Na Rachel Balama
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limempongeza Rais Jakaya
Kikwete, kukutana na viongozi wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni na
kujadili maendeleo ya mchakato wa Katiba Mpya kwa amani na utulivu.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa BAKWATA, Shekhe Suleiman
Lolila, wakati akitoa salamu za baraza la Idi katika Msikiti wa Aly Farouk
jijini Dar es Salaam.
Alisema kitendo cha Rais Kikwete, kukubali kukutana na viongozi
hao, kinaonesha kuwa mchakato wa Katiba Mpya unaoendelea nchini utafanyika na
kumalizika kwa amani na utulivu.
Alisema rais alitumia busara na kuonesha ustaarabu wa hali ya juu,
pale aliporuhusu kuanzishwa kwa mchakato mzima wa Katiba Mpya, ambayo itakuwa
ndiyo dira na mwongozo wa nchi kwa vipindi vingine vijavyo.
Aidha, aliwataka wale wote wanaosimamia amani wasimame kidete
kutekeleza hilo
na kuwaonya wale wanaofanya dhuluma, uonevu ili kila Mtanzania popote alipo
aweze kufaidi matunda ya amani.
Oktoba 15, mwaka huu, Rais Kikwete, alikutana
na viongozi hao Ikulu, Jijini Dar es
Salaam ili kujadili mapendekezo ya kuboresha sheria ya
kurekebisha sheria ya mabadiliko ya katiba.
Shekhe Lolila, aliitaka Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi kusitisha utekelezaji wa mchakato wa kutotahiniwa kwa masomo
ya dini katika mitaala ya elimu ya sekondari na pia kufanya mazungumzo na
viongozi wa shule zinazoendeshwa na taasisi za dini ili kufikia mwafaka.
Naye, mgeni rasmi katika Swala ya Baraza la
Idi, Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, aliwataka Watanzania kwa ujumla
kuepuka ushabiki kwa jambo lolote lile ili kudumisha amani.
Alisema pia ni vyema Waislamu wakadumishe
maadili ya dini yao kama
wanavyoelekezwa katika vitabu vitakatifu ili kudumisha amani na kwamba Serikali
ipo makini kuhakikisha amani ya nchi inaendelea kuimarika.
Pia aliwataka Waislamu kutafuta elimu popote
pale duniani kwa kuwa Serikali imeweka sera nzuri katika elimu na kuwataka
kuongeza michango yao
kwa ajili ya elimu ya juu. Alisema kwa sasa michango wanayotoa hailingani na
wingi wao.
Aliwataka viongozi wa dini hiyo wafikirie
kuanzisha chuo kikuu kingine katika kanda mbalimbali hapa nchini ili kuandaa
vijana na kuzalisha wataalamu.
"Chuo Kikuu cha Kiislamu kipo kimoja tu
Morogoro, hivyo kutokana na wingi wenu hamkustahili kuwa na chuo kimoja tu,
jambo ambalo halistahili," alisema Profesa Maghembe.
Naye, Kaimu Mufti, Shekhe Abibu Makusanya,
aliitaka Serikali ioneshe makali kwa kuhakikisha wale wote wanaoonesha ishara
mbaya za uvunjifu wa amani wachukuliwe hatua za sheria ili iwe mfano kwa
Watanzania wengine.
Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar,
Dkt. Ali Mohamed Shein, amewataka Wazanzibari kuyachukua mafunzo ya ibada ya
Hijja kuwa mwongozo wa maisha yao
ya kila siku.
Rais Dkt. Shein ameeleza hayo jana wakati
alipokuwa akizungumza katika Baraza la Idi Mkoa wa Kusini Unguja.Katika hotuba
yake hiyo ambayo alitilia mkazo umuhimu wa wananchi kuishi kwa upendo na
kulinda amani na utulivu, aliwaambia wananchi wa Zanzibar kuwa wasichezee amani
iliyopo iwe kwa kauli zinazohatarisha amani hiyo ama kwa vitendo.
"Tusichezee wala tusidharau amani
tuliyonayo badala yake tuitunze na tuiendeleze, kwani inapotoweka inachukua
muda mrefu na inakuwa vigumu kuirejesha tena hali hiyo," alisema.
Aliwakumbusha wananchi wa Zanzibar kuwa
wao ni watu wamoja hivyo hawana budi kuishi kwa misingi ya udugu, umoja na
masikilizano na kusisitiza kuwa bila ya amani Zanzibar haiwezi kufikia malengo iliyojiwekea
ya kuendeleza ustawi wa nchi na watu wake.
Alifafanua kuwa wageni wakiwemo watalii na
wawekezaji wanaokuja nchini miongoni mwa vivutio vikubwa kwao ni hali ya
utulivu, amani na ukarimu wa watu wa Zanzibar
hivyo vitendo vyovyote vinavyokwenda kinyume na sifa hizo vinaweza kuathiri
uchumi na ustawi wa Zanziba
No comments:
Post a Comment