Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, amesema ataendelea kusimamia
sheria ya barabara namba 30 ya mwaka 1973 hadi anaingia kaburini kwa
kuhakikisha hakuna magari ambayo yanazidisha uzito na kuharibu barabara, anaripoti
Goodluck Hongo.
Dkt. Magufuli aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika hafla ya
kutilia saini mikataba mitatu ya ujenzi wa barabara za Dodoma- Manyara inayopita Mayamaya-
Babati-Bonga.
Barabara
nyingine ni Tunduru- M a n g a k a - Mtambaswala na kusema kuwa, barabara hizo
z i n a j e n gwa kwa gharama kubwa hivyo watendaji wote wa Wizara ya Ujenzi
kupitia
Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS), wanapaswa kusimamia sheria.
Alisema usimamizi makini wa sheria za barabara, utasaidia
kuzifanya zidumu zaidi kwani Rais Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara hiyo
kusimamia sheria ambapo kitendo cha wamiliki wa magari kuzidisha uzito,
kinamchukiza sana.
“Sipo tayari kuona matajiri wachache wakiharibu barabara na
kujipatia faida kubwa wakati barabara hizi zinajengwa kwa mkopo unaolipwa na
kodi za wananchi.
“Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, mimi nitaendelea kusimamia sheria
hadi naingia kaburini kwa kuhakikisha hakuna magari yanayozidisha uzito na
kuharibu barabara,” alisema Dkt. Magufuli.
Aliongeza kuwa, kama matajiri hao
wataachiwa waendelee kuzidisha uzito, barabara zilizopo hazitadumu kwa muda
mrefu na wananchi maskini wataendelea kulipa kodi.
“Nchini Ujerumani, uzito wa magari yote ni tani 40, Uingereza tani
40, Ufaransa 40, Urusi 38 lakini Tanzania tani 56, wakati mwingine tunakamata
hadi tani 96,” alisema.
Akiwazungumzia wakandarasi waliochukua zabuni ya ujenzi wa barabara
hizo, Dkt. Magufuli aliwaonya na kusisitiza kama
hawawezi kazi ni bora wasisaini mikataba hiyo ili watafute wakandarasi wengine
wenye uwezo.
Alisema kama wamekubali kusaini, wanapaswa kuanza kazi mara moja
kwani Serikali ndio iliyokopa na walipakodi ni Watanzania hivyo si kukaa miezi
sita ndio waanze kazi.
“Mameneja wa TANROADS katika mikoa ambayo miradi hii inafanyika,
lazima msimamie kikamilifu ujenzi huu na kama
mradi ukisuasua katika eneo lako ujue hutufai kufanya kazi hivyo uondoke mara
moja,” alisema.
Kwa upande wake, mbunge wa Kasulu Mjini, mkoani Kigoma, Bw. Moses
Machali (NCCR-Mageuzi), aliipongeza Serikali kwa kusikia kilio cha wananchi na
kuwajengea barabara na daraja la Mto Malagarasi ambapo yeye si mhafidhina; bali
kama serikali imefanya mema inapaswa kupongezwa.
“Jema ni jema tu hata kama likifanywa na nani hivyo mimi si
mhafidhina, kama Serikali imefanya mema basi
inapaswa kupongezwa,” alisema.
Aliongeza kuwa, licha ya Serikali kuwajengea Daraja la Mto
Malagarasi, bado barabara zingine ikiwemo ya Nyakanazi ina hali mbaya, hivyo
pamoja na kuipongeza serikali kwa kusaini mikataba hiyo, utekelezwaji wake ni
jambo lingine.
“Kusaini mkataba ni jambo moja na Mkandarasi kufika eneo la mradi
ni hatua nyingine, Daraja la Mto Malagarasi halitoshi bali tunaomba Barabara ya
Nyakanazi nayo iwekwe lami,” alisema.
Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Dodoma kwa tiketi ya Chama cha Wananchi
(CUF), Bi. Moza Abeid Said, alisema anaipongeza serikali ya CCM kwa kutekeleza
ahadi zake, lakini zisifanywe karibu na uchaguzi kwani kilio cha barabara hizo
ni cha muda mrefu.
Alisema ingawa yeye ni Mbunge kutoka upinzani, anaipongeza
Serikali hasa inapotatua kero za wananchi bali wasiwasi mkubwa ni utekelezaji
wake kwani wabunge wamekuwa wakilalamikia miradi mingi ambayo imesainiwa lakini
haijatekelezwa.
“Waziri Magufuli ameweza kutekeleza ilani ya CCM katika sekta ya
miundombinu ya barabara... amefanya kazi nzuri, barabara ya Babati-Iringa
ikijengwa kama walivyosaini mikataba, itawasaidia sana
wananchi wa Mkoa wa Dodoma,”
alisema.
Naye Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale, alisema
mradi huo unatekelezwa kwa awamu ya pili ambapo awamu ya kwanza ulitekelezwa
kwa mkopo wa sh. bilioni 472 na awamu ya utatekelezwa kwa gharama ya sh.
bilioni 538.88.
Alisema
fedha zimetoka katika Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na nyingine kutoka
Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ambapo fedha nyingine zimetoka serikalini.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wabunge wote kutoka mikoa ya Manyara, Dodoma, Mtwara na Ruvuma ambao miradi hiyo inapita katika
majimbo yao.
NI VILE TU MAGUFULI RAIS KIKWETE ANAKUPIGA TAF ISINGEKUWA HIVYO VIKWAZO UNAVYOPATA UNGEJIUZULU
ReplyDeleteHongera mzee Magufuli, Rais Mh.Kikwete akiwahutubia wananchi eneo la barabara ya kwa sadala Masama na baadaye ielekee Siha. Ulitoa siku 30, sasa yapata miaka miwili. Hakuna kilichofanyika. Wananchi wanaoishi kando ya barabara ya Bomangombe Kuelekea. Sanya juu walifanyiwa kiini macho mwaka na nusu sasa kwa maelezo wasindeleze maeneo yao hadi leo hatujui kinachoendelea. Baba njoo huku kutengua hiki kitendawili. Tujue la kufanya.
ReplyDeleteKWA KELI MAGUFULI UNAJITAHIDI SANA KEEP IT UP
ReplyDeleteYec lazima ujue wajibu wako
ReplyDelete