26 July 2012

JK atuma zsalamu za pongezi India


Na Willbroad Mathias

RAIS wa Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za pongezi Rais wa India, Bw. Prunab Murkjee, kwa kuchaguliwa kuwa kiongozi wa 13 wa Taifa hilo.

Taarifa iliyotolewa kwenye vyombo habari Dar es Salaam jana, ilisema Rais Kikwete amempongeza kwa dhati Bw. Murkjee baada ya kuibuka mshindi katika Uchaguzi Mkuu nchini humo.

Kupitia salamu hizo, Rais Kikwete alisema ushindi wake umekuja kwa wakati muafaka kwani Serikali ya Tanzania na India zinashirikiana katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.

“Nakutakia mafanikio mema kwenye majukumu yako kama kiongozi wa nchi, natarajia tutafanya kazi kwa pamoja ili kudumisha uhusiano uliopo kati yetu,” alisema.

Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kukumbushia malengo na ndoto za Serikali ya Tanzania kufanya kazi kwa ushirikiano na India.

“Ni matumani yangu wakati wa utawala wako, tutafungua ukurasa mpya wa ushirikiano kwa ajili ya masilahi ya wananchi wetu,” alisema Rais Kikwete.


No comments:

Post a Comment