Na Penina Malundo
RAIS wa Jakaya Kikwete, jana amemwapisha
Msajili Mpya wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji mstaafu Francis Mutungi baada ya aliyekuwa
akishikilia nafasi hiyo, Bw. John Tendwa kustaafu. Ak i z u n g umz a b a a d a
y a kuapishwa Ikulu, Dar es Salaam, Jaji Mutungi alisema ingawa kazi
hiyo inachangamoto kubwa,
amejipanga kikamilifu kuifanya kwa uadilifu.
Alisema
katika utendaji kazi wake, anatarajia kutenda haki na usawa bila ubaguzi
wowote. "Mimi bado mgeni katika ofi si hii, sina maneno mengi ila kazi hii
ni nzito, nahitaji ushirikiano wa kila Mtanzania," alisema Jaji Mutungi.
Aliongeza
kuwa, baada ya miezi mitatu atazungumza na wananchi kuhusu mikakati yake katika
ofi si hiyo. Kwa upande wake, Bw. Tendwa alisema kazi kubwa iliyopo katika Ofi si ya Msajili ni kukuza demokrasia.
"Kipindi cha uongozi wangu katika Ofi si ya Msajili nimekabiliana na
changamoto nyingi, vyama vya siasa vilikuwa na migongano mingi kwa viongozi
wake lakini nilihakikisha vimesimama. "Kustaafu
kwangu si mwisho wa maisha yangu bali ni njia moja wapo ya kunifanya niendelee
na kazi zangu katika taasisi nyingine za kijamii," alisema
No comments:
Post a Comment