01 August 2012
Mtui kuiwakilisha nchi mashindano ya scania
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Scania Tanzania, jana ilimuaga Erasmus Mtui ambaye ni mshindi wa mashindano ya madereva yanayojulikana kama 'Tanzania Driver Of The Year' yaliyofanyika katika viwanja vya Biafra, Dar es Salaam Novemba 19 mwakajana.
Baada ya kuibuka mshindi katika mashindano hayo, Mtui (44) alijiriwa kuwa dereva katikakampuni ya usafirishaji ya Super Star Forwarders ya Dar Es Salaam.
Mtui anakwenda nchini Afrika Kusini katika mashindano ya Bingwa wa Mabingwa yatakayofanyika kuanzia Agosti 9 hadi 11 mwaka huu mjini Sun City.
Akizungumza Dar es Salaam jana katika hafla fupi ya kumuaga, Mtui alisema amejiandaa vya kutosha kukabiliana na mashindano hayo na hatimaye kurudi na ushindi.
Naye Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Scania, Mark Cameron alisema kwamba‘ Dereva ndio kiungo muhimu katika uchumi, mazingira na usalama.
"Madereva wenye utaalamu na wana openda kazi yao husaidia kuendesha kwa usalama barabarani, hutumia mafuta kidogo, hii husaidia kiwango kidogo cha uchafuzi wa mazingira hivyo ni watu muhimu na ndiyo maana tuliamua kuwashindanisha,” alisema.
Alisema Scania ilianzisha mashindano ya madereva kwamara ya kwanza mwaka 2003 katika nchi za ulaya.
Meneja huyo alisema wanamtakia kheri Mtui aende akafanye vyema katika mashindano ya Afrika Kusini na wanaimani atarudi na ushindi kwa kuwa wanamuamini na amejiandaa vyema.
Kwa upande wa Ofisa Masoko Msaidizi wa kampuni hiyo,Margaret Legga alisema mashindano hayo ya Afrika Kusini yatashirikisha nchi kutoka Marekani ya Kusini, Ulaya, ASIA na Afrika.
Kutoka Afrika nchi za Tanzania, Botswana, Lesotho, Malawi, Namibia na wenyeji Afrika Kusini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment