Na Mwandishi Maalum,
China
Tanzania
inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhusiano na China, ambapo vijana wa Kitanzania
175 wapo katika magereza ya nchini humo, kutokana na makosa ya uhalifu yakiwemo
ya kusafirisha dawa za kulevya.
Kauli hiyo
ilitolewa na Balozi wa Tanzania
nchini China
, Abdulrahman Shimbo, wakati akisoma taarifa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
aliyewasili nchini humo jana kwa ziara ya kikazi.
"Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya
kimahusiano na China ambapo
vijana wa Kitanzania 175 wapo katika magereza ya nchini China kutokana
na makosa ya uhalifu yakiwemo ya kusafirisha dawa za kulevya," alisema na
kuongeza;
"Kati ya
hao, watatu uraia wao ni wa kutiliwa mashaka. Kati yao
48 wako China Bara, Hong Kong wapo 117 na Macao wapo 10. Kati ya hao 175, wanawake ni
34, ambapo 28 wako Hong Kong na sita wako China bara."
Akizungumza na
maofisa ubalozi pamoja na wajumbe wa msafara wake, Waziri Mkuu alisema tatizo
la dawa za kulevya linaharibu sifa ya Tanzania pamoja na mahusiano baina
yake na nchi marafiki.
"Tunahitaji
kufanya kazi ya ziada ili kupambana na wasafirishaji wa dawa za kulevya. Watu
175 ni wengi kwa nchi moja, lakini cha kusikitisha zaidi ni idadi kubwa ya
wanawake waliokamatwa... wizara zinazohusika inabidi tukae na kuweka mkakati wa
pamoja," alisema Pinda.
Kuhusu misaada ya China
kwa Tanzania,
Waziri Mkuu alisema, kuna miradi ya kufa na kupona ambayo itabidi iwekewe uzito
katika ziara yake. Aliainisha miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa reli ya kati,
usambazaji wa umeme na ukuzaji wa utalii baina ya Tanzania na China hasa fursa
ya kuanzisha usafiri wa ndege wa moja kwa moja baina ya China na Tanzania.
Waziri Pinda amewasili Beijing, China
saa 10 jana jioni na kuanza vikao ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi yake ya
siku tisa kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo.
Leo Waziri Mkuu atakuwa na
mazungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Li Keqiang, Rais wa Benki ya Exim ya China, Rais wa Benki ya Maendeleo ya China na
uongozi wa China Railway Jianchang Engineering
No comments:
Post a Comment