. David John na Frank Monyo
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC), imemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji mstaafu
Francis Mutungi, kusitisha utoaji wa ruzuku kwa baadhi ya vyama vya siasa kwa
kushindwa kuwasilisha hesabu za ukaguzi wa fedha tangu mwaka 2009.
Agizo hilo lilitolewa Dar es
Salam jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw. Zitto Kabwe, alipokutana na
Msajili huyo ili kufahamu mahesabu ya ruzuku zinazotolewa kwa vyama hivyo.
Bw. Kabwe
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), alisema agizo hilo limeanza jana ili kubaini kama
vyama hivyo havikukaguliwa kwa mujibu wa sheria au la.
Alisema uamuzi
huo umekuja baada ya Jaji Mutungi kushindwa kutoa ripoti ya ukaguzi wa hesabu
baada ya kukutana naye kwa lengo la kutaka kujua matumizi ya Fedha hizo ambazo
zinatokana na kodi za wananchi.
Alivitaja
baadhi ya vyama hivyo kuwa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kinapokea sh.
bilioni 50.9, CHADEMA sh. bilioni 9.2, CUF sh. bilioni 6.2 na NCCR-Mageuzi sh.
milioni 677.
"Hivi ni
baadhi ya vyama ambavyo vimekuwa vikipokea ruzuku, hivyo kamati imemtaka
Msajili kwenda kujipanga upya ili atuletee majibu sahihi ya fedha hizo ili
kuondoa mgongano uliopo kati ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) na Ofisi ya Msajili," alisema Bw. Kabwe.
Alisema
Serikali ilitoa sh. bilioni 67.7 mwaka 2009 ambazo ni ruzuku kwa vyama vya
siasa, lakini tangu mwaka huo hakuna taarifa zozote za mahesabu ya CAG, Ofisi
ya Msajili na vyama husika.
"Hizi ni
fedha za wananchi ambao ndio wanalipa kodi ambao wanapaswa kujua matumizi ya
fedha zao, lazima tupate majibu yaliyokamilika kutoka kwa Msajili,"
alisisitiza Bw. Kabwe.
Kutokana na hali hiyo, kamati ilishindwa
kuendelea na majadiliano ya matumizi ya fedha za ruzuku hadi ukaguzi huo
utakapokamilika ambapo katika kikao hicho, vyama vitatu ndivyo viliitikia wito
wa Msajili kukutana na kamati hiyo
No comments:
Post a Comment