Na Eliasa Ally, Iringa
MKUU wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christina
Ishengoma amewataka wazazi mkoani humo kuchangia chakula shule za msingi na za
sekondari za kata hiyo ili wanafunzi waweze kupata mlo wa mchana wakati wakiwa
shuleni badala ya kurudi nyumbani ili kuongeza kiwango cha ufaulu
.Akizungumza
jana ofisini kwake kuhusiana na uchangiaji wa chakula shuleni, Dkt. Ishengoma
alisema kuwa wazazi wa watoto ambao wanasoma katika shule za msingi na
sekondari katika mkoa huo wamekuwa nyuma katika kuchangia chakula shuleni ili
wanafunzi waweze angalau kupata mlo mmoja wa mchana hali ambayo imesababisha
baadhi ya wanafunzi ambao wanashinda njaa kushindwa kuyapokea vema masomo
wanayofundishwa.
"Natoa wito kwa
wananchi wote kuhakikisha kuwa mpango huu unafanyika katika shule zetu zote
mkoani Iringa ili kuongeza kiwango cha ufaulu cha wanafunzi pamoja na
kuimarisha afya zao, ninawaomba viongozi wa vijiji na serikali za mitaa
wahamasishe na kusimamia vizuri ili kuhakikisha kuwa mpango huu unakuwa
endelevu," alisisitiza Dkt. Ishengoma.
Hata hivyo, alizitaja
shule za msingi zilizopo mkoani Iringa ambazo wanafunzi wake wanapata chakula
na wasiopata chakula kuwa katika Manispaa ya Iringa Mjini jumla ya shule 49
zilizopo, zinazopata chakula zipo 21, Iringa Vijijini shule zipo 145 zinazopata
chakula zipo 129
Pia wilaya ya Kilolo
zipo shule 111 zinazopata chakula zipo 98 na Mufindi kuna shule za msingi 176
ambapo zinazopata chakula zipo 72 na kufanya jumla ya shule za msingi 320
mkoani Iringa kupata chakula cha mchana ambapo 481 wanafunzi wake hawapati
chakula cha mchana.
Akizungumzia shule za
sekondari katika Mkoa wa Iringa, Dkt. Ishengoma alizitaja zinapata chakula
katika Manispaa ya Iringa zinazopata chakula zipo 11 kati ya sekondari 26,
Iringa Vijijini zipo sekondari 32 zinazotoa chakula zipo 21, wilaya ya Kilolo
kuna sekondari 38 zinazotoa chakula zipo zipo 19 ambapo Mufindi kuna sekondari
55 zinazotoa chakula zipo 36; na hivyo kufanya jula ya sekondari 87 zinazotoa
chakula kati ya sekondari 151 zilizopo.
Aidha, Mkuu wa mkoa
alizitaja changamoto nyingine ambazo zinaukabili Mkoa wa Iringa kuwa ni pamoja
na kutokuwepo kwa maji safi kwa matumizi ya wanafunzi katika maeneo ya shule,
uelewa mdogo wa jamii kuhusu umuhimu wa mpango wa chakula shuleni.
Nyingine ni ushiriki mdogo wa wananchi katika
kuchangia chakula, ukosefu wa wafadhili, mabweni, miundombinu katika shule
husika yakiwemo mabwalo ya chakula pamoja na vifaa vya kuchukulia chakula na
kuhifadhia
No comments:
Post a Comment