Na Fatuma Mshamu
SHIRIKA la Hifadhi ya Taifa (NSSF)
linatarajia kukusanya kiasi cha sh. bilioni 706.41 kutoka kwenye michango ya
wanachama wake katika mwaka huu wa fedha.Meneja kiongozi
wa huduma kwa wateja Eunice Chiume alisema kuwa kiasi hicho cha fedha
kinatokana na uandikishaji wa wanachama 169,241 wa mpango wa lazima na
wanachama 85,158 wanaojiunga kwa hiari.
Alisema katika
kipindi h i k i wa a j i r iwa 3 , 0 6 2 wanatarajiwa kuandikishwa na
kuunganishwa na waajiri 19,231 wa sasa na kufanya ongezeko la asilimia 84.07.Chiume alisema,
"Kiasi cha sh. bilioni 199 kitalipwa kwa wanachama watakaoacha kazi au
kustaafu huku kiasi cha sh. bilioni 5.19 kitalipwa kwa ajili ya mafao ya
matibabu kwa wanachama 254,399."
Alisema, katika
mwaka huu wa fedha shirika linatarajia kuwekeza sh. bilioni 951.4 ukilinganisha
na sh.bilioni 751.4 ambazo ziliwekezwa katika mwaka wa fedha 2012/13 sawa na
ongezeko la asilimia 21.06.
Alisema kuwa
shirika linatarajia kukusanya mapato ya sh. bilioni 181.1 kutoka kwenye vitega
uchumi ukilinganisha na mapato ya sh. bilioni 120.1 zilizokusanywa mwaka jana,
pia thamani ya mfuko kwa mwaka jana ilikuwa sh. trilioni 2.1 na inatarajiwa
kuongezeka na kufikia sh. trilioni 2.6 sawa na ongezeko la asilimia 19.23.Aidha aliongeza kuwa katika
mashindano mbalimbali ya michezo iliyofanyika mwaka huu timu ya mpira wa pete
ya Business Times Limited iliibuka na ushindi
No comments:
Post a Comment