Na Willbroad Mathias
ASKARI wa vikosi vya zimamoto nchini wametakiwakubadilika ili waweze kwendana na tekonolijia mpya ya vifaa vya kupambana na majanga ya moto.
Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaama na Katinu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani,Bw.Mbarak Abduluwakil wakati akizundua kifaa kipya cha kuzima moto kiitwachwa DASPA 5.
Bw. Abduluwakil alisema kuwa kadri siku zinavyokwenda kumekuwepo na mabadiliko makubwa kitenolijia na hivyo wanatakiwa kwenda nayo ili kuweza kukabiliabiliana na majanga ya moto.
"Mnatakiwa kubadilika kwani teknolojia inakua kila kukicha na endapo mtafanya hivyo mtaweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa,"alisema Katibu Mkuu huyo.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Kampuni ya You are Solution Tanzania ambao ndiyo waagizaji wa kifaa hicho Bw.Damian George ,alisema endapo kitatumiwa ipasavyo kitasaidia kupunguza matumizi makubwa ya maji.
Alisema kuwa kifa hicho kimetengenezwa kwa teknojia ya kisasa ili kukabiliana na majanga ya moto.
Nukubali Kifaa hicho cha kuzima moto ni kizuri lakini kesho tusilazimishwe kupitia Wizara yako kukinunua. Tafuta na vingine ututangazie ili tuchague madukani. Tangaza na MAKAMPUNI mengine yenye kifaa hicho ili kuwe na ushindani.
ReplyDeleteMtindo huu unaonyesha unatengeneza njia ya MSHIKO.