Na David John
WANANCHI
wa Kijiji cha Nganje, Kata ya Magawa Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani
wameilalamikia Ofisi ya Serikali ya Kijiji hicho kwa kushindwa kuitisha mkutano
wa wananchi katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu kwa lengo la kutoa taarifa
ya maendeleo ya kijiji hicho
. Hayo wa l i ya b a i n i s h a mwishoni mwa wiki
katika mk u t a n o wa wa n a n c h i ul iofanyika ki j i j ini hapo ambapo
akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake, Yusufu Ababuu alisema ni muda mrefu
sasa umepita Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji anashindwa kuitisha hata mkutano
mmoja wa wananchi kwa ajili ya kutoa taarifa zozote za maendeleo ya kijiji sasa
ndiyo kwanza baada ya kupita mwaka anaitisha mkutano.
"Kwa muda mrefu wananchi tumekuwa tukihitaji
mkutano wa kijiji ili kuweza kupata taarifa za maendeleo ya kijiji ukizingatia
kuna vyazo vingi vya mapato, lakini huduma za kijamii imekuwa ni tatizo ,jambo
ambalo tunashindwa kulielewa sisi kama
wananchi wa hapa," alisema Ababuu.
Alisema kuwa kijiji hicho kina wafugaji wengi pamoja
na mashamba ukiachi l i a mbali shughuli za uvuvi na Serikali ya kijiji inapata
fedha zinazotokana na vyanzo hivyo lakini wananchi wanakosa t a a r i f a z a
mk a k a t i wa maendeleo ya kijiji hicho.
"Tuna Mwenyekiti wetu hapa wa kijiji lakini cha
kushangaza hatuoni jitihada zake zaidi tunashuhudia kila kitu kikifanywa na
mtendaji amb a y e p i a wa n a n c h i tumepoteza imani naye kwani na yeye
hatuoni kama anatufaa hapa kijiji," alisema Athumani Idd mmoja wa
wanakijiji.
Kat ika hatua nyingine wananchi hao waliiomba
halmashaur i ya Mj i wa Mkuranga kumpa uhamisho mtendaji huyo katika kile
walichodai kupoteza imani naye hasa katika kusimamia mapato ya Serikali ya
kijiji hicho.
Akijibu malalamiko hayo ya wananchi, Mwenyekiti wa
Serikali ya Kijiji hicho, Edward Kaveva al i sema kuwa s i kwe l i kwamb a
katika kipindi hicho chote hakuwahi kuitisha mkutano wa wananchi lakini
kinachotokea anapoitisha mkutano wananchi hawajitokezi.
"Si kweli kwamba mikutano haifanyiki ila
wananchi wangu si watu wa kutaka kujua taarifa za maendeleo ya kijiji chao, na
mikutano inapoitishwa hawahudhurii badala yake wanatoa malalamiko
mitaani," alisema.
Pia
alisema hata malalamiko wanayotoa kuwa mtendaji ana sauti kuliko yeye si kweli
kwani kila kiongozi ana majukumu yake ya kikaz
No comments:
Post a Comment