Nasra Kitana na Shufaa Lyimo
Kocha
Mkuu wa timu ya Simba, Abdallah Kibadeni amesema leo anatarajia kuanika
mikakati yake, ambayo ataitumia Jumamosi watakapocheza na Prisons katika mchezo
wa Ligi Kuu jijini Dar es Salaam.Akizungumza na waandishi wa habari hizi jana
kwa simu katika kambi hiyo iliyopo Bamba Beach, Dar es Salaam, Kibadeni alisema
kiujumla timu inaendelea vizuri na mazoezi.
"Tupo tumetulia tunaendelea vizuri na
mazoezi kuhakikisha Jumamosi tunatoka na ushindi," alisema Kibadeni.Vile
vile aliongeza kuwa timu yake imeanza mazoezi Jumatatu, ambapo kila mchezaji
ana morali ya hali ya juu."Tulianza mazoezi Jumatatu kwa ajili ya mchezo
huo, ambao naamini utakuwa na ushindani mkubwa," alisema.Alisema mikakati
hiyo, ambayo ataianika ni kwa lengo la kuchukua ubingwa mapema kabla Ligi Kuu
haijamalizika.Simba inashika nafasi
ya kwanza katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 15.
No comments:
Post a Comment