Na Elizabeth Mayemba
MABINGWA wa Bara Yanga wameanza kuivutia kasi Azam FC, kwa ajili ya mchezo wao wa Jumamosi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, utakaochezwa Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kostadin Papic alisema timu yake iliingia jana kambini katika Makao Makuu wa klabu hiyo Makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, ambapo mazoezi wanafanyia Uwanja wa Shule ya kimataifa ya Tanganyika Upanga,Dar es Salaam.
"Azam ni timu nzuri hivyo tunatakiwa kujiandaa kikamilifu, naimani tutashinda mchezo huo kwa kuwa kikosi changu kimetokea kwenye mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika,"alisema Papic.
Alisema ligi ilipofikia ni ngumu hasa kwa wapinzani wao Azam ambao wanataka kushika nafasi za juu, hivyo watakuwa na kazi ya ziada siku hiyo,
Papic alisema katika kikosi chake anakabiliwa na majeruhi Salum Telela na Yaw Berko, lakini wengine wanafanya mazoezi kama kawaida na jana alitarajiwa kuangalia afya za wengine katika mazoezi ya jioni.
Alisema anaimani kabisa wachezaji wake watakuwa na ari kubwa ya ushindi ili kuhakikisha wanazoa pointi zote tatu katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment