Na Fatuma Rashid
Mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
(VPL), inaanza raundi ya tisa leo kwa timu ya Tanzania Prisons kushuka dimbani
dhidi ya Ashanti United Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya
jiji la Dar es Salaam.
Tanzania
Prisons ya Mbeya inayofunzwa na Kocha Jumanne Charles inashikilia nafasi ya 10
katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi saba huku Ashanti United
ikiwa nafasi ya 13 kwa kuwa na pointi tano.
Katika mechi ya leo, kila timu itatakiwa
kutoka na ushindi ili kujiweka vizuri na kufufua matumaini kwenye msimamo wa
ligi hiyo.
Kikosi cha Prisons, kina wachezaji watatu
majeruhi ambao ni Jumanne Elifadhili aliyeumia juu ya jicho na kushonwa nyuzi
tatu katika mechi dhidi ya Simba, Jimmy Shoji mwenye kadi tatu za njano na
Hamis Maingo aliyeumia bega juzi katika mazoezi.
Shoji alipata kadi za njano katika mechi dhidi
ya Yanga, JKT Ruvu na Simba.Katika mechi iliyochezwa mwishoni mwa wiki, Ashanti
iliifunga Coastal Union mabao 2-1 mechi iliyochezwa Uwanja wa Chamazi, nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Nayo Prisons itaingia uwanjani
ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa bao 1-0 na Simba katika mechi ya ligi
hiyo iliyochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam..
No comments:
Post a Comment