26 July 2012
Waislamu kuweni wanyenyekevu'
Na David John
MKURUGENZI wa Kituo cha Utamaduni cha Irani, Bw. Morteza Sabouri, amewataka waumini wa Kiislamu kujenga tabia ya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu kila wakati badala ya kusubiri mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Bw. Sabouri alisema Waislamu wanatakiwa kumuomba Mungu kila siku badala ya kujenga tabia kuchagua muda wa kufanya ibada.
“Mungu anawataka Waislamu watende mema kila siku hivyo lazima tuwe watu wa aina hii badala ya kusubiri katika Mfungo wa Ramadhani, sio maagizi ya Mwenyezi Mungu,” alisema.
Katika hatua nyingine, Bw. Sabouriametoa pole kwa Waislamu wote na Watanzania ambao ndugu zao wamefariki dunia katika ajaali ya meli ya Mv Skagit iliyozama hivi karibuni.
“Vifo hivi ni pigo kubwa kwa Taifa hasa ukizingatia kuwa, mwaka mmoja umepita tangu kutokea ajali nyingine kama hii na kupoteza maisha ya Watanzania wengi hivyo tunapaswa kuwa karibu zaidi na Mwenyezi Mungu,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment