01 August 2012
Mabadiliko ya matumizi ya ardhi wananchi washirikishwe
Na Rose Itono
TANZANIA ni moja kati ya nchi zinazoongoza kwa kuwa na migogoro ya mara kwa mara ya ardhi yanayosababishwa na sababu mbalimbali.
Huu ni ukweli usiofichika kwani ni mara nyingi tumekuwa tukisikia fujo na ghasia kutoka maeneo mbalimbali nchini kutokana na ardhi.
Hali hii ni dhahiri inaonyesha dhahiri kuwa tatizo la ardhi ni kubwa na hivyo busara inatakiwa kufanyika ili kuweza kumaliza matatizo hayo ambayo sasa hivi yameota mizizi.
Hivi karibuni tumesikia zaidi ya wanakijiji 63 wa kitongoji cha Uvinje, Saadan wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakipinga vikali hatua ya ulipwaji wa fidia na uhamishwaji kwenye makazi yao kwa ajili ya kupisha upanuzi wa mipaka ya Hifadhi ya Saadan.
Wanakijiji hao kutokana na mgogoro huo walimtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kuingilia kati ili kuweza kupatiwa haki yao.
Wakazi hao wamemuomba rais kutumia hekima na busara kuhakikisha mgogoro mkubwa unaoendelea katika kitongoji hicho tangu mwaka 2000 kupatiwa ufumbuzi.
Mgogoro mkubwa katika kitongoji hicho ni kutokana na kutokubaliana na oparesheni ya kuhamishwa kwenye makazi yao kwa ajili ya kupisha upanuzi wa mipaka ya Hifadhi ya Saadani.
Nionavyo ipo haja kwa serikali kuwashirikisha wadau ambao ni wananachi kila wanapotaka kufanya jambo ambalo ni la maendeleo.
Kutokana na tabia ya kutowashirikisha wananachi katika mambo mbalimbali ya maendeleoi hali ya kutokubaliana kama wakazi wa kitongoji hiki yamekuwa yakisababisha migogoro ya mara kwa mara.
Kama inavyofahamika wakazi wa kitongoji hiki wamedumu kwa miaka mingi tangu enzi za mababu zao hivyo sualka la kutaka kuwahamisha pasipo kuwaelimisha ni kuanzisha mgogoro ambao hauna sababu.
Nionavyo kwa upande wangu migogoro mingi ya ardhi hutokana na kutoridhishwa na kiasi cha fedha wanachotakiwa kulipwa kama fidia ya makazi yao.
Hii inatokana na kutoridhika na kiasi cha fedha ambazo Serikali huwa imeandaa kuwalipa wananchi hao kulingana na hali halisi ya maisha ya sasa.
Nionavyo pia ipo haja ya kuziangalia upya sheria ambazo zimepitwa na wakati na hata ikiwezekana ni lazima busara ifanyike kwa kuangalia hali halisi ya maisha wakati wa kuwalipa fidia wananachi pale wanapotakiwa kuhamishwa ili ziendane na wakati.
Kutokana na hili rais ana kila sababu ya kuingilia ili kuleta suluhu kwa wakazi hao ambao tangu mwaka huko nyuma ambapo ulikuwa mbunge wao.
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Bw. Hossen Abdalah anasema Julai 25, mwaka huu waliitisha kikao kati yao na diwani wa kata ya Mkange kueleza kuwa kilio chao kikubwa ni mipaka.
Mwaka 2005 kuna mwanakijiji mwenzao alifariki baada ya kutokea vurugu na viongozi wa shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Nionavyo kulinyamazia tatizo hili ni kuchochea vurugu ambazo zinaweza kusababisha watu kumwaga damu na kuishia kuunda tume ambazo nyingi majibu yake huwa ni hakuna.
Ili hali kama hiyo isitokee hakuna budi viongozi ngazi za juu kuingilia kati ili kuweza kusaidia kutatua mgogoro kati ya wakazi hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment