- NI KUTOKA 90% hadi 70%, WATU 2,400 WATOA MAONI
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kupunguza Umaskini
nchini (REPOA), umebaini utendaji wa Rais Jakaya Kikwete, umepungua kutoka
asilimia 90 mwaka 2008 hadi asilimia 71 mwaka 2012
.Idadi ya
Watanzania wanaotaka Rais awajibike kwa Bunge la Jamhuri ya Muungani wa Tanzania,
inazidi kuongezeka ambapo mwaka 2012, zaidi ya asilimia 55 walipendekeza
awajibike.
Matokeo ya
utafiti huo yaliyowasilishwa Dar es Salaam jana, yalikusanya maoni ya watu juu
ya utendaji wa Rais, Bunge, Mahakama na kupewa jina la "Afro
Barometer".
Akiwasilisha
matokeo hayo, Mtafiti Msaidizi wa ripoti hiyo, Stephen Mwombela, alisema
utafiti umebaini imani ya Watanzania dhidi ya utendaji wa Rais Kikwete, Baraza
lake la Mawaziri na Bunge la Jamhuri ya Muungano, inazidi kudorora.
Alisema
utafiti huo ulikusanya maoni ya watu 2,400 nchi nzima kipindi cha Mei hadi Juni
2012 ambapo watoa maoni ni watu wenye umri kuanzia miaka 18, wenye elimu
tofauti na wasio na elimu.
"Pamoja
na kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, mhimili wa mahakama, bado
imani yake kwa wananchi ni kubwa na imezidi kuongezeka ukilinganisha na
Serikali, Bunge," alisema.
Aliongeza
kuwa, kwa mujibu wa ripoti hiyo asilimia 84 ya Wazanzibari bado wanaamini
utendaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema watu
wengi waliokosoa utendaji wa Rais ni wenye elimu kuanzia sekondari na kuendelea
ambapo mwaka 2008, utendaji wa Rais uliungwa mkono wakati mwaka 2012, asilimia
60 tu, ndio waliounga mkono.
Ripoti hiyo pia
imeonesha asilimia 70 ya Watanzania waishio mijini, wanaamini Rais anafanya
kazi yake kwa ufasaha sawa na anguko la asilimia 19 ambapo mwaka 2008 ilikuwa
asilimia 89.
Alisema
wananchi waishio vijijini, mambo si mazuri kwani idadi ya wanaopinga utendaji wa
Rais imeongezeka kutoka asilimia 8 mwaka 2008 hadi 26 mwaka 2012.
Upande wa
Bunge, matokeo ya utafiti yanaonesha asilimia 61 ya Watanzania hasa wasio na
elimu bado wanaamini Bunge linafanya kazi yake kwa umakini.
Aliongeza kuwa, hali hiyo inaonesha imani
dhidi ya utendaji wa Bunge, inazidi kushuka ambapo mwaka 2008, asilimia 65 ya
Watanzania waliamini kwamba Bunge linawajibika ipasavyo.
Mtokeo hayo yameonesha kwamba, mwaka 2012
asilimia 61 tu ya Watanzania waishio Bara wana imani na Bunge na Visiwani Zanzibar ni asilimia 64.
Ak i z u n g umz a b a a d a y a kutangazwa
kwa matokeo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa PEROA, Profesa Samwel Wangwe, alisema
matokeo hayo yana ujumbe kwa Serikali ili iweze kuwaelimisha wananchi matarajio
ya kijamii na kiuchumi.
"Watanzania wanatakiwa kuelezwa nini
maana ya utendaji wa Rais na Bunge, naamini haya ni mawazo ya wananchi,"
alisema na kuongeza kuwa, viongozi wanatakiwa kuwajibika katika nafasi zao ili
kurudisha imani kwa wananchi.
Alisema utafiti wao utaendelea kuboreshwa
kila mwaka kwa kufanyika nchi nzima ili kuhakikisha sauti za watu zinasikika;
hivyo lazima kila kiongozi awajibike katika nafasi yake.
Upande wa Mahakama, matokeo yanaonesha
wanaopinga utendaji wake idadi yao
imepungua kutoka asilimia 26 mwaka 2008, hadi 25 mwaka 2012.
Wananchi waishio
vijijini ndio wanaongoza kwa kuwa na imani kubwa na makahama kwa asilimia 77,
waishio mijini ni asilimia 70 tu.
"Ni kawaida kuona kila Serikali mpya huwa
na imani juu ya wananchi wake na muda unavyokwenda, mambo hubadilika,"
alisema Dkt. Jonas Kipokola, ambaye ni mtafiti na mtumishi mstaafu wakati
akitoa maoni yake kuhusu ripoti hiyo.
Aliongeza kuwa; "Kuongezeka au kupungua
kwa imani ya watu kwa Serikali yao,
inategemea ni namna gani Serikali inavyowasiliana na watu wake na kujenga
mtazamo gani.
"Nadhani
tungeyatumia matokeo ya tafiti hizi kuisukuma Serikali ifanye kazi yake vizuri
ili kutimiza matakwa na imani ya wananchi," alisema. Naye Bw. Victor
Kimesera, ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), aliukosoa utafiti huo na kudai kuwa, hauoneshi hali halisi ya mambo.
"Tunajua uelewa wa watu dhidi ya utendaji
wa mihimili ya nchi bado ni mdogo sana...ripoti
haioneshi hali halisi ya mambo," alisema baada ya kuwasilishwa ripoti
hiyo.
Aliongeza kuwa, Watanzana wengi hawajui
wajibu wa mbunge na kuitaka Serikali, ione umuhimu wa kuboresha elimu,
kuhakikisha tafiti kama hizo zinatoa majibu
halisi ya matatizo ya Watanzania.
"Naamini kuanzia mwaka 2005, imani ya
Watanzania juu ya Rais Kikwete ilikuwa kubwa ndiyo maana tafiti zilionesha
imani kubwa juu yake imeanza kushuka," alisema.
Naye
Dkt. Abel Kiyondo, alisema Bunge lipo kwa ajili ya kutetea wananchi lakini kwa
Bunge la Tanzania,
halipo kwa ajili ya wananchi bali linawakilisha vyama vyao
No comments:
Post a Comment