08 March 2012

Waandamana kupinga JWTZ kuwanyang'anya ardhi

Na Jane Edward,
Arusha
WANANCHI kutoka kata tatu za,Mlangalini,Moshono na
Nduruma, Wilayani Arumeru,Mkoani Arusha wameandamana hadi Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Arusha,wakipinga kitendo cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) Kikosi cha 977 KJ kuwanyangánya Ardhi yao.


Wananchi hao walikuwa wameambatana na watoto wadogo jana wakiwa na sare za shule huku wakiwa wameshikilia matawi ya miti mikononi pamoja na mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kulaani kitendo cha JWTZ kuwazuia kufanya shughuli za maendeleo katika eneo lao kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu.

Wakazi hao ambao walinza safari hiyo kutoka Mushono na kukumbwa na
vikwazo vya polisi ambao walikuwa wakiwazuia wasiendelee na maandamano
hayo, lakini ilishindikana na hatimaye  waliamua kutumia busara na kuwaachia njia ili waweze kufika kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Bw. Magesa Mulongo kufikisha malalamiko yao.

Wakazi hao walisema katika kipindi cha miaka mitatu tangu mwaka 2010 JWTZ imewazuia kufanya shughuli zozote za maendeleo ikiwemo kukarabati hata nyumba zao pindi zinapopata nyufa , kulima na ujenzi wa makazi yao.

Mmoja wa wananchi hao,Bw. Emanuel Masamaki alidai ya kuwa serikali
imeshindwa kuutatua mgogoro huo baina yao na JWTZ katika kipindi hicho
hali inayowafanya waishi kama wakimbizi ndani ya nchi yao .

Alisema mgogoro huo walishafikisha kwenye ngazi husika za serikali
hakuna hatua yoyote ambayo imekuwa ikifuata badala yake wananchi hao
wamezidi kunyanyasika katika nchi yao na kutelekezwa kama vile hawana
viongozi kabisa.

Aliongeza kuwa, wanashikitishawa pia na kitendo cha serikali kukalia taarifa ya tume iliyoundwa kwa ajili ya kushughulikia mgogoro huo kwani waliamini kwamba mara baada ya tume kuchunguza na kutoa mapendekezo serikali ingetoa maamuzi haraka juu ya mgogoro huo.

Naye Bw. Zebedayo Laizer alisema kuwa, katika kipindi chote cha mgogoro baina yoa na JWTZ amekuwa akifuatilia ngazi zote ikiwemo ofisi za mkuu wa mkoa ili kupata majibu sahihi kutokana na malalamiko yao, lakini wamekuwa wakipata majibu ambayo yanaonekana ni ya kisiasa zaidi na kushindwa kuwaridhisha wananchi wao.

Pamoja na hayo wamemtuhumu Mbunge wao , Bw. Goodluck Ole Medeye kuwa ni
msaliti kwani katika kipindi cha nyuma aliwaahidi kushughulikia mgogoro
wao haraka na pindi anapoondoka jimboni humo amekuwa akikaa kimya na kuonekana akiunga mkono jitihada za jeshi hilo kuchukua ardhi yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mulongo aliwasihi watulie na waache vurugu kwani serikali ni tulivu na hadi kufikia Machi 20 mwaka huu , serikali itatoa tamko juu ya kumaliza mgogoro huo baada ya Kamati iliyoundwa na wananchi hao, Mkuu wa mkoa, JWTZ pamoja na Wizara ya Ardhi kujadiliana na kutoa tamko rasmi juu ya hatua gani
zichukuliwe ili kumaliza mgogoro huo.

Alisisitiza kuwa mgogoro huo ulishafika hadi kwa Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda hivyo Machi 20 mwaka huu watatoa jibu sahihi juu ya kumaliza mgogoro huo kati ya JWTZ na wananchi hao.

1 comment:

  1. SUALA LA JWTZ KUJICHUKULIA ARDHI MAENEO MBALIMBALI NCHINI LINAONYESHA WAZI NI LA KIUJANJA UJANJA. HATUKATAI JESHI KUCHUKUA MAENEO KWA AJILI YA MIPANGO YAKE. KWA NINI JESHI LICHUKUE ARDHI ILIYO KARIBU NA MIJI AU MAENEO YA WAKULIMA?

    KUNA MAPORI MENGI MBALI NA WANANCHI YENYE RUTUBA KAMA NI YA JKT NA YA KUFANYIA MAZOEZI.

    JANJA YAO NI KUCHUKUA ARDHI HIYO NA KUJA KUIUZA KWA BEI YA JUU. WACHUKUE ARDHI KAMA NI YA SERIKALI LAKINI SIO YA KUJA KUDALALIA.

    MAMA TIBAIJUKA AINGILIE KATI HUU UJANJA. NADHANI SERIKALI HAIUZI ARDHI YAKE AU KUKATA VIWANJA.

    KUNA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WLIO NYUMA YAO KAMA SUALA LA MEREMETA

    WANANCHI MSIKUBALI MAMBO HAYA. KAZENI BUTI KUTETEA HAKI ZENU.

    ReplyDelete