Na Grace Ndossa
WAZIRI wa Kilimo Chakula na Ushirika Christopher Ch i z a a n
awa s i l i s h a mswada wa sheria ya vyama vya ushirika Bungeni kesho kwa
ajili ya kusomwa kwa mara ya pili.Akizungumza hivi
karibuni alisema kuwa mswada huo utasaidia kurekebisha sheria ya vyama vya
ushirika pamoja na kuundwa kwa Tume ya kusimamia vyama hivyo ili viweze kufanya
kazi kwa ufanisi.
Alisema kuwa
mswada wa sheria hiyo mpya ya mwaka 2013 azma yake ni kufufua vyama vya
ushirika pamoja na kuweka mazingira stahiki kwa wanachama na kuwepo kwa uongozi
ambao unawajibika kwa wanachama.
"Kutungwa kwa sheria mpya ya mwaka
2013 ambao mswada huo utasomwa kwa mara ya pili katika kikao cha 11 cha bunge
azma yake kubwa ni kufufua vyama vya ushirika pamoja na kuwepo kwa uongozi
imara ambao wanachama watakuwa na imani nao," alisema Chiza.
Alisema kuwa sheria ya vyama vya
ushirika iliyopo kwa sasa haikidhi viwango na imepelekea vyama vingi vya
ushirika kufa na wanachama wamekosa imani navyo kutokana na ubadhirifu mkubwa
kwenye vyama hivyo.
Al i o n g e z a k uwa s h e r i a
inayotumika ni ya mwaka 2003 kutokana na mabadiliko ya kiuchumi kuna vipengele
ambavyo vimepitwa na wakati, hivyo sheria hii mpya ya mwaka 2013 itasaidia
kuondoa upungufu uliokuwepo.
Pia alisema kutakuwepo kwa tume
itakayojitegemea na itapata ruzuku kutoka serikalini kwa ajili ya kuhakikisha
vyama vya ushirika vinafanya kazi ipasavyo na kuondoa malalamiko yaliyokuwepo
kwa wanachama.
Hata hivyo alisema sheria iliyopo
haitoi adhabu ya kutosha kwa wanaohusika na ubadhirifu wa fedha ndiyo maana
walipitia vipengele hivyo na kuvifanyia marekebisho ili iweze kutumika.
Alisema kuwa katika sheria hiyo pia
walipendekeza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick
Utouh kukagua mahesabu ya vyama vya ushirika ili kudhibiti ubadhirifu huo kwa
vyama vya ushirika.
No comments:
Post a Comment