08 March 2012

TAZARA wamtaka Waziri wa Uchukuzi ajiuzulu

  • Walimu nao waipa serikari siku 14
Tumaini Maduhu na Boniventure Vitus
WAFANYAKAZI wa Shirikala la reli Tanzania(TAZARA) wamemtaka Waziri wa Uchukuzi Bw, Omari Nundu ajiuzulu kutokana na kushindwa kusimamia madai  yao ya  mwezi januari na februari.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wenzake mmoja wa Wanyakazi wa Shirika hilo ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema kuwa,takwimu zinaonyesha shirika hilo linaingiza zaidi bilioni tatu kwa mwezi.

Alisema kutokana na kutokuwa na usimamizi mzuri wa pesa hizo kumepelekea wafanyakazi wa shirika hilo kutolipwa madai yao kwa muda muafaka.

Aliongeza kuwa Viongozi hao wakijiuzulu kuatasidia kwa kiasi kikubwa Shirika hilo kuafanya kazi kwa uafanisi pamoja na kuondoa migogoro inayojitokeza katika shirika hilo.

``Takwimu zinaonyesha shirika linaingiza biloni tatu kwa mwezi,na sisi tunadai bilioni 1.1 za mshahara  kwa wafanyakazi  kwa nini tusilipwe pesa zetu kwa wa wakati muafaka kwasababu wengine tunategemewa na familia zetu ili kuendesha maisha yetu``alisema na kuongeza.

Hata hivyo aliongeza kuwa Viongozi wa Serikali wamekuwa na tabia za kupeleka taarifa za uwongo Wizarani kwakusema Shirika hilo halina matatizo yoyote.

``Kumemekuwa,, na tabia ya baadhi ya Viongozi kusema uwongo kwenye Shirika letu hakuna matatizo yoyote,lakini ukinaglia kwa namna au nyingine ndani ya shirika letu kuna matatizo mengi.

Alisema kuwa, hatua ya mwisho waliyoifikia ni Waziri wa Uchukuzi Bw Omari Nundu ajiuzulu kutokana na kushindwa kusimamia madai yao.

Katika hatua nyingine alisema kuwa wamekuwa wakikatwa asilimia kumi ya mishahara yao kwenda NSSF lakini chakushangaza makato hayo hayafiki NSSF.

hata hivyo alisema kuwa, mishahara yao isikatwebali wapewe fursa ya kujiunga ma mifuko mingine.

Akizungumza kwa naiaba ya wasafiri wenzake Bi Anitha Sanga alisema kuwa, mgomo umesababishia hasara nyingi ikiwemo kukwama kwenye shughuli zao walizotarajia kuzifanya.


1 comment:

  1. Ama kweli kila mahali sasa itakuwa ni mgomo na tusubiri tuone!hakuna uwajibikaji ni siasa tuu na ripoti za kupika,imefika wakati wa kuwaondoa CCM madarakani kwani ukweli wameshindwa kila kona,haya shime wananchi msiogope au kutishwa kuhusu mabadiliko wakati ndio huu.

    ReplyDelete