Na Penina Malundo
Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA), imezitaka mamlaka husika kuchukua tahadhari kukabiliana na
mafuriko yanayoweza kutokea msimu wa mvua ili kukabiliana na madhara ambayo
yanaweza kusababishwa na mafuriko yakiwemo magonjwa ya mlipuko.
Akizungumza
na wadau mbalimbali Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Ibrahim
Nassib, alisema utabiri unaonesha kutakuwa na mvua za wastani katika baadhi ya
maeneo. Nassib alisema TMA inapotoa taarifa za
utabiri, mamlaka husika zinatakiwa kushirikiana bega kwa bega ili kujua ni
jinsi gani wataepuka madhara yanayoweza kuletwa na mvua hizo.
Alisema taarifa za mamlaka hiyo zinatakiwa
kufanyiwa kazi kikamilifu ili kusaidia wananchi kuepukana na madhara
yatakayojitokeza.Aliongeza masuala ya hali ya hewa yanaendana
na masuala mbalimbali ikiwemo ya afya, kwani asilimia kubwa mvua za msimu
zinapoanza kunyesha hutokea magonjwa mengi ya mlipuko.
Naye Mjumbe wa Bodi ya TMA, James Ngeleja,
alisema taarifa hizo za hali ya hewa ni muhimu kwa masuala ya afya kwani
mamlaka hizo zitatakiwa kuchukua tahadhari stahiki ikiwa ni pamoja na kuzibua
mitaro na kuondoa mashimo yanayohifadhi mbu.
No comments:
Post a Comment