KUMASI, Ghana
Timu ya Ghana (Black Stars) juzi usiku iliiangamiza
Misri, mabao 6-1 katika mechi ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia
mwakani nchini Brazil
na kujitengenezea mazingira mazuri ya kwenda kucheza fainali hizo.
Mshambuliaji Asamoah Gyan alianza kuifungia Ghana bao la kwanza dakika ya tano,huku
mchezaji wa Misri, Wael Gomaa akijifunga
dakika ya 21 akiwa katika
harakati za kuokoa.
Mohamed Aboutrika aliipatia bao pekee la penalti Misri dakika ya 41,
huku Majeed Waris akiifungia Ghana
bao lingine dakika ya 44.
Kipindi cha pili kilianza kwa Ghana
kuliandama lango la Misri ambapo, Gyan akafunga bao la tatu dakika ya 51.Kama
haitoshi, Sulley Muntari aliifungia Ghana bao lingine dakika ya 72 kwa
mkwaju wa penalti.
Christian Atsu
alihitimisha karamu ya mabao baada ya kuifungia Ghana bao la sita na kuifanya timu
hiyo kujijengea mazingira mazuri ya kwenda Brazil.Timu hizo zinatarajiwa
kurudiana nchini Misri,lakini haijajulikana itakapofanyikia kutokana na vurugu
zilizopo Misri.
No comments:
Post a Comment