27 August 2013

POLISI YANASA MAJAMBAZI 4 ARUSHA



Omari Moyo na Queen Lema,Arusha
JESHI la Polisi mkoani Arusha, imewakamata watu wane wanaodaiwa kuhusika na tukio la ujambazi kwa mfanyabiashara wa madini ya tanzanite hivi karibuni, wakiwa na bastola mbili zinazodaiwa kutumika katika
tukio hilo.

 Tukio hilo lilitokea Agosti 23 mwaka huu, katika Mtaa wa Pangani, mjini humo ambapo mfanyabiashara Bw. Aber Musa (35), aliporwa sh. milioni tano, madini yenye thamani ya sh. milioni 60 na kujeruhiwa kwa risasi.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Liberatus Sabas, alisema baada ya tukio hilo, walifanya msako usiku na mchana. "Tumefanikiwa kuwanasa watuhumiwa wakiwa na silaha mbili ambao ni Shangai William Semboi (38) mkazi wa Sokon 1, mjini hapa na Ally Hussein 'Dogoo' au Sadock (28) mkazi wa Tabata, Dar es Salaam. "Wengine ni Eugen Donas Mushi 'Mbuna' (28) mkazi wa Makao Mapya na Josephat Jerome Shirima (29), mkazi wa Sombetini, wote wanaishi jijini Arusha," alisema.
Aliongeza kuwa, watuhumiwa walikutwa na bastola aina ya Browning model 83 cal 9, yenye namba 4738 ikiwa na risasi 10 na nyingine aina ya LAMI ikiwa na risasi 12, wakiwa na gari aina ya Toyota Vitz, namba T 368 AUH. Pia walikutwa na pikipiki wanazodaiwa kufania uhalifu zenye namba T 352 CBW na T464 APH aina ya Honda. 
 Kamanda Sabas, alisema watuhumiwa wote wanahusishwa na matukio mbalimbali ya uhalifu yaliyotokea jijini humo ambapo taratibu zinafanyika ili waweze kufi kishwa mahakamani. Aliwaomba wananchi watoe ushirikiano wanapobaini dalili za vitendo vya uhalifu au mipango ya kuwepo vitendo hivyo ili wahusika waweze kudhibitiwa kabla ya kutenda uhalifu

No comments:

Post a Comment