Na Mwali Ibrahim
WABUNGE wanawake wamesisitiza kuendelea kuisaidia timu ya soka ya wanawake 'Twiga Stars' ili kuhakikisha inafika mbali.
Akizungumza Dar es Salaam jana, katika maadhimisho ya siku ya Wanawake kwa wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya Business Times Limited inayochapisha magazeti ya Majira, Spoti Starehe na Business Times, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee alisema wameamua kufanya hivyo ili kuhakikisha wanawake wanajiwezesha wenyewe.
Alisema, awali walijikusanya ili kujadili namna ya kuisaidia timu hiyo baada ya kuona inahitaji msaada mkubwa ,hivyo wameona wanahaki ya kuisaidia kwa hali na mali ili ifike mbali
"Napenda kusisitiza kuwa sisi kama wabunge wanawake tumedhamiria kwa nia moja kuweza kuisaidia timu hii ili kuhakikisha tunawawezesha wanawake wenzetu kupiga hatua nzuri zaidi ya kimichezo kwani tunaamini wanaweza," alisema Halima.
Sambamba na hao wapo baadhi ya wabunge ambao nao wamejitolea kwa hali na mali kuhakikisha wanaisaidia timu ya taifa ya Netiboli 'Taifa Queens' ili kuhakikisha nayo inashiriki vyema katika mashindano ya Afrika yanayotarajia kufanyika mwezi Mei mwaka huu, katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment