WANANCHI mkoani Morogoro wametakiwa kushirikiana kikamilifu na Jeshi la Polisi katika kupambana na vitendo vya uhalifu vikiwemo ujambazi, maujaji na utumiaji wa madawa ya kulevya kutokana jeshi hilo kuhitaji nguvu ya ziada ili kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa.
Mwito huo ulitolewa jana na Mkuu wa mkoa huo, Bw.Joel Bendera wakati akifunga mafunzo ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kwa wananchi wa Kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro.
Katika mafunzo hayo jumla ya wananchi 47 walihitimu mafunzo hayo liliwapongeza kwa kuwa tayari kujitolea kushirikiana na jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu ambao kwa kiasi kikubwa unatishia usalama wa rai.
Bw.Bendera alisema, kuwa idadi ya askari polisi pamoja na vitendea kazi haitoshelezi hivyo ipo haja kwa viongozi wa kata na mitaa kuwahamasisha wananchi kulisaidia Jeshi la Polisi kwa kulinda usalama wao na mali zao.
Aliwaomba, wadau mbalimbali mkoani hapa kukisaidia kikundi hicho cha ulinzi shirikishi kupata vifaa vya kufanyia kazi kuwa mstari wa mbele kushirikaiana nao katika suala zima la ulinzi shirirkishi.
Aidha, aliwataka wananchi kujenga tabia ya kuwafichua wahalifu mbalimbali wakiwemo wa ujambazi huku akiwaonya baadhi ya askari kuacha tabia ya kuvujisha siri za watoa taarifa kwani zinaweza kuvuruga amani.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha polisi jamii mkoani hapa Inspekta Idd Ibrahim alisema, mafunzo hayo ni ya kwanza katika kata hiyo kwa mwaka huu hata hivyo lengo la jeshi la polisi ni kutoa mafunzo kama hayo katika kata nyingine za Manispaa ya Morogoro.
Inspekta Idd alisema, mafunzo hayo yaliyoendeshwa kwa mwezi mmoja yalilenga kuwafundisha mambo mbalimbali ikiwemo dhana ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi, ukamataji salama na upekuaji chunguzi wa makosa ya jinai, haki za mtuhumiwa baada ya kukamatwa na namna ya kujenga ushahidi wa kesi.
Hata hivyo, Inspekta Idd alisema kuwa kikundi hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utendaji wao wa kazi ikiwemo ya ukosefu wa vifaa vya kufanyia kazi kama filimbi, tochi makoti, buti, vitambu vya mahudhirio, sare na ukata wa fedha za kujikimu.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Bw.Samuel Msuya alilipongeza jeshi hilo kwa hatua waliyofikia ya kuwashirikisha wananchi katika ulinzi kwa kupitia dhana ya polisi jamii kwani wahalifu siku zaote wanaishi katika jamii
Hata hivyo Diwani huyo aliwataka wananchi wa kata hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha na kikundi cha ulinzi shirikishi kilichoundwa ndani ya kata kwa kutoa taarifa za uhalifu na panapotokea tatizo la uhalifu wasiwafiche wanaohusika kama wanafahamika kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kuchangia kuleta maendeleo.
****************
3THIRD
Fidelis Tairo akanusha
kuhifadhili mahakama
DIWANI wa Kata ya Kingo, Bw.Fidelis Tairo amekanusha uvumi uliokuwa ukienezwa kumiliki Mahakama ya Mkoa wa Morogoro kwa kutumia vibaya uongozi wake katika kuingilia shuguhuli za mahakama hiyo hususan kutoa misaada mbalimbali kwa lengo la kuonekana kama yeye ni sehemu ya chombo hicho cha dola.
Akizunngumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Diwani huyo alisema, kumekuwa na makundi mbalimbali ndani ya kata yake yanayomshutumu kwa mambo ya hapa na pale kwa lengo la kumchafua kisiasa ili asionekane mtendaji mzuri wa kazi za kuhudumia jamii.
Bw.Tairo alidai kuwepo watu wasiomtakia mema wakipita sehemu mbalimbali ndani ya kata na nje ya kata yake wakitangaza kuwa yeye amekuwa akitoa misaada mbalimbali katika mahakama (mahakama ya mwanzo) na kupelekea yeye kuwa na sauti katika mahakama hizo.
“Napenda niwafahamishe wananchi na umma kwa ujumla kuwa, sijawahi kutoa msaada wowote katika mahakama za Morogoro Mjini, kwa maslahi yangu binafsi na pia sina sauti wala nguvu yeyote katika mahakama hizo," alisema Bw.Tairo.
Aidha, alibainisha kuwa Mahakama ni chombo ambacho ni huru na hakiwezi kuingiliwa na chombo chochote iwe Bunge ama Serikali na hivyo kuwataka wananchi wa Manispaa ya Morogoro wapuuzie uvumi huo unaosambazwa na watu wasiopenda maendeleo katika jamii kwani wengi wao ni makundi ya kuchafuana kisiasa.
Aliongeza kuwa shughuli za maendeleo katika kata zinaletwa na wananchi kwa kushirikiana na viongozi wa kata kuanzia diwani hadi watendaji wa chini na hivyo kwa kushirikaina na watendaji wake walifanikiwa kuweka kibao kinachoelekeza Mahakama ya Nunge ilipo katika kata yake na ndipo wananchi wasiopenda maendeleo wakaanza uvumi wa maneno kwamba diwani amekuwa sehemu ya mahakama.
Hata hivyo aliwataka wananchi wa Kata ya Kingo na Manispaa ya Morogoro kwa ujumla na kutojiingiza katika makundi ya watu wasiopenda maendeleo, wasioshirikiana na viongozi wao katika katetea maslahi yao na kukaa vijiweni na kuanzisha majungu kwa viongozi ili wasionekane watendaji wazuri katika kutatua changamoto mbalimbali za jamii.
No comments:
Post a Comment