27 August 2013

RUFAA DHIDI YA ZOMBE AGOSTI 29



Na Rachel Balama
MA O M B I y a M k u r u g e n z i w a Ma s h t a k a Nchini (DPP) ya kuongezewa muda wa kukata rufaa dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaama, Abdallah Zombe na askari wenzake wanane walioachiwa huru katika shtaka la mauaji yanatarajiwa kusikilizwa Agosti 29, mwaka huu
.Maombi hayo yatasikilizwa katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam mbele ya Jaji Aloyisius Mujuluzi.Katika shauri hilo DPP aliwasilisha maombi ya kuomba kuongezewa muda wa kukata rufaa, baada ya mahakama ya Rufaa ya Tanzania kutupilia mbali rufaa ya awali kwa sababu ilikuwa na makosa ya kisheria.
Rufaa hiyo ilitupwa baada ya kubaini kuwapo kwa dosari katika hati ya kusudio la kukata rufaa na mahakama kukataa kuamuru makosa yaliyojitokeza yafanyiwe marekebisho.Katika shauri hilo mbali na Zombe, wajibu rufaa wengine ambao pia ni polisi ni, Christopher Bageni, Ahmed Makele, Jane Andrew, Koplo Emmanuel Mabula, Michael Shonza, Abeneth Saro, Rajabu Bakari na Festus Gwasab.Serikali ilikata rufaa hiyo kupinga hukumu iliyotolewa Agosti 17, mwaka 2008 na Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment