27 August 2013

MTANDAO UNAOFADHILI UJAMBAZI HADHARANI



Anneth Kagenda na Salma Mzee
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, wiki ijayo litaweka hadharani majina ya mtandao unaofadhili matukio ya ujambazi na kuendeleza uhalifu nchini. Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema watu hao ambao wengi wao wana vitambi, wamekuwa wakiharibu sifa ya nchi kwa kufadhili uhalifu jambo ambalo haliwezi kukubalika, hivyo wamejipanga kuhakikisha mtandao huo unakamatwa na kushtakiwa.Akizungumzia suala la Bw. Aquiline Maiko Masubo (42), ambaye anashikiliwa na jeshi hilo akijifanya Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa, Kamishna Kova alisema wanaendelea kukusanya taarifa mbalimbali za watu waliotapeliwa. 
"Inaonesha huyu mtuhumiwa alijihusisha na utapeli sehemu mbalimbali na kuwagusa watu wengi...baada ya upelelezi wa matukio yote aliyofanya kukamilika,jalada lake lilipelekwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali " alisema.. Kamishna Kova aliongeza kuwa hivi karibuni kumeibuka uhalifu wa kitapeli kwa njia za mtandao ya simu, kijamii na kibenki ambapo katika hatua ya kwanza,jeshi hilo limeanza kuwasaka matapeli katika  vyombo vya Ulinzi na Usalama.Alisema uchunguzi wa kina unaendelea ili kuwabaini watu wanaofanya utapeli kwa kujifanya ni watumishi wa Serikali,Mashirika ya Umma na taasisi mbalimbali. 
 Uchomaji KKKT 
 Akizungumzia tukio la kuchoma moto Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea, alisema jeshi hilo kwa
kushirikiana na wataalam wa ugaidi kutoka Makao Makuu ya Polisi, wanafanya upelelezi wa tukio hilo ambalo limetokea Agosti 24 mwaka huu. Alisema katika tukio hilo, waumini 20 wakiwa wanaendelea na ibada, ghafl a walitokea watu wane wasiofahamika, kuingia kanisani na kutupa bomu moja lililotengenezwa kienyeji kwa kutumia chupa ya bia aina ya Castle ikiwa na utambi, mafuta yanayodhaniwa ya taa madhabahuni. 
Kamishna Kova alisema, hasara iliyopatikana ni kuungua kwa Bwiablliicah momojaa ,m zuoltioa gaamrib alepnoy we antaum hbaoa T 482 BAF, aina ya Toyota Crester aKmanbiaslao hniil om. ali ya Mchungaji wa hil oK laimtikeaam huaat ukau tunmyiinag tienken, ojleosjhiai ywaa kkiustausma iial is iklauhdah iubnitaio ufahnayliwfua kmwaean weoa fmanbyaalbimiabsahlai ran cwhiannia hoatosaa fkeudshaab azbaios hbae nuksia, lakmuzai swafia rois hkau wnaa mdogo. 
"Usafirishaji huu umeleta madhara makubwa, katika jitihada za kukomesha uhalifu huu, tumekubaliana na baadhi ya kampuni za simu nchini zinazojihusisha na utumaji, uhamishaji fedha kwa njia ya elektroniki, wawajibike kutuma fedha kwa wafanyabiashara, kwa kuanzia elimu hii itatolewa na Kampuni ya Vodacom. Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara wa Vodacom, 
Bw. Jackson Swaga, alisema hivi sasa wafanyabiashara hawana sababu ya kubeba fedha nyingi kupeleka benki bali watumie mfumo mpya wa kampuni hiyo ili mfanyakazi aweze kutumiwa mshshara wake ili kuziba mianya ya uhalifu unaoendelea.

1 comment:

  1. Hivi gazeti la zamani kama hili halina mhariri?Tutapataje habari wapendwa au ndio wamewaambia mfiche siri kwa kitu kidogo?

    ReplyDelete