Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
limemuomba radhi mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe aliyenyimwa mpira na
mwamuzi aliyechezesha mechi ya Ligi Kuu kati ya timu yake dhidi ya Mgambo
Shooting, baada ya kupachika mabao manne.
TFF imesema kutokana na hatua
hiyo ambapo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ilishinda mabao 6-0,
mwamuzi huyo hataadhibiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa
TFF, Boniface Wambura alisema kitendo cha mchezaji kupewa mpira pale anapofunga
mabao kuanzia matatu katika mechi moja halipo kwenye sheria ya ilani imani ya
haki katika mpira wa miguu 'fair play'.
Wambura
alisema walimuita, Tambwe wakamuomba msamaha ambapo muda wowote kuanzia sasa
anajipanga, ili kuuchukua mpira wake. Katika mechi hiyo mabao mawili yalifungwa
na Haruna Chanongo hivyo kufanya idadi ya mabao kuwa 6-0
No comments:
Post a Comment