01 August 2012
EBSS kuwashamoto Coco Beach leo
Na MwandishiWetu
MASHINDANO ya kusaka vipaji kwa washiriki wa Bongo Star Search (EBSS) kwa Mkoa wa Dar es Salaam yanaanza leo Coco Beach.
Tofauti na mikoa mingine ambapo usaili ulichukua siku mbili, huu Dar es Salaam utachukua siku tatu ambapo mpaka sasa vijana walio wengi wameonesha nia ya kushiriki katika usaili huo.
Akizungumzia usaili wa Dar es Salaam jana Jaji Mkuu wa EBSS 2012, Ritha Paulsen alisema kutokana na historia ya mkoa huu katika usaili wake kuhudhuriwa na watu wengi zaidi, hivyo anategemea ushindani kuwa mkubwa zaidi.
Kwa sasa EBSS imeshamaliza kusaka vipaji mikoani huku Mkoa wa Tanga ukiwa wa mwisho katika ziara yake ya mikoa nane na tayari saba imemalizika.
Ritha alisema mapema mwezi ujao washiriki wataanza kuingia kambini kwa ajili ya mashindano hayo na kuongeza kuwa EBSS kwa mwaka huu itakuwa ni bora zaidi.
“Nashukuru Mungu kuwa tumemaliza salama mikoani na kwa sasa ndiyo tunaingia rasmi Dar es Salaam kwa ajili ya kufunga kabisa pazia la ushiriki wa EBSS,” alisema Ritha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment