Na Theonestina Juma, Kagera
ZAIDI ya
wazee 300 huuawa hapa nchini kila mwaka kutokana na umaskini na uchu wa kutaka
mali na si kwa madai ya ushirikina kama inavyodaiwa katika jamii. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mratibu wa chama cha
Saidiawazee wilayani Karagwe (SAWAKA), Livingstone Byekwaso katika warsha ya
siku moja iliyoendeshwa na chama hicho kwa waandishi wa habari mkoani Kagera
kuwajengea uelewa juu ya ufuatiliaji wa matatizo yanayowakabili wazee.
Alisema, "kila mwaka wazee zaidi ya 300 wanauawa
hapa nchini kwa tuhuma za uchawi si kweli, tatizo kubwa ni kunyang'anywa mali
zao; na hii inatokana na umaskini uliopo kwa baadhi ya vijana na ukosefu wa
ajira," alisema.
Alisema wazee hao zaidi ya 300 wamekuwa wakiuawa hasa Kanda ya
Ziwa, katika Mikoa ya Kagera, Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza na Tabora. Pia
wazee hao wamekuwa wakinyanyaswa zaidi katika Mkoa wa Kagera ambapo wazee
wamekuwa wakifyekewa mashamba yao.
Alisema wazee wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo
maagizo yanayotolewa na Serikali hayapewi uzito wowote kama ya kutibiwa bure
katika hospitali za umma.
Alisema wazee wamekuwa wakitwikwa mzigo wa kulea watoto yatima
ambao wazazi wao hufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Alisema asilimia 54 sawa na watoto yatima milioni mbili wamekuwa
wakihudumiwa na wazee baada ya wazazi wao kufariki kwa ugonjwa wa Ukimwi.
Halikadhalika alisema, asilimia nne ya wazee hapa nchini ndiyo
wako katika mfumo wa pensheni na asilimi 96 wanaobaki hawamo katika mfumo huo
jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa kuishi katika mazingira magumu
ikiwemo namna ya kupata mahitaji yao ya kila siku kama chakula, malazi na
mavazi.
Naye Makamu Mwenyekiti wa umoja wa Shirika la Tanzania Social Protect
Network, Ramadhani Msoka katika ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu mwaka
2011
No comments:
Post a Comment