Na Fatuma Rashid
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji
chake cha Redd's Original, imezindua tamasha la mitindo na ubunifu kwa
wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini, litakalojulikana kama 'Redd's
Uni-Fashion Bash'
Akizungumza
katika uzinduzi huo Dar es Salaam jana, Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah
alisema tamasha hilo
lenye lengo la kuinua vipaji vya wanafunzi katika tasnia ya mitindo,
linatarajiwa kuanza mwezi huu na kumalizika mwezi ujao.
Butallah
alisema, tamasha hilo
kwa sasa litashirikisha vyuo vyote vya elimu ya juu vilivyopo katika Mikoa ya
Dar es Salaam, Iringa, Kilimanjaro na Mwanza.
" Tunataka
kuinua vipaji vya wanafunzi wa vyuo katika tasnia ya mitindo, kupitia maonesho
yatakayofanywa na wanafunzi wa vyuo hivyo, hapa tunataka wale wenye ubunifu
kuonesha ubunifu wao wa mitindo, hivyo hii ni fursa kwao kujitangaza na
kudhihirisha uwezo wao," alisema Butallah.
Kuhusu ushiriki,
Butallah alisema kutakuwa na fomu maalumu zitakazosambazwa katika vyuo husika,
ambapo wanafunzi wanamitindo na wabunifu watazijaza na majaji watazipitia na
kupata wabunifu 10 na wanamitindo wa idadi hiyo kutoka kila mkoa, ambao
watapata fursa ya kuonesha mavazi yao
siku ya tamasha.
Kuhusu zawadi, Meneja Habari na Mawasiliano
wa TBL, Edith Mushi alisema kutakuwa na zawadi mbalimbali ambapo washindi
watano wa ubunifu na idadi kama hiyo ya
wanamitindo kutoka kila mkoa wataondoka na fedha taslimu.
Edith alisema kwa upande wa wabunifu mshindi
wa kwanza ataondoka na sh. 700,000 wa pili sh. 500,000, wa tatu sh. 300,000
huku wa nne na wa tano kila mmoja akiondoka na sh. 100,000. Kwa upande wa
wanamitindo mshindi wa kwanza atapata na sh. 500,000 wa pili sh. 400,000 wa
tatu sh. 300,000 wakati wa nne na wa tano wakipata sh. 100,000 kila mmoja.
No comments:
Post a Comment