*MAT: Hatarudi nyuma hadi mawaziri wang'oke
*Amana huduma zasimama, Muhimbili hali tete
*Waomba radhi wananchi, wasema nia yao nzuri
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akikabidhi Ripoti ya Utawala Bora iliyoandaliwa na Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM), Tanzania kwa kiongozi wa Jopo la Wataalamu wa Masuala ya Utawala Bora (CRM) Afrika, Bw. Akere Muna, ambao wapo nchini kwa ajili ya kupitia ripoti hiyo na kutoa mapendekezo juu ya hatua muhimu zinazopaswa kuchukuliwa na Serikali. (Picha na Tagie Mwakawago).
Rehema Maigala na Rachel Balama
MADAKTARI nchini wameanza mgomo usiokuwa na kikomo kama walivyokuwa wameazimia baada ya Rais Jakaya Kikwete kukataa kuwaondoa kazini Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Haji Mponda na Naibu wake, Dkt. Lucy Nkya.
Mgomo huo umeanza ikiwa ni siku moja tangu Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, atangaze msimamo wa Rais Jakaya Kikwete, kuwa hawezi kuwaondoa mawaziri hao kwa shinikizo la madaktari hao.
Kuanza kwa mgomo huo kumesababisha huduma kusimama kwa zaidi ya asilimia 80 kwa baadhi ya hospitali huku vitengo vya mapokezi ya wagonjwa vikiwa havina watu.
Wakati mgomo huo ukiwa umeanza kwenye baadhi ya hospitali nchini, jijini Dar es Salaam viongozi wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) wamesema madaktari kote nchi wataendelea na mgomo hadi pale Serikali itakaposalimu amri na kuwafukuza kazi mawaziri hao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Rais wa MAT, Dkt. Namala Mkopi, alisema; "Tumesikitishwa na kauli ya Waziri Mkuu (Pinda) ya kusema kuwa hafahamu dai la wao kutaka mawaziri hao waondolewe na badala yake anasema ni dai jipya."
Alisema Februari 9, mwaka huu katika mkutano wao na Bw. Pinda, waziri huyo alisema anaanza kwa kuwawaibisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi. Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Deo Mtasiwa, ili kupunguza migogoro iliyotokea.
Dkt. Mkopi aliongeza kwamba kwa upande wa mawaziri, Bw. Pinda aliwaambia kuwa kwa kuwa viongozi hao ni wa kisiasa suala hilo atalifikisha kwa Rais.
Alisema kitendo cha serikali kushindwa kulifanyia kazi dai lao hilo, kumewafanya kukosa uvumilivu.
"Kama kuvumilia, tumeishavumilia mwezi mmoja sasa ni bora ingekuwa mshahara tungevumilia kwani tunajua bajeti bado lakini kwa hawa mawaziri (Dkt. Mponda na Dkt. Nkya) wanaoonekana machoni hatukubali kurejea kazini."
Alisisitiza kuwa mgogoro huo usingefika hapo ulipo kama busara ingetumika. "Serikali itumie utawala bora kuwaondoa hao mawaziri," alisema. Alienda ndani zaidi kwa kufichua siri kuwa mgomo huo umeanza baada ya kupata baraka kutoka kwa madaktari bingwa ambao walikuwa na mkutano juzi asubuhi.
Kwa msingi huo alisema mgomo huo una baraka zote kwa kuwa madaktari wamebaini serikali inataka kuingiza siasa kwenye taaluma hiyo nyeti kwa maisha ya binadamu.
Aliwaomba wananchi wasiwaelewe vibaya kwani lengo lao ni kuboresha huduma ya afya nchini, kwani hata wakilazimishwa kwenda kufanyakazi, hakuna kitu kitakachoendelea kwa kuwa hospitali haina vifaa, vitanda wala dawa.
Walipoulizwa mawaziri wakifukuzwa watarejea kazini, madaktari hao walisema; "Mawaziri hao wakiondoka tunarudi kazini mambo mengine tutaongelea mezani...waziri alituahidi kusafisha wizara ya afya, sasa haijasafishika kama mawaziri hao bado wapo ofisini."
***Hali ya utoaji huduma Muhimbili
Hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jana ilianza kudorora kwani wagonjwa wengi waliokuwa wakifika hospitalini hapo walikuwa wanapangiwa tarehe ya mbali kwa madai kuwa madaktari wapo kwenye vikao.
Hali hiyo iliwanyong'onyesha wagonjwa pale walipokuwa wakiondoka hospitalini hapo bila huduma yoyote. Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Uhusiano wa Taasisi ya Mifupa (MOI), Bw. Juma Almasi;
"Ni kweli madaktari leo wapo kwenye vikao ndiyo maana baadhi ya wagonjwa hawakupata huduma, lakini hakuna mgomo wowote unaoendelea," alisema, Bw. Almas.
Hali katika hospitali ya Amana
Katika Hospitali ya Amana ya Jijini Dar es Salaama mgomo huo ulionekana kuathiri utoaji huduma kwa asilimia zaidi ya 80 na kusababisha wagonjwa kuondoka bila kupata huduma.
Hali hiyo ilisababishwa na madaktari kutokuwepo kwenye vyumba vyao vya kutolea tiba na wale wachache walioonekana walikuwa wakiuliza wagonjwa waliokaa kwenye mabechi kwamba hakuna huduma.
Waandishi wetu waliofika hospitalini hapo walishuhudia wagonjwa waliokuwa wodini wakilalamika kukosa huduma. Wodi zingine zilikuwa na wauguzi peke yao.
Katika wodi ya wajawazito alikuwemo muunguzi mmoja ambaye alikataa kutaja jina lake akifanyakazi ya kupokea wajawazito, japo hakukuwa na watu wa kuwahuduma.
"Tunapokea wajawazito lakini hakuna huduma kwa kuwa madaktari wamegoma, hatuwezi kufanyakazi bila madaktari," alisema muuguzi huyo.
Kwa upande wa eneo wanapokaa wagonjwa wa nje watu waliofika walikuwa wakitangaziwa kwamba hakuna huduma, hivyo kulazimika kuondoka.
Mgonjwa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maimuna Suleiman, alisema kuwa wodi ya watoto wachanga waliozaliwa wakiwa wanaumwa madaktari hawakupita na mbaya zaidi wagonjwa alikuwa wakiruhusiwa na wauguzi.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Dkt. Aisha Mahita, alithibitisha kuwepo kwa mgomo. Hata hivyo alisema Manispaa kwa kushirikiana na uongozi wa hospitali watajitaidi kuhakikisha wagonjwa wa dharura wapata huduma.
Alisema watachukua madaktari waliopo kwenye zahanati na vituo vya afya kwenda kuongeza nguvu Amana.
Nchi hii inafanya kazi kisiasa,bila kujali taaluma.Ovyoooooo.Subirini 2015.Chadema Oyeeeeeeeeeeeeeee.
ReplyDeleteMbarikiwe.
Ukweli inabidi sasa kama nchi wananchi tuingie kwenye mgomo mkubwa na tuazimie kuukataa uongozi uliopo kwani hauna dhamira ya kweli ya kuwasidia wananchi angalieni Uganda mawaziri zaidi ya wanne wamekwisha kujiuzulu Tanzania kuna nini?siasa tu basi.Hivi hakuna waziri Tanzania anaewajibika hata kwa makosa ya wazi?ama hii ndio Tanzania
ReplyDeletemaoni ya chura
DeleteNaungana na msemaji wa kwanza na wa pili.Serikali yetu sasa imedhihirisha kuwa iko kwa maslahi yake binafsi na walio madarakani na sii kwa maslahi ya Watanzania.Ni wakati muafaka kwa Watanzania kuungana na Madaktari kudai haki zetu za msingi na sii afya tu bali hata Elimu ,Maji,Umeme na Barabara.
ReplyDeleteacha siasa. ongea kitaaluma. au na wewe ni daktari?
DeleteTuingie mtaani haraka tuandamane nafikiri tuliowapa madaraka hawajui wajibu wao. Jamani tuunge mkono madaktari.
ReplyDeleteThe doctors need too much than the government can afford
DeleteNaungana na msemaji wa kwanza kuwa kweli viongozi wetu wanalinda maslaha yao na sio maslaha ya walio wengi wala doctors they dont need too much which the government cant afford ndugu zangu acheni kutawaliwa akili ccm itawaburuza maisha hebu badilisheni muone mambo na kama hayakuwa vumilieni miaka 5 mengine muwaondowe hao mlowabadilisaha muweke wengine muone kama hawatofika hata kusamehe posho zao wakakutendeeni mazuri na nyie wengine acheni siasa vile vile mgomo ni haki yao mimi mwenyewe nilikuwa namgonjwa muhimbili hali halisi nimeiona wagonjwa mpaka chini dawa hakuna unaandikiwa ukanunue ukiwakabidhi wauguzi baadhi yao hampi mgonjwa wako na mengi mengineo ambayo kwa serikali inayojivuna imeleta maendeleo imewaletea wenye pesa maskini afe .
DeleteTuingie mtaani haraka tuandamane nafikiri tuliowapa madaraka hawajui wajibu wao. Jamani tuunge mkono madaktari.
ReplyDeleteMaoni yko potofu
DeleteSIJAWAHI KUSIKIA MADAKTARI WA NCHI ZINGINE WANAGOMA. NI TANZANIA TU.
ReplyDeletejE WEWE UNAWEZA KUMWONW MWENZAKO ANAUMWA HALAFU UKAGOMA KUMSAIDIA?
UNAWEZA KUONA MWENZIO ANAKUFA HALAFU WEWE UKAGOMA KUMUHUDUMIA?
MADAKTARI WANAJITAPA KUWA WAO WANA ROHO NGUMU. WAnaweza KUMWACHA MTU AFE KWA KUA WAMEZOEA KUONA WATU WANAOKUFA
Tanzania's doctors are unprofessional. They are politicians
DeleteNdugu yangu naona weww umelalaga na kukoromaga madaktari wa nje wanagoma au husikilizi habari tena wao wangoma kwa maslahi yao zaidi kuliko vitendea kazi amka ndugu yangu hao viongozi wa tanzania nao wamezidi washazoea kusikia watu wangapi wamejufa kwa maafa haya na yale na kutoa mkono na pesa mbili za rambi rambi hawana lolote kama kweli wanuchungu na vifo hivyo basi haraka wanatikiwa waweke kiti moto tena kiwe live wawaulize masuala kwanini wamefikia hatua ya kugoma na sio kuwaburuza mahakamani au kulaumiwa na watu wachache kama nyie wenye pesa zenu mnajua mnaweza kuafford matibabu kwenye spitali za binfsi kama kweli mnaona uchungu na nyie mnatakiwa mshinikize mawaziri husika waachilie ngazi na watakopewa madaraka mfanye ufuatiliaji matakwa yao yasikilizwe hasa kwa upande wa vitende kazi halafu madaktari wakigoma tutajua Tanzanian'doctors are very professional kwani watibu chanzo cha ugonjwa na sio kama madaktari wa baadhi ya nchi za ulaya wanaokumiminia madawa hata kama yanaside effect hawajali nendeni mkatembee muone madaktari wa Tanzania wanastahili sifa wanachohitaji ni vitendea kazi vya kisasa muone kama atasafirishwa mtu kwenda nje au iwe kwa utashi wake mwenyewe walaumuni wanasiasa wanaokuvurugeni akili watanzania wenzenu tukioko nje tuko tayari kurudi makweti ili tuwe magavana wazuri wa kukuelimisheni na kuwapa changa moto serikali yoyote ile itakayokuwa madarakani pindi tukihakikishiwa usalama wetu na hapo ndio penye ugumu serikali ukiokosowa itakutafutia mizengwe uonekane umeshakufa tunakuombeni msiliamu upande mmoja .
Deletekwa serikali ya tanzania mawaziri wa afya ni bora kuliko maisha ya watanzania. Mzee mwinji alijiuzulu kwa makosa ya mauaji SHINYANGA ambayo yeye hakuhusika. mawaziri hao wa afya wangeiga mfano huo wa kuwajibika ili kuokoa maisha ya watanzania.
ReplyDeletechonde chonde tuokoeni kwa nyie kujiuzulu
Ina maana kwa madaktari ni bora wagonjwa wafe kuliko uwepo wa mawaziri wa afya?
DeleteMadaktari wana ROHO MBAYA. Ni wabinafsi na wanadhalilisha taaluma yao
ReplyDeleteHao wote wanolaumu mgomo wa madaktari au wanaosema ni Tanzania tuu madaktari wanagoma hata hajijui yuko ulimwngu gani Tanzaniz ina viongozi wasiojali maslahi yenu mnaowachaguwa na kwa vile hataki kubadilisha uwongozi huo mtabakia maisha na migomo nadhani wewe hujapata kuwa na mgonja ukaiona joto ya jiwe ndo maana au ni mtoto wa mkubwa fulani na wewe unatibiwa katika private hospital kama wao wenyew wanvyopelekana marekani uingereza na kwengineko ndo maana taaluma zote tanzania zinadharauliw sio elimu udaktari tu na mengineyo wamejikita kuimarisha chama zaidi na sio wananchi na vile tkubali ukweli asilimia kubwa ya wapiga kura ndio wasiosoma wanaendelea kuburuzwa. na kwanini mnawalaumu madaktari na wanasiasa mnawaacha nyuma hawana uzalendo wako kwa binfsi zao na jamaa zao wachache kasome udaktari halafu ufante kazi tanzania na nakuombea dua utoke nje ukaone namna taaluma ya madktari inavyoheshimiwa wacha ujinga kuwalaumu madaktari uingereza waligoma pamoja na wauguzi lakini kwa vile serikali kwa kiasi fulani ikachukuwa hatua na kurekebisha vifaa na zana pamoja na mishahara. Na hao mawaziri rogho mbaya kuliko madaktari kwani wakionyesha mfano wakajiuzulu itakuwa mwisho wa maisha yao nawaunga madaktari wao mgomo wao wanadai vitendea kazi na sio mshahar acha kasumba hizoo.
Deletena wewe kasome udaktari uonje joto la jiwe. madaktari wa tanzania wanafanya kazi kwenye mazingira magumu, hakuna vifaa/ vitendea kazi vya kutosha hivyo kufanya huduma yake kuwa duni na serikali inatumia pesa nyingi kwa masuara yasiyo ya msingi
ReplyDeleteMuda umefika wa kuwatia makofi madaktari wetu Kwa kuwa wamekosa akili. Wanawauwa wanaotarajia wawaunge mkono yaani wananchi. Halafu wanatoa rufaa kwa mawaziri waende wakatibiwe nje ya nchi . Wana akili kweli kwa hili? Wangekataa kutoa rufaa na wakakataa kuwahudumia viongozi kwanza> Haziwatoshi kabisa na kwa hili wasiongee kwani siku moja pale muhimbili tutawashauri wenye wagomjwa wao wahakikishe kila daktari anatoka na ngeu halafu tutaona watatibiwa wapi
ReplyDeleteWakwansengero kama kuwapiga makofi au kuwatoa ngeu ni Viongozi wanokula viapo na kutowa ahadi za uwongo sasa kam kweli wewe una uwezo wa kuwapiga wenye taaluma makofi kampige waziri kwanza nadhai hamfahamu kama kuna kitu kinaitwa sacrifice na hii iko namna mbili ama moja ni kugoma kuhudumia wagonja which to my view iwe ni last resolution na ndio iliyotumika hapa ama ya pili kulalam kwa vionozi lakini jee tujiulize tanzania tunao viongozi ambao wafanya maamuzi kwa malalamiko ya umma jibu hatuna sasa huu mgomo ndio sahihi kama kweli viongozi mliowachaguwa ni wakweli na wanaimani basi na wao waache roho mbaya wajiuzuli zazn na vitendea kazi pamoja na madawa yamiminwe mahospitali wache upumbavu wa kufanya masherehe ya upuuzi ambao yanapoteza mamilioni ya fedha hujapata nini wewe kuwa na monja au hat hujaumwa wewe au unapesa za kwenda private hukijui kinachowapata maskini za Mungu walala hoi wanpoumwa funukeni akili na acheni kutawaliwa kimazo .
ReplyDelete