizo kubwa.
“Kuna kama
hawa wazee wetu, wengi ndiyo wenye Yanga, wanaijua kiunaga ubaga kuanzia tangu
ilipoanzishwa mpaka leo, sasa hawa ndiyo kila kitu kwa kweli,” aliongeza.Lakini
Mwalusako alienda mbali na kudai kuwa watu wengi wa mikoani watapata fursa hiyo
kupitia mchezo wao na Simba utakaopigwa Jumapili ijayo.
“Tulisubiri mpaka
kuelekea pambano la watani wa jadi, ndiyo zoezi hili (shughuli) lianze kwa kuwa
tunaamini kuna wanachama wengi watakuja kuangalia mchezo huo na hiyo itakuwa
fursa kwao kupiga kura za maoni,” alisema.Akizungumzia
maandalizi ya mchezo wa Jumapili, Mwalusako alisema wao kama
viongozi wamemaliza kila kitu kwa ajili ya mchezo huo.
Mchezo huo wa
mzunguko wa tisa utapigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba yenyewe
imejificha Bamba Beach Kigamboni nje kidogo ya Dar es Salaam kwa ajili ya
kufanya maandalizi ya mchezo huo wa kihistoria.
Mwalusako ambaye ni
beki wa zamani wa timu hiyo, alisema kilichobaki kwa sasa ni kazi ya benchi la
ufundi la timu hiyo kumaliza kazi iliyobaki.“Sisi kama uongozi
tumemaliza kazi yetu kwa asilimia kubwa, benchi la ufundi ndiyo limebaki na
jukumu la mwisho kwa ajili ya kuandaa timu hiyo,” alisema.
Aliongeza kuwa mchezo
huo utakuwa ni mgumu japokuwa wana imani na kikosi chao kuibuka na ushindi
katika mchezo huo kutokana na kuwa na wachezaji bora.“Tuna kikosi bora na
kizuri, pia tumejiandaa vizuri, naamini utakuwa mchezo mgumu, japokuwa tuna
imani ya kushinda, lakini chochote kinaweza kutokea kwa kuwa soka ni mchezo wa
bahati,” alisisitiza.
Wakati huo huo,
Meneja wa Yanga, Hafidhi Salehe amesema timu yao
ipo vizuri tangu walipotua Pemba kwa ajili ya
kambi ya kujiandaa na mchezo wa mahasimu zao Simba.Hafidhi alisema kwa
sasa wanafanya mazoezi ya nguvu na jana walikwenda ufukwe wa Misali, ili
kuwajenga wachezaji kuwa na nguvu pamoja na pumzi za kutosha.
“Timu inaendelea
vizuri na mazoezi leo jioni (jana), tunacheza na timu moja ya huku ikiwa ni
sehemu ya mazoezi kwa ajili ya mchezo huo, pia tunashukuru kwamba hatuna
majeruhi katika kikosi chetu,” alisema.
Alisema
wamefurahishwa na hali ya hewa ya Pemba kuwa
ya utulivu, ambapo wachezaji wamekuwa na hamasa kubwa ya kuhakikisha wanapata
ushindi katika mchezo huo.
S imb a n a Ya n g a z o t e zimeshacheza michezo nane, lakini
wametofautiana kwa pointi tatu ambapo Wekundu wa Msimbazi ndiyo wanaongoza ligi
kwa pointi 18, huku Yanga wakishika nafasi ya nne kwa pointi 15.
No comments:
Post a Comment