06 March 2012

Mbaroni kwa kulawiti watoto tano

*Wana umri wa miaka 8 hadi 12, wananchi wamshambulia
 Na Faida Muyomba, Geita

MKAZI wa Kijiji cha Nyamalembo, Wilaya ya Geita, mkoani Mwanza, Bw. Mbaga Julius (25), anashikiliwa na Jeshi la Polisi akituhumiwa kulawiti wanafunzi watano wa Shule ya Msingi Mseto, iliyopo mjini hapa.

Wanafunzi hao ambao ni wavulana (majina yamehifadhiwa) wenye umri  kati ya miaka nane hadi 12.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya jeshi hilo, zinasema tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki saa mbili asubuhi katika eneo la Mtaa wa Nyamalembo.

Taarifa hizo zimedai kuwa, Bw. Julius alikamatwa na jeshi hilo kwa kushirikiana na baadhi ya wazazi wa watoto hao. Baada ya kukamatwa, alikutwa na wanafunzi wengine wanne katika himaya yake na anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Mmoja kati ya wazazi wa watoto hao (jina tunalo), mkazi wa Mtaa wa Bomani, wilayani hapa, alisema baada ya kuona mabadiliko ya mtoto wake katika masomo, aliamua kufuatilia kwa walimu ili kujua tatizo linalomrudisha nyuma kimasomo.

“Baada ya kufuatilia, walimu walinieleza kuwa mtoto wangu ni miongoni mwa wanafunzi ambao hawafiki shuleni hivyo niliporudi nyumbani, nilimbana na kumuuliza kwanini haendi shule ndipo akaanza kutoa siri nzito,” alisema.

Alivitaka vyombo vya dola, kutenda haki kwa kuhakikisha mtuhumiwa anafikishwa mahakamani kwani watoto waliofanyiwa kitendo hicho wameathirika kisaikolojia.

Baadhi ya watu walioshuhudia tukio la kukamatwa kwa mtuhumiwa, walisema Bw. Julius nusura auawe na wananchi ambao walianza kumshambuliwa kwa mawe kabla ya kuokolewa na polisi.

Mwandishi wa habari hizi, alipomtafuta Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Deusdedith Nsimeki, ili kuzungumzia tukio hilo, simu yake ya mkononi ilikuwa imefungwa.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Barlow, alisema hana taarifa za tukio hilo kwa kuwa yuko nye ya Mkoa kikazi.

“Niko safarini, mtafute RCO, Nsimeki ndiye anakaimu nafasi yangu,” alisema, Kamanda Barlow.


1 comment:

  1. wekeni Kurasa(Page) yenu facebook.... share tu haitoshi...

    pia ninyi ni gazeti kubwa san jitahidini kuwa na website na si blo ili tuweze kupambana katika dunia ya utadawazi

    ReplyDelete