CHAMA cha
Wananchi (CUF), kimedai kusikitishwa na kauli ya Spika wa Bunge, Bi. Anne
Makinda anayodaiwa kuitoa hivi karibuni, Mjini Bagamoyo, mkoani Pwani ili
kushinikiza wananchi kulipa tozo ya laini za simu sh. 1,000 kila mwezi, anaripoti
Mwandishi Wetu
.Naibu Mkurugenzi Habari, Uenezi na Haki
za Binadamu wa CUF, Bw. Abdul Kambaya, aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika taarifa yake kwa
vyombo vya habari.Alisema Bi. Makinda aliyasema hayo
baada ya ufunguzi wa mafunzo ya wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu
(PAC), Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Bajeti.
Aliongeza kuwa, katika ufunguzi huo Bi.
Makinda alisema: “Haya maendeleo tunayotaka sisi kama Watanzania yatapatikana
kwa kulipa kodi, hata vitabu vitakatifu vinasema kila mtu lazima achangie.”
Kutokana na kauli hiyo, Bw. Kambaya
alisema chama hicho kinaamini kila vocha ya simu anayonunua mwananchi kuna
asilimia zinazoingia katika mfuko wa Serikali.
“CUF tulitarajia kabla ya
kufikiria jinsi ya kuendelea kumbebesha mzigo mwingine mwananchi, yeye kama
msimamizi mkuu wa Bunge, wangeweka mikakati na mipango inayotekelezeka ya
kumuinua mwananchi kiuchumi.
No comments:
Post a Comment